(MUHIMU)Trafiki wa Ubungo KERO!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

(MUHIMU)Trafiki wa Ubungo KERO!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee wa Gumzo, Jul 21, 2008.

 1. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #1
  Jul 21, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watumiaji wa barabara ya mandela hususani kutokea buguruni, tabata na mabibo kuelekea ubungo wanalijua hili la hawa trafiki.

  Kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiendesha shughuli zao za 'kiusalama' eneo linalotizamana na SONGAS.Awali tulijua kuwa ukaguzi waliokuwa wanaufanya ulilenga kugundua kasoro zilizozopo kwenye magari ya mizigo na daladala.Magari yalikuwa yanasimamishwa eneo nililolitaja na trafiki wanachukua muda mfupi kukagua kisha daladala linaingia kituoni.Wakati mwingine abiria wenyewe tulikuwa tunaamua kushuka kwa kuwa eneo lenyewe siyo mbali na kituo cha daldala.

  Kwa sasa hali imebadilika na kile tulichokuwa tunakiona kuwa ni ukaguzi sasa ni BIASHARA.Kila siku asubuhi trafiki hujipanga pale ubungo na kuisimamisha kila daladala inayopita pale.Yafuaatayo hujitokeza:
  a)Kila trafiki anajitahidi kusimamisha daladala nyingi iwezekanavyo na kila mmoja anaelekeza daldala zake zisimame eneo analotaka yeye trafiki.
  b)Trafiki haji kukagua gari mpaka abiria wote washuke na kuondoka.
  c)Kadri siku zinavyokwenda ukaguzi haufanyiki bali kondakta na dereva au kondakta peke yake anamfuata trafiki alikosimama na baada ya muda mfupi wanaruhusiwa kuondoka.

  Alhamisi ya wiki iliyopita daladala niliyokuwa nimepanda ilisimamishwa lakini dereva hakusimama.Nilimuuliza kwa nini hakutii akanijulisha kuwa wameshawazoea matrafiki hao na wanajua wanachokitaka.Hakuficha kuwa kila trakifi pale anataka fedha la sivyo daladala itapata taabu siku nzima barabarani.

  Leo asubuhi tena daladala niliyopanda ilisimamishwa dereva akasimama.Abiria tukashuka lakini mimi sikuondoka bali nilijivuta taratibu alipokuwa trafiki aliyesimamisha daladala ile.Alikuwa anamlalamikia kondakta wa ile daladala kwa kuwa ijumaa iliyopita hakumletea fedha kama walivyokubaliana.

  Uchunguzi wangu umebaini kuwa kila daladala ina trafiki wake na wakati mwingine daladala inaposimamishwa huwa haisimami kwa kuwa dereva na konda wake wana utaratibu wa kumpa mshiko trafiki wao muda wowote hata baada ya kazi.

  Utaratibu huu umesababisha KERO zifuatazo kwa RAIA:
  a)Kucheleweshwa barabarani bila sababu za msingi.
  b)Abiria wanashushwa mbali na kituo cha daladala.Sasa hivi hali ni mbaya kwa kuwa trafiki wanalikimbia eneo la karibu na Songas na wamesogea mpaka karibu na daraja (Riverside).Abiria wenye mizigo wanalazimika kutafuta mikokoteni au wabebaji.

  Hii ni RUSHWA na hatua zisipochukuliwa tutaendea kuonewa mpaka tunaingia kaburini
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2008
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hali ni hiyo hiyo pale BANANA Ukonga kwa daladala BUBU zinazoelekea Kitunda, Nyantira, Machimbo. Hapo hata jamaa wa SUMATRA wana mgao wao. Kaazi kwelikweli Nchi hii.
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni NJAA inayo sababishwa na serikali yenu kuwalipa 85000/= kwa mwezi kisha anafamilia ndani anasomesha ana ndugu wanao mtegemea anatakiwa ale+avae+anywe+ahonge vimada.Kwa hiyo inabidi atumie ubongo wake ipasavyo ili aishi na aendelee kuwepo mjini.Hii ndo Bongo mkuu serikali inapaswa iboreshe mishahara ya wafanyakazi na sio kupiga kelele weee sasa wasipo chukua kidogo hapo we unafikiri wataishi vp hawa???Na kugoma hawawezi kutokana na uwoga wetu waTZ.
   
 4. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #4
  Jul 21, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ebwana kweli wee!Njaa ndio tatizo na naugana na signature yako, hwawezi kuung'ata mkono unaowapa kula wasije kosa kula yao kesho.
  Wenye meno ndio wanaotafuna nchi kweli.
   
Loading...