MUHIMU: SOMA, SAIDIA, Mtanzania mwenzetu anateseka ............ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MUHIMU: SOMA, SAIDIA, Mtanzania mwenzetu anateseka ............

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VIKWAZO, Jul 10, 2011.

 1. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Abbas: Mguu wagu unanitesa, nisaidieni jamani[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  mwenye uwezo wa kusaidia awasiliane kwa namba 0786272409 au 0655304336


  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 10 July 2011 10:27[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][​IMG]
  Abas akiwa amejipumzisha nyumbani kwao.​
  Na Julius Magodi(gazeti mwananchi)

  ABBAS Abdalaah (31) aliapoanza kuvimba uvimbe mdogo katika mguu wake wa kulia hakujua kuwa ulikuwa ni mwanzo wa ugonjwa ambao hatimaye ungemfanya ashindwe kutembea.Ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujulikani, umemfanya Abbas kulala kitandni muda wote akilazimika kubebwa na watu watano kumpeleka nje kujisaidia.

  Matumaini aliyokuwa nayo ya kupata tiba ya ugonjwa wake, yameanza kutoweka baada ya msamaria aliyejitokeza kumpeleka Hospitali ya Seliani mjini Arusha kushindwa kutimiza ahadi yake.

  , ndizo anaona zimesababisha mpaka sasa asipate msaada.

  "Vurugu hizi zilizoaanza Machi mwaka huu , ndizo zilizosabisha leo niwe bado hapa sina msaada, kwani mmoja wa wawekezaji katika Bonde hili alikuwa ameaahidi kunisaidia kunipeleka hospitali ya Seliani," anasema kwa uchungu akiwa amelala katika kitanda chake kilichopo sebuleni kwenye nyumba ndogo ya nyasi ya Bibi yake, Zuhura Abdalah.

  [​IMG]Akisimulia historia ya ugonjwa wake huo, anasema alianza kuvimba kiumbe kidogo katika mguu wake mwaka 2005, wakati huo akiwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu kijiji hapo.

  Anasema hakuwa na wasiwasi kwamba huo ungekuwa ugonjwa mkubwa ambao ungemfikisha hapo alipo.

  Taratibu mguu ulianza kuvimba, hali ambayo ilimfanya baba yake mzazi, mzee Abdallah Juma mwaka 2008, kumpeleka Hospitali ya Hydom, Wilaya ya Mbulu ambako baada ya kumchunguza hawakuona ugonjwa, ingawa mguu ulikuwa umevimba.

  "Hydom hawakuona ugonjwa, nikawauliza mbona bado mguu umevimba kwa nini hamuoni tatizo, wakanishauri nirudi nyumbani, " anasimulia kwa uchungu kijana huyu mchangamfu.

  Ingawa madaktari katika hospitali hiyo hawakuona tatizo lolote katika mguu wa Abbas, lakini mguu mzima ulizidi kuongezeka unene, mwaka 2009 wazazi wake wakaamua kumpeleka Hospitali ya Mission ya Dareda, Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

  Huko waligundua alikuwa na matatizo katika seli za mwili hivyo wao hawakuwa na uwezo wa kumtibu na kumshauri aende Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

  Anasema mwaka uliofuatia alikwenda KCMC ambako alifanyiwa uchunguzi na matokeo yalionyesha kwamba alikuwa na matatizo ya maji kujaa katika mguu na pia alikuwa na tatizo la nyama kuongezeka katika mguu wake.

  Abbas anasema baada ya kungulika tatizo hilo aliuzwa na daktari wake kama ana uwezo wa kulipia matibabu ya ugonjwa wake nje ya nchi, lakini alisema hana uwezo.

  "Baada ya kueleza kuwa sina uwezo, basi huo ukawa ndio mwisho wa uwezo wao kunisaidia, nilirejea nyumbani nikiwa bado nina uwezo wa kutembea mwenyewe," anasema.

  Hata hivyo akiwa amekata tamaa ya kupata matibabu aliendelea kuishi huku akifanya shughuli zake za kila siku kwani mbali ya mguu kuendelea kuvimba , lakini hukuwa akisikia maumivu.

  Machi mwaka huu ndio mwezi ambao utabaki katika kumbukumbu zake zaidi kijana huyu, kwani ndipo aliposhindwa kutembea na kuwa mtu kulala kitandani.

  Tangu wakati huu kasi ya mguu kuvimba iliongezeka huku akiwa hawezi hata kusimama kwani akitaka kutoka nje ya nyumba anatakiwa kubebwa na vijana watano wenye nguvu. Mbali ya kuvimba sasa ana kidonda ambacho kinamsumbua katika mguu huo.

  Wakati akiendelea kuwaza tiba ya ugonjwa wake, Mei mwaka huu mzazi wake alikwenda kumwomba mmoja wawekezaji katika Bonde lenye mgogoro la Kiru kumsaidia hela za matatibu katika Hospitali ya Selian Arusha, alikubali.

  Hata hivyo, kama waswahili wanavyosema ng'ombe wa masikini hazai , wakati akijindaa kumsaidia mgogoro mkubwa ukaibuka kati wa wananchi wenzake na wawekezaji 19 waliopo katika bonde hili, uliosabisha kuibuka vurugu.

  Vurugu hizo zilizosababisha watu wawili kuuawa na mali za wawekezaji yakiwamo mashamba ya miwa na magari kuchomwa moto, zilifuta matumaini ya kupata msaada huo.

  "Naona huyu mwekezaji amekasirika kutokana na mgogoro au naye kakimbia makazi yake kutokana na vurugu hizi, sasa sina msaada mwingine," anasema kwa masikitiko.

  Anaomba mtu yeyote mwenye uwezo amsaidie kumpa hela za matibabu ili apone na kurejea katika hali yake ya kawaida.

  "Ninaomba watu wenye uwezo wanisaidie kunipatia hela niende hospitali ili nami niwe kama watu wengine jamani, nateseka," anasema.

  Baba mzazi wa Abbas mzee Juma anasema yeye hana uwezo wa kumlipia matibabu ya mtoto wake kwa sababu ya kipato kidogo.

  Anasema yeye ni mkulima ambaye mashamba yake yamechukuliwa na wawekezaji hivyo kumfanya asiwe na kipato chochote.

  Anaomba wasamaria wema kumsaidia mtoto wake ili aweze kurejea katika hali yake ya zamani

  Mzee Juma akiwa amekaa kando kado ya mtoto wake ambaye alikuwa akimsikiliza kwa makini, anasema hivi sasa hawezi kuwa mbali na mtoto wake kwani anahitaji mtu kuwa naye karibu.


  Maoni yangu: mbunge MH kisyeri werema chambiri nina hakika hii iko ndani ya uwezo wako, bakuri lipite hapo dodoma bunge na sisi wananchi pia tutachanga, huyu tunaweza kuokoa maisha yake mbona harusi tunaweza?
  JF tunaweza tufanya ili kwa nguvu zetu au na kumshinikiza mbunge kupitisha bakuli hapo bungeni. hii inawezekana wandugu tusaidie kwa maombi na mali

  kila mwenye credit amtumie message ili aombe msaada kwa wabunge wenzake kwa ajili ya ABBAS, kila hatakaye fanya hivyo na MUNGU ambaliki pale alipopungukiwa,
  tafadhali hata ukitoa jaribu kutuma message kwa huyu mbunge tunaweza kuokoa maisha ya huyu mwenzetu kwa kumshikiniza mbunge kuwa na huruma naye, ili amuombe msaada bungeni au serikalini.


  UPDATE:
  Maxence atapokea michango yote ya wana Jamii Forums.
  Na ata toa report baada ya kupokea michango ...
  Kwa anaye taka kuwasiliana na Maxence directly ..
  Number hii hapa +255713444649 ...(
  0713444649 )

  KUCHANGIA:
  M-PESA: +255 755 642929
  ZAP: +255 784 526 444
  BANK: CRDB - Acc # 01J2092391800 - Maxence M. Melo
  CREDIT Cards:
  https://www.jamiiforums.com/payments.php
  PayPal, send to: mwanakijiji@klhnews.com


  MPAKA SASA: Tumeshapokea TZS 125,000/= (hata michango iliyokuja kuisaidia JF imeunganishwa)
  Watakaochangia zaidi list itawekwa chini hapa, tujitahidi kufikia mwisho wa juma hili tuwe tumewasilisha.

  ====================
  Michango kuanzia Julai 18, 2011

  1. Chakaza - TZS 50,000/=
  2. Kilewo - TZS 50,000/= (kapeleka mwenyewe)
  3. SOMEONE - $100.00
  4. Arabian Falcon - TZS 50,000
  5. Maxence Melo - TZS 100,000
  6. Fidel80 - TZS 30,000
  7. Hakutoa ID - TZS 25,000
  8. Hakutoa ID - TZS 30,000
  9. BAK - TZS 23,000 (hazijachukuliwa, will confirm)
  10. afrodenzi - USD 158.00
  11. Aine - TZS 20,000
  12. First Born - TZS 10,000
  13. SOMEONE - USD 47.00
  ​mods mbalikiwe kwa kazi nzuri
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  shukurani , inatia huruma sana anyaway mimi natajitoa kwa kadri ya uwezo wangu, ili mbunge kuomba msaada bungeni ni muhimu hapo watu wanauwezo posho ni nyingi wachangie na uhai
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  DA! very sorry.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Allah akbar......mwenyezmungu muondolee mtihan mja wako ABAS
   
 5. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mungu wangu!
   
 6. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  POLE SANA,
  Inasikitisha kwa mateso anayopata huyo mgonjwa pamoja na wazazi wake,
  Kwa hali aliyonayo huyo kijana ,wazazi wake hawawezi tena kujishughulisha hata na shughuli za uzalishaji.
  Mbunge wake akilisimamia hili kidete kwa kupitisha bakuli kwa hao wabunge wote naamini huyu kijana atapata matibabu,
  POLE NYINGI SANA.
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  vipi kuhusu mmc,nafikiri hospital yetu kubwa ina wataalam wazuri!!je kuna viongozi wa serikali kama mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa,mbunge/???nafikiri ana haki ya kupata matibabu bure,hela ni zetu,sipendi kutukana lakini ikibidi tutafanya hivyo!
   
 8. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Abbas ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kiru Ndogo, anasema vurugu za wananchi na wawekezaji wa Bonde la Kiru, Wilaya ya Babati mkoani Manyara,

  mbunge wa hapa mahali sio shekifu? na ni mkuu wa mkoa pia?

  wabunge waliopo humu mpe habari hapo mjengoni tafadhali
   
 9. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Vipi tunaweza kusaidia? Tuwekewe contacts na msaidieni ku-organise bank account ambayo watu tunaweza kufikisha michango yetu.
  Poleni sana.
   
 10. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  nadhini kwa hapa invisible au mex wajitokeza watupe jinsi ya kuchangia ili JF na sisi tusaidie kidogo hapo,
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  naomba niweke mambo wazi,kama hizi tktk malecela na pinda wanaenda kutibiwa maukimwi yao ulaya na india kwa mambo ambayo sio serious basi ana haki mara 100apate matibabu bure,tumewakalia kimya sana hawa watu,lazima wafanye hivyo!hela ni zetu!
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Mama yangu mateso gani haya jamani..

  JF tujitolee jamani ..
  muanzisha thread fanya juu chini
  U organize mahali tutatuma kitu kidogo kigodo..

  Tumsaidieni jamani...
  Niko tayari.
   
 13. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Naunga mkono hoja ila la maukimwi silijui, kwa huyo mkuu kupata matibabu ni muhimu
  wakuu nani ana fahamu mbunge wa hapo mahali ?
  hakuna wana harusha humu ndani? hapa tunatafuta wabunge wawili babati mashariki au maghalibi mmoja wao ni muhusika sana hapa.
  bakuli lipite hapo bungeni

   
 14. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  hawa wabunge wanapata fedha nyingi sana na lazima wajifunze kuweka fungu la kufanya kazi kama hizi!
   
 15. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  niko mazingira ambayo siwezi kulifanikisha ili vizuri, nimeomba msaada kwa Invisible
  nasubilia majibu yao wanasema je? bila wao kuwezesha kukusanya hapa hii kitu mimi ninamikono mifupi zaidi
  sipo weza kuwafikia walengwa, kama kuna mtu manyara tafadhali tutafutie mbunge wa hapo mahali website ya bunge inanizingua
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Mwili wote umenisisimka kwa uwoga. Mungu amnusuru huyo kiumbe na hayo mateso. M pesa inaweza kuwa rahisi kwangu kuchangia chochote. Wekeni namba.
   
 17. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  tupo arusha na nafikiri ni jirani sana,tuwapigie kelele hawa watu wanaotakiwa kufanya hiyo kazi,kutoa michango haisaidii kwenye mambo kama haya,kama tuna serikali ifanye hiyo kazi mara moja!kama hatuna serikali na viongozi tutatoa michango!
   
 18. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  je unaweza kujua nani mbunge wa hapo mahali?
   
 19. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  simfahamu mbunge wa eneo hilo,kwa vyovyote atakuwa anatoka ccm
   
 20. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ingesaidia pia kama tukifahamu jina halisi la ugonjwa wenyewe (kwa kitaalamu) na gharama(quote) ya matibabu/operesheni yake na ni nchi gani? Naamini humu ndani kuna madaktari na wadau wa taasisi za misaada (Charities) ambao wanaweza kumsaidia kupatikana matibabu nafuu zaidi na ya uhakika.
   
Loading...