MUHIMU: SERIKALI IINGILIE KATI UTOAJI WA PESA ZA KUJIKIMU VYUONI

stormryder

JF-Expert Member
Mar 23, 2013
2,181
2,494
Kumekuwepo na tatizo linalosababishwa na uongozi wa baadhi ya vyuo nchini kugoma kutoa fedha za kujikimu kwa baadhi ya wanafunzi mpaka wa ingie MIKATABA kandamizi(Ni singependa kuweka wazi hapa) ndio wapewe fedha zao.

Tunafahamu kuwa kuna watu mbali mbali hupitia hapa jamii forums. Hivyo jitahidini kufatilia ukiritimba huu unasababisha ukandamizaji kwa baadhi ya wanafunzi hasa wanaotekea familia za kada ya chini.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kwel aice mana mm mwenyeweeee nilikuwa na sup moja tu wamenipunguzia mkopo nalipa laki nne Saiv kutoka 1000000
 
Kwel aice mana mm mwenyeweeee nilikuwa na sup moja tu wamenipunguzia mkopo nalipa laki nne Saiv kutoka 1000000
Serikali lazima iwachukulie Hatua, wakuu wa vyuo hadi maafisa mikopo

Kuna uchafu wanaufanya sana, kupitia majukwaa kama haya wanaweza kupata taarifa zitaakazo wasaidia.

Magufuli hadi sasa ameshapeleka fedha zote vyuoni lakini, kuna baadhi hata 50% ya wanafunzi hawajapata fedha zao, kwa sababu ya mashariti ambayo hata bodi hawayajui
 
Usiposema ubaya au uovu unaofanyika na wewe unakuwa ni sehemu ya huo uovu......

Kama umegundua tatizo na uovu unaofanyika pamoja na wahusika wote, then usitie shaka kuusema maana MUNGU yupo upande wa wale wasioficha maovu, na huwalinda kwa uwezo wake mkubwa alionao....

So usiogope naomba useme tu bila shida....
 
Kumekuwepo na tatizo linalosababishwa na uongozi wa baadhi ya vyuo nchini kugoma kutoa fedha za kujikimu kwa baadhi ya wanafunzi mpaka wa ingie MIKATABA kandamizi(Ni singependa kuweka wazi hapa) ndio wapewe fedha zao.
MKUU kwa maamuzi haya nawe unalea hayo hayo usio yataka. Unaweza ukasema linalo kukera bila kutaja majina ya wahusika.
 
Kumekuwepo na tatizo linalosababishwa na uongozi wa baadhi ya vyuo nchini kugoma kutoa fedha za kujikimu kwa baadhi ya wanafunzi mpaka wa ingie MIKATABA kandamizi(Ni singependa kuweka wazi hapa) ndio wapewe fedha zao.

Tunafahamu kuwa kuna watu mbali mbali hupitia hapa jamii forums. Hivyo jitahidini kufatilia ukiritimba huu unasababisha ukandamizaji kwa baadhi ya wanafunzi hasa wanaotekea familia za kada ya chini.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.
Kama hutaki kuweka wazi endelea kupambana na huo uozo kimya kimya. No one will know and rescue you from that situation.
 
Wenye sup hela ya kujikimu hucheleweshwa wanaweza kukaa mda mrefu bila kusaini hawatoi sababu hapo.
Huwezi kusaini hela ya kujikimu kama hujalipa ada na wengine hutumia hizo ela kuongezea ada lakini wao hawalitambui hilo. Na kuna muda unasainishwa fom kuonesha ada unalipa lini pale utakapopewa ela ya kujikim na ela inakuwa bado haijaingia
 
Kwel aice mana mm mwenyeweeee nilikuwa na sup moja tu wamenipunguzia mkopo nalipa laki nne Saiv kutoka 1000000
Hii haisababishwi na kuwa na sup ni bodi wenyewe hupunguza hii ela kama mwaka juzi walitoa tangazo kuwa kunaeza kua na mabadiliko katika mikopo...
 
Wenye sup hela ya kujikimu hucheleweshwa wanaweza kukaa mda mrefu bila kusaini hawatoi sababu hapo.
Huwezi kusaini hela ya kujikimu kama hujalipa ada na wengine hutumia hizo ela kuongezea ada lakini wao hawalitambui hilo. Na kuna muda unasainishwa fom kuonesha ada unalipa lini pale utakapopewa ela ya kujikim na ela inakuwa bado haijaingia
Nili wahi msikia waziri akisema ni marufuku kuzuia watu kupata fedha zao za kujikimu, kisa hawajasajiliwa

Nadhani kama hili linafanywa ni wazi viongozi wa hizi taasisi zetu wanakiuka agizo la waziri
 
Wabongo waoga kweli,yani umeshindwa hata kutaja matatizo husikaau hata chuo na bado unatumia ID fake sasa ingekuwa real name ingekuwaje?
 
Pesa ya kujikimu hutelewa kila baada ya wiki 8 kwa semester.
Tunavozungumza leo tarehe 20/Nov/2019 ni wiki ya tatu ya masomo wiki ijayo ni nusu ya awamu ya kwanza ya pesa za kujikimu itakuwa imefika, ila Katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar Es Salaam karibu nusu ya wanafunzi hawajapokea pesa zao, na wengine fedha zao zitakatwa na Chuo moja kwa moja kama moja ya sharti walilo lazimishwa kulikubali ili wasifutuiwe usajili vinginevyo wanalazimishwa kuahirisha mwaka.

Hawa wanafunzi wengi wao wanategemea huduma za hostel za hapo chuo, ambazo hazitegemei usajili wao na walikuwa wakisubiri pesa hiyo ya kujikimu walipie hostel, wakati huo huo chuo kimewapa mwisho wa kuwa wamelipia vyumba ni tarehe 26 - NOV -2019
 
Back
Top Bottom