MUHIMU SANA: MGONJWA ANAWATAFUTA NDUGU ZAKE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI (ona picha)

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
48,666
67,982
Brethrens;
Nilipokea email hii kutoka kwa rafiki zangu ikiwa iko forwarded kwa watu tofauti, na mimi kwa nafasi yangu nikaona si vibaya kama nitaitumia JF kufikisha ujumbe huu, picha zipo chini hapa. Kama utaona labda humfahamu au una matatizo binafsi na thread hii ntafurahi kama utakaa kimya, sikutumwa ila ni utu tu nikaamini kuwa lolote laweza mfika yoyote popote wala sihusiani na swali lolote lile.

Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipokea mgonjwa toka Hospitali ya Mwananyamala tarehe 18/08/2011 akiwa mahututi na hajitambui. Inasemekana kuwa mgonjwa huyu aliokotwa na wasamaria wema barabarani akiwa amegonjwa na gari usiku wa kuamkia tarehe 18/08/2011 ambao walimpeleka Hospitali ya Mwananyamala.

Kwakuwa alikuwa ameumia sana Hospitali ya Mwananyalama iliamua kumleta Hospitali ya Taifa Muhimbili ili aweze kupata huduma na uchunguzi mkubwa zaidi.Mgonjwa huyu hajulikani jina lake kwani hawezi kuongea toka alipoletwa kutokea Mwananyamala. Mgonjwa huyu alifanikiwa kuonwa na madaktari bingwa siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 na kufanyiwa uchuguzi wa vipimo mbalimbali ikiwemo X-Ray ya tumbo, kichwa, kifua na kiuno. Matokeo ya vipimo hivyo yalionekana kuwa kichwani kulikuwa na damu kidogo iliyoganda kutokana na kuvujia kwa ndani, picha za kifua na kiuno zilionyesha kuwa hakuna tatizo.Picha ya tumbo ilionyesha kuwa bandama lilipasuka hali iliyopelekea kufanyia upasuaji siku hiyohiyo ya tarehe 18/08/2011 ili kuondoa bandama. Baada ya upasuaji mgonjwa alipelekwa moja kwa moja chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) siku hiyo hiyo ya tarehe 18/08/2011.HALI YAKE:Tangu apelekwe ICU hali yake bado ni mbaya, hajitambui.

Aidha tangu tarehe 18/08/2011 hakuna ndugu au jamaa aliyejitokeza kuulizia hali ya mgonjwa huyu.Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unaomba yeyote anayemfahamu mgonjwa huyu atoe taarifa kwa ndugu na jamaa zake ili waweze kufika kwa usaidizi zaidi.View attachment fwmgonjwaanawatafutanduguzake.zip 2A525891.jpg 2A588128.jpg 2A617296.jpg 2A647293.jpg TACH] 2A095602.jpg
 

Attachments

  • 2A404921.jpg
    2A404921.jpg
    42.7 KB · Views: 110

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
48,666
67,982
Kama atatokea mtu akawa na fununu za kuskia ndugu waliopotelewa na ndugu yao, wawasiliane na Muhimbili
 

Bigirita

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
15,893
7,196
Duh!
I can feel that, imeshanitokea hiyo.
Kijana alikuja mjini baada ya kushindwa shule huko kijijini, bange bange! Wakashindwa kuelewana na mama yake, alivyokuja town akatafutiwa attachment kwenye kijiwe flani, alfu kumi, tano kwa siku hakosi. Baada ya muda bange ikawa tamu, akipata alfu kumi leo, kesho yake haendi kijiweni.
Akashindwa kazi, akaingia mitaani, akawa konda, mpiga debe, siku ya siku akatembelewa na semi trailler. Akakaa muhimbili 3days hakuna ndugu anayejua, siku ya nne akazinduka akampigia mama yake, mama yake akapiga cm dar kwa ndugu zake, ile kwenda wakakuta tayari dogo katangulia mbele za haki.

inauma sana!
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
48,666
67,982
Yeah, kuna haja ya kumsaidia huyu naye, huenda ikawa ni the same story, tumsaidie
Duh!
I can feel that, imeshanitokea hiyo.
Kijana alikuja mjini baada ya kushindwa shule huko kijijini, bange bange! Wakashindwa kuelewana na mama yake, alivyokuja town akatafutiwa attachment kwenye kijiwe flani, alfu kumi, tano kwa siku hakosi. Baada ya muda bange ikawa tamu, akipata alfu kumi leo, kesho yake haendi kijiweni.
Akashindwa kazi, akaingia mitaani, akawa konda, mpiga debe, siku ya siku akatembelewa na semi trailler. Akakaa muhimbili 3days hakuna ndugu anayejua, siku ya nne akazinduka akampigia mama yake, mama yake akapiga cm dar kwa ndugu zake, ile kwenda wakakuta tayari dogo katangulia mbele za haki.

inauma sana!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom