Muhimu Sana: Kwa Wana CCM wote napenda kukumbushana mambo ya muhimu kuzingatia katika Uchaguzi mdogo

Boniphace Kichonge

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Messages
1,320
Points
2,000
Boniphace Kichonge

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2017
1,320 2,000
Kwa Wana CCM na wote wenye mapenzi mema na wote wa Chama chetu.
Jumapili ya tarehe 26/11/2017 tunaelekea kwenye uchaguzi wa madiwani katika jumla ya kata 43 nchini kote. Kama sehemu ya maandalizi nimeona ni vizuri kukumbushana mambo ya muhimu kuzingatia ili ushiriki wetu uwe na matokeo chanya.
Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo:
1. Kutunza vizuri kadi ya kupigia kura na kwenda nayo siku ya uchaguzi
2. Kujua sehemu utakayopigia kura
3.Kuhakiki jina lako
4. Kuwahi kufika kituo cha kupigia kura mapema
5.Kumkumbusha mwana CCM mwenzako kwenda kupiga kura. Waweza ongozana naye au hata kuwasiliana naye kwa njia ya simu.
6.Kutoa ushirikiano wa kutosha
kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama pamoja na Tume ya Uchaguzi.
7.Kutovaa mavazi yeyote yenye kuashiria alama za chama
8.Kupigia kura yako kwa umakini wa hali ya juu kwa kuzingatia maelekezo kutoks Tume ya Uchaguzi.
9.Kuondoka mara tu baada ya kupigia kura yako au kukaa umbali unaoruhusiwa kisheria.
10. Kuwa na tahadhari dhidi ya watu wenye malengo mabaya ya kuharibu Uchaguzi au kutishia amani. Unashauriwa kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la polisi.
11. Kutumia lugha ya staha wakati wote uwapo katika kituo cha upigaji kura.
12.Msubiri matokeo rasmi yatakayotolewa na Tume ya Uchaguzi.
13.Kupeana msaada mbalimbali kabla na baada ya kupiga kura kwa mfano usafiri au kupeana maelekezo mbalimbali.
13. Kuendelea kuiombea amani nchi yetu pamoja na Rais wetu John Magufuli.
14. Kufanya uhakiki ili kujua kama wote mmepiga kura. Fuatilia ujue kwanini mwenzako hajafika
Ushindi in dhahiri kwa CCM
Aksanteni.
+255 769 004297
 

Forum statistics

Threads 1,343,137
Members 514,956
Posts 32,774,899
Top