TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Baada ya matangazo meengi ya kujinasibu sana kuhusu nyumbani kumenoga nikanunua simcard ya TTCL....Duh kumbe nimeingia mkenge.....kwanza coverage yake siyo kiviile kama nilivyofikiria...yaani hata ukisagiri Dar - Dom inapatikana kwa tabu sana....sasa hivi hapa nillipo ni Dom Town pamoja na kuweka 25GB za internet hopeless kabisa....nimeweka ya Voda 80 MB ya kukopa Tsh 500 ....net imefunguka vizuri....na hii ni mara nyingi maeneo mbalimbali....sasa najiuliza TTCL mnakwama wapi mbona huduma zenu za kusua sua sana?...MwaKA jana Aprili niliomba uwakala ...kila siku nikienda napigwa kalenda na maelekezo napewa tofauti tofauti....nika nyoosha mikono.....au likiwa shirika la umma basi ndiyo lazima liachwe nyuma kila kitu?
Solved
 
Hi,
Sometime last year, my wife and self acquired two TTCL mobile SIM cards from one of your promotions official. Despite handing copies of our NIDA cards, both numbers ended up being registered under one name.
In wake of the TCRA's new regulations what can be done to rectify the matter? we both would like to retain your services.
Thanks.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)

- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)

- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?

- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.

- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu.

Rudi Nyumbani Kumenoga

Nina line ya TTCL, kuna wakati nikbadilisha na kuweka hiyo line kwenye baadhi ya simu, inaniandikia TIGO badala ya TTCL, swali langu ni kwanini inakuwa hivyo?
 
Mvua ikinyesha shida, ukiingia chumbani shida,ukiwa remote area shida,ukiwa kwenye mkusanyiko wa watu shida.Boresheni network.
 
Nina line ya TTCL, kuna wakati nikbadilisha na kuweka hiyo line kwenye baadhi ya simu, inaniandikia TIGO badala ya TTCL, swali langu ni kwanini inakuwa hivyo?
Hiyo ni ROAMING.
Yaani ni kwamba TTCL ina minara michache sana.
Hivyo wameona washee minara na kampuni ya TIGO.
 
TTCL Customer Care

Hi,
Sometime last year, my wife and self acquired two TTCL mobile SIM cards from one of your promotions official. Despite handing copies of our NIDA cards, both numbers ended up being registered under one name.
In wake of the TCRA's new regulations what can be done to rectify the matter? we both would like to retain your services.
Thanks.
 
Jamani TTCL hapa tabata kimanga, jirani na shule ya msingi kisukuru mtandao wenu unasunbua sana. Internet haipatikani kabisa. Ni muda mrefu hamtaki kutatua tatizo hili. Kulikoni TTCL Itabidi tuseme nyumbani HAKUNOGI
 
Uzi wa kipumbaf sana huu.

Iweje wateja tujiulize na kujijibu sisi wenyewe kwa njia ya zogo wakati staff walioanzisha uzi hawatoi majibu, ushauri wala suluhisho lolote.

Ina maana walianzisha uzi huu kutusanifu na kutung'ong'a akili zetu siyo?
 
Wakuu niko dodoma, niko kwenye hotel inaitwa dodoma hotel,

Jengo la pemben yangu ni makao makuu ya ttcl,

Maajabu ambayo nimeshangaa Yan Mpaka hapa nilipo ambapo ni karibu kabisa na makao Yao makuu napo network hakuna

Ni bora serikali ikataifisha hata halotel au Vodacom na ikawa ndio kampun ya serikali kuliko hawa ttcl,

Kama pemben ya jengo lao hakuna network je huko nje ya mji Kuna Hali gani?
2020-07-22 12.44.00.png
 
Back
Top Bottom