mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Swala la Serikali tatu limeanza kupigiwa kelele na baadhi ya watu has wakidai ni mzigo kwa taifa. Wengi wa hawa wanaonekana ni wanaccm. Amelisemea Sumaye, Leo Sita naye kalisemea. Swali je, hawa viongozi na baadhi ya watu wanaopinga serikali tatu wnandhani hayo ni maoni ya tume imeamua kujiwekea yenyewe au ni maoni ya wanannchi? Je ni kweli hawa watu wana uchungu na walala hoi kubebeshwa mzigo wa kuendesha serikali tatu au wana ajenda zao binafsi? Ushauri kwa tume. Kablay ya rasimu kwenda kwenye mabaraza kuna umuhimu wa tume kufafanua hasa yale mabo yaliyokaa kitaalamu zaidi hasa hili la serikali tatu na mengine. La sivyo kutakuwa na upotoshaji mkubwa sana kwenye mabarzaya katiba na mwisho itakuwa vurugu mechi. Tafadhali Tume itoelee ufafanuzi vipengele ambavyo ni rahisi kupotoshwa.Binafsi naamini serikali tatu zitasaidia walau kuzuia kuvunjika kwa muungano haraka. lakini tukirudi kwenye serikali mbili muungano utavunjika immediately. Na serikali moja haiwezekani kwa sasa. Itakuwa balaa zaidi. Serikali moja ni tiketi ya wazi kuvunja muungano.