Muhimu kufahamu, MTINDI: Huimarisha kinga ya mwili, hurefusha maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimu kufahamu, MTINDI: Huimarisha kinga ya mwili, hurefusha maisha

Discussion in 'JF Doctor' started by babalao, Feb 24, 2011.

 1. babalao

  babalao Forum Spammer

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtindi unaorodheshwa kuwa miongoni mwa vyakula bora kutokana na kuwa na virutubisho vingi vya aina mbalimbali ambavyo vina faida nyingi katika mwili wa binadamu.


  Vikitajwa kwa uchache virutubisho hivyo, imethibitika kuwa mtindi ni chanzo kizuri cha ‘Calcium’, ‘Phosphorus’, ‘Riboflavin (vitamin B2), ‘Iodine’, ‘vitamin B12’, ‘Pantothenic acid (vitamin B5) ‘Zinc’, ‘Potassium’ na ‘Molybdenum’. Mbali ya virutubisho hivyo, ndani ya mtindi kuna ‘bakteria hai’ ambao ni muhimu kiafya katika mwili.

  HUREFUSHA MAISHA
  Utafiti unaonesha kuwa unywaji wa mtindi mara kwa mara, hasa katika kundi la wazee, uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa mbalimbali umeonesha kuongezeka na kufanya mfumo wa kinga ya mwili kuwa imara zaidi.


  Katika utafiti mmoja, walichaguliwa wazee 162 ambao walipewa utaratibu wa kunywa mtindi na maziwa zaidi ya mara 3 kwa wiki na kufuatiliwa maendeleo yao kwa muda wa miaka mitano. Baadaye utafiti huo ulionesha kuwa idadi ya vifo vya wazee hao ilipungua kwa asilimia 38 ukilinganisha na kundi la wazee wasiotumia au waliotumia mtindi kiasi kidogo sana.

  KINGA KWA KINA MAMA
  Aidha, mtindi umeonesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya maradhi ya kuambukiza ukeni (vaginal infections). Katika utafiti mmoja uliohusisha wanawake wenye magonjwa ya kuambukiza sehemu za siri, baada ya kutumia mtindi kiasi cha paketi moja kila siku kwa muda wa miezi sita, maambukizi waliyokuwanayo wanawake hao kabla yalitoweka.

  KINGA YA MWILI
  Utafiti uliofanywa kwa wanyama, wakiwemo panya na kuchapishwa kwenye jarida moja la masuala ya virutubisho nchini Marekani (Journal Of Nutrition), umeonesha kuwa unywaji wa mtindi kila siku, huamsha na kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili kupambana na magonjwa kadhaa ya maambukizi, ikiwemo saratani ya utumbo.

  HUONDOA LEHEMU MBAYA MWILINI
  Katika hatua nyingine, mtindi umeonekana kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha lehemu mbaya mwilini (LDL (bad) cholesterol) na wakati huo huo kupandisha kiwango cha lehemu nzuri mwilini (HDL (good) cholesterol). Kwa maana nyingine, ikiwa mtindi unaondoa lehemu mbaya, mtumiaji anajiepusha pia na hatari ya kupatwa na tatizo la shinikizo la damu.

  KUPUNGUZA UZITO
  Mbali ya faida hizo, mtindi pia umeonekana kupunguza mafuta (fat) mwilini na kwa maana hiyo una uwezo wa kupunguza unene unaotokana na mafuta mengi mwilini.

  MUHIMU KUZINGATIA
  Jambo muhimu la kuzingatia ni unywaji wa mtindi halisi uliotengenezwa kutokana na maziwa halisi ya ng’ombe, siyo mtindi uliotengenezwa kutokana na maziwa ya unga. Siri kubwa iliyomo kwenye mtindi ni ule uchachu unaotokana na ‘bakteria hai’ wanaopatikana baada ya maziwa kuganda na kuchachuka.
   
 2. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  thanks for information
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ahsante baba ushauri
   
 4. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda apach ayako!
   
 5. t

  tbetram Member

  #5
  Feb 25, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa. Mwanzoni nilipoona neno mtindi katika title nilidhani utaongelea juu ya matiti!!
   
 6. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante Babalao kwa taarifa hii ambayo ninaitumia kama fursa katika kuongeza uzalishaji wa maziwa ya ng'ombe na ku-process mtindi.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kiswahili mbofumbofu!

  Ina maana makabila ya kichungaji wana chances kubwa kuishi maisha marefu kuliko wengine?
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Feb 25, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Asante kwa taarifa. Ninakunywa mtindi kila siku na faida zake ninaziona.
   
 9. e

  ejogo JF-Expert Member

  #9
  Feb 25, 2011
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nimeipenda, asante sana. Sasa ni mtindi zaidi!
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Feb 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  asante kwa taarifa njema nilidhani upo kwenye uchumi tu kumbe mpaka kwenye afya safi sana mkuu
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Feb 25, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ebu tutajie mkuu na mtindi huu tanga fresh vp jamani unavirutubisho
   
 12. babalao

  babalao Forum Spammer

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chunguza kama unatokana na maziwa halisi wengine huwa wanachakachua unaofaa zaidi ni ule unaotoka kwa wafugaji.
   
 13. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Shukrani! Ni taarifa nzuri!
   
Loading...