Muhimili wa Mahakama utajinasua vipi uwakala wa CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimili wa Mahakama utajinasua vipi uwakala wa CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 31, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Muhimili wa Mahakama utajinasua vipi uwakala wa CCM?

  Kuna hofu kuu iliyotanda nchini katika medani ya siasa kwamba endapo Mhakama, ambacho ni muhimili muhimu wa nchi unaotarajiwa kutoa haki (na hivyo kuweka mustakabali wa nchi katika njia ya usalama) itazembea kutoa maamuzi ya mapema na ya haki kuhusu rufaa ya suala la mgombea binafsi, basi uchaguzi mkuu wa October utakuwa umeingia dosari kubwa kiasi kwamba utakuwa siyo huru na haki.

  Inasikitisha kuona kwamba Muhimili wa Mahakama uko tayari kubeba mzigo huo kama wakala wa chama tawala (CCM) kwani kuchelewesha kutoa maamuzi ya haki na ya haraka kuhusu suala hilo ni muafaka na unafuu kwa CCM. Mahakama itaweka historia ya kusaidia kuifinya demokrasia ya kweli hapa nchini.

  Hili ni suala moja, jingine ni kuhusu usajili wa CCJ ambao umekwama kwa Msajili wa Vyama na huenda suala hilo likafika kwenye Muhimili huo wa kutoa haki ambako maamuzi yake yatangojewa kwa shauku kubwa na wananchi: iwapo Mahakama itasalimu amri ya CCM kwa kuuunga mkono hatua ya Msajili ya kutokiandikisha chama hicho mapema.

  Aidha Mchungaji Mtikila anatarajia kwenda Mahakamani kuzuia Uchaguzi Mkuu iwapo wagombea binafsi hawataruhusiwa katika uchaguzi wa mwaka huu. Huo pia utakuwa mtihani mkubwa kwa Mahakama katika kutoa haki na iwapo itajinasua kama ni wakala wa CCM!
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tabia ya Muhimili wa Mahakama unashangaza sana kwa kuogopa kutenda haki na kwa wakati. Ni muhimili pekee ambao hauna mwakilishi kwenye kamati kuu za chama tawala -- CCM (yaani CCM-NEC na Kamati yake kuu) kwa hivyo ni muhimili ambao ungepaswa kuwa neutral zaidi kwani ina fursa kubwa ya kuchangia katika kuleta demokrasia ya kweli -- na siyo ile ya kihuni tunayoishuhudia ile inayoipendelea chama tawala.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuna bahati mbaya -- kila kitu ni hasi kwa wanaotaka kutafuta haki. Inavoonekana hakuna pa kukimbilia. Kwa mfano, waziri mmoja wa kikwete kasema CCj hakiwezi kusajiliwa -- utadhani yeye ndiye Msajili. Na ninawahakikishieni, hili suala hata likifika Mahakama, hakuna kitu, kwani in this country a minister is more supreme than the judiciary.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tatizo la mahakama za Tanzania na afrika kwa ujumla ni njaa za mahakimu na tabia tegemezi tuliyorithishwa na wakoloni.
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Nina wasi wasi sana kama Mahakama itatutendea haki na kutupa wananchi haki yetu ya kuchaguliwa na kuchagua katika chaguzi mbalimbali. Hofu hii inakuja baada ya kuona jinsi mahakam zetu zinapotoa hukumu sio kwa kufuata sheria na haki bali kwa kuangalia utashi wa watawala wetu!! Mfano hai ni huu wa kumhukumu mtu kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kutumia hovyo madalaka ya ofisi yake; ushahidi uliotolewa mahakamani ni dhahili kuwa huyu mhusika hakufanya kosa bali wakubwa wake ndio waliohusika lakini kwa kutumia mbinu ya wengi wape mahakimu wawili walimuona ana hatia, na mmoja ambae alikuwa kiongozi wao na mwenye uzoefu hakukubaliana na wenzie hivyo mtuhumiwa kukutwa na hatia. Nachelea kusema kuwa mbinu hiyo hiyo ya wengi wape itatumiwa na mahakama ya rufaa kutunyima haki yetu ya kuwa na mgombea binafsi kwa kigezo sio cha haki ya wananchi bali kwa hao majaji watakaokuwa wengi kubainisha kuwa kuruhusu mgombea binafsi itakuwagharama kubwa kwa Taifa kwani itabidi kuahirisha uchaguzi mwezi October!! Swali langu kwao ni je kuna gharama kubwa kwa binadamu zaidi ya kuahirisha au kumyima haki yake? Mahakama ziepushe maafa kwa kulinda haki za binadamu.
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  tatizo la Tanzania ni kwamba mihimili mitatu ya dola badala ya kuchungana inalindana. Bunge lilipoonekana kuihoji serikali, serikali nayo ikaja na kuhoji posho mara 2 za wabunge - wote wakafyata mkia - nikune nikukune. Mahakama japo haina mwakilishi wa moja kwa moja katika CCM CC na CCM NEC vitendo vyake vinaashiria kuwa wamo kwa remote. Ni kesi ngapi za uchaguzi zinazohusu wagombea wa ccm zimehukumiwa nao wakashindwa? Ebu ona za kuwashtaki wapinzani zinavyopelekwa haraka haraka nk. Suala la mgombea binafsi - muda wa kukata rufaa ulishapita -tangu 2006, lakini wakaipokea rufaa na sasa hawataki kutoa hukumu; wanasubiri rais atangazwe ndipo waseme mgombea binafsi ruksa nk nk.
  Kweli wananchi watakapokata tamaa na kuona hawana pa kukimbilia - wataenda msituni! Tusije tukalaumiana.
   
Loading...