BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,167
Lazima tulifuatilie swala hili hadi tujue ukweli umelalia wapi. Kama Muhimbili ndio wanasema ukweli kwamba hakuna vichanga vilivyopoteza uhai kwa kukosekana umeme, basi gazeti lililoandika habari ambazo hazikuwa na ukweli ni lazima lishutumiwe. Waandishi wa magazeti wanaoandika habari za uwongo siku zote lazima wapigwe vita hapa JF
habarileo; Friday,February 29, 2008 @06:11
Halima Mlacha
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imekanusha taarifa kuwa watoto watano waliolazwa hospitalini hapo wamekufa kutokana na kukosa hewa baada ya kukatika umeme.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano hospitalini hapo, Aminiel Aligaesha, hakuna mtoto yeyote aliyekufa kutokana na kukosekana kwa umeme hospitalini hapo.
"MNH inatoa ufafanuzi kuwa hakuna mtoto yeyote aliyekufa kutokana na kukatika kwa umeme, pia hakuna mashine zinazotumia umeme katika wodi ya watoto waliozaliwa njiti, ila kuna mashine za kuwapa joto," alisema Aligaesha.
Alisema hospitali hiyo ina jenereta sita ambazo umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ukikatika tu, huunganishwa katika maeneo yote muhimu, ikiwamo wodi hiyo ya watoto waliozaliwa njiti.
Akizungumzia tukio hilo linalosadikiwa kusababisha vifo vya watoto watano, alisema umeme huo wa Tanesco ulikatika saa 9 usiku jana na jenereta hizo ziliwashwa usiku huo huo na kufanya kazi hadi saa 3 asubuhi.
"Ni dhahiri kuwa maeneo yote ya Muhimbili yaliathirika kutokana na kutokuwapo kwa umeme na ndiyo maana jenereta zetu ziliwashwa ili kuendelea kutoa huduma katika maeneo yote muhimu, ikiwamo maabara kuu (CPL), jengo jipya la wagonjwa wa nje (NOPD), vyumba vya kufanyia upasuaji, vyumba vya wagonjwa mahututi (ICU) na maabara maalumu ya watoto," alisema.
Alisema umeme wa Tanesco ulirejea kuanzia saa 7.30 mchana na hakuna madhara au tatizo lolote kubwa lililojitokeza.