Muhimbili wanagoma kwa faida ya nani?? Tuongelee hili na si la Pinda na V8 yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimbili wanagoma kwa faida ya nani?? Tuongelee hili na si la Pinda na V8 yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eliesikia, Dec 6, 2010.

 1. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Badala ya kujunguana hapa JF basi tuangalie na hili... Hali mbaya sana kwa wauguzi.. Hapa ukiwa na Malaria Sugu lazima ufwe


  Kwa kweli tanzania ni pabaya hasa unapotawaliwa na wasanii ambao kwa sasa wako Belgium kwa ajili ya luxury escort badala ya kukaaa na kuangalia jinsi gani ndugu wanapukutika pale Muhimbili.... Hela zetu za kodi zikinajisiwa poa!!! Lakini maisha yetu tuachieni ati... Hata Muhindi alipovamiwa alisema Mi kupa wewe kila kitu hata ile fichwa lakini roho yangu achia...
  SERIKALI TUOKOENI WATATUUA HAWA KAMA WANAPEWA HELA NDOGO!!!!!.... HAWAWEZI KULIPWA KAMA WANYAMA LAKINI WAFANYE KAZI KAMA BINADAMU

  BAADHI ya wafanyakazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam, wamesema wamekuwa wakifanya kazi lakini wakiwa wanaendesha mgomo baridi unaotokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili, ikiwemo mishahara midogo.

  Wafanyakazi hao walisema hayo jana, walipozungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, aliyetembelea hospitali hiyo ili kujitambulisha kwa wafanyakazi.

  Mmoja wa wafanyakazi hao, Premis Saidia, alisema wamekuwa wakifanya kazi nyingi na kwa muda wa ya saa 24, lakini wanalipwa mishahara midogo.

  "Watu wanafanya kazi kwa mgomo baridi wapo kama hawapo kutokana na matatizo hayo,"alisema Saidia.
  Alisema wafanyakazi wengi wa sekta ya afya ni wazuri na wawajibikaji lakini hawalipwi mishahara na marupurupu makubwa.

  Alisema tatizo hilo ndilo linalosababisha baadhi ya watumishi wa sekta hiyo, kukimbia kwenye hospitali za watu binafsi na kwenda nje ya nchi.


  Wafanyakazi hao pia walilalamikia kutokuwepo kwa Mkurugenzi Mtendaji katika hospitali hiyo na kwamba nafasi hiyo imekuwa wazi tangu Novemba mwaka jana, alipostaafu mkurugenzi wa zamani.


  "Nachelea kuamini kwamba hospitali hii inaendeshwa kisiasa. Tangu mkurugenzi amestaafu ni mwaka mmoja sasa anakaimu mtu mwingine hata maamuzi yake yatakuwa ya kukaimu,"alisema Saidia.

  Mfanyakazi mwingine, Theresia Yomo, aliiomba serikali kuwaangalia wafanyakazi wanaosihi na virusi vya Ukimwi ambao bado wana nguvu za kufanya kazi ili waweze kupata posho na chakula.

  Rehema Mwaipaja alilalamikia ubaguzi katika kuwasomesha madaktari na wauguzi na kuacha watumishi wa kada nyingine.


  "Wataalamu wa kada zote tunahitaji kwenda na wakati lakini wanasomeshwa ni madaktari na wauguzi tu, je mgonjwa anahudumiwa na watu hao wawili,"alihoji Mwaipaja.

  Source: Mwananchi
   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu waswahili wanasema, "wapambanapo mafahari wawili ziumiazo ni nyasi".Kimsingi ukiangalia kwa undani unaweza kuona kuwa wafanyakazi wa muhimbili ni kama vibarua na vijakazi, serikali haiwajali hata kidogo. Jaribu kuangalia mishahara yao na mazingira yao ya kazi halafu ulinganishe na wenzao wa Kenya, Uganda na Rwanda, utaona kuwa they are being treated like shite. Sasa why should they work their ... off kwa mtu ambaya hajali. Ukiskia seniors wao wanaongea utaona kuwa wanachoongea ni maneno tu lakini hakuna cha maana kinachofanyika.

  Jaribu kuangalia ofisi zao, vyoo vyao, vifaa vyao, unaweza kuona kama ni gereza au some kind of dirty place. Lakini angalia ofisi za mabosi wao wa kisiasa, full AC, manukato, mazulia, coffee, tea hata bia kwa wingi. Na wakifanya kazi wao, hao mabosi dio wanatake credit, ungekuwa wewe ungekubali ujinga huo?
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Jamani hebu tuweni wakweli. Katika nchi hii watumishi wanaolipwa vizuri, ni wa Afya. Utakuta mtu ana shule ndogo lakini analipwa vizuri kuliko mwenye BA. Ukweli ni kwamba hawana chembe za uzalendo na wana ajenda zaidi ya wanayoitamka.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  huna maana kabisa....... kuna watu wanaoteseka hapa tz kama madaktari na kundi la waalimu?!!!

  think beyond the next meal!!!
   
 5. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli hali ya pale ni noma sana jamni acha tu
   
 6. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu uzalendo maana yake nini? Kufanya kazi bila ya kupewa stahili yako au kufanya kazi bila kudai mshahara sio uzalendo na wala watu huwa hawaombwi wala kufundishwa uzalendo. tungekuwa na serikali inayotekeleza majukumu yake kwa wananchi ungeuona uzalendo. Daktari anayelipwa sh laki tano ua basi hata sita kwa mwezi angukuwa mzalendo kama kodi inayotokana na makato ya mshahara wake na wafanyakazi wengine ingetumika kuboresha huduma za afya...vitanda kwa wagonjwa, madawa, vitendea kazi nk..pengine hujui, lakini fahama kuwa madaktari na wauguzi hawa in many occassions wanalazimika kutake risk kwa ajili ya wagonjwa. Leo katika zama hizi za UKIMWI madaktari wanafanya operesheni bila ya kuvaa googles (miwani kuwakinga na damu inayoweza kurukia usoni/macho na pengine kuwaambukiza UKIMWI) n.k nimeshuhudia wauguzi wakivaa glovu moja kawasababu ziko chache..katika mazingira haya hawawezi kuwa wazalendo hata kidogo. swala la watu wenye BA kulipwa kidogo ni kichekesho ndugu yangu...kumbuka it takes one three years kupata BA na daktari anasoma 5 years plus 1 year internship.LAKINI la muhimu ni kuwa kama walio na BA wanaona mshahara wanaopata sio stahili yao wanaruhusiwa kuelezea malalamiko yao na sio kusema madaktari wakae kimya kisa tu wanaolipwa mshahara mdogo wako wengi.
   
Loading...