Muhimbili wakataa kumpatia kijana maiti ya mkewe kwa kushindwa kulipa deni

Mbotonho

New Member
May 13, 2020
2
22
Ni baada ya kushindwa kulipa Tsh. 1,470,800. Aamua kurejea Mtwara. Kaburi lililochimbwa kwa ajili ya kumhifadhi marehemu lafukiwa.

Pia soma > Naibu Waziri wa Afya Dkt Ndugulile: Ni marufuku Hospitali kushikilia maiti kwa kile kinachotajwa hadi pale gharama za matibabu yake zitakapolipwa

Ni mkasa uliompata bwana Shaaban Mtepa, mkazi wa mji mdogo wa Kitama wilayani Tandahimba. Ilikuwa tarehe 13 Juni siku ambayo Bi Zainabu Shaibu Mazoa alihisi uchungu uliotokana na ujauzito na hivyo kulazimika kukimbizwa hospitali ya wilaya ya Tandahimba kwa ajili ya huduma ya kujifungua.

Alipofika hospitalini hapo alifanyiwa upasuaji kisha alijifungua mtoto mwenye afya njema lakini mama mwenyewe hakuwa na maendeleo mazuri ya kiafya kwani alivuja uchafu mwingi sana kwa muda wa siku nne mfululizo na ilipofika siku ya tano alirejeshwa theatre kwa ajili ya upasuaji mwingine.

Hali yake iliendelea kuwa tete kwani tatizo lile lile la kuvuja uchafu liliendelea na madaktari waliamua kumfanyia upasuaji kwa mara ya tatu. Hata hivyo hakukuwa na mafanikio yoyote kwa hiyo walilazimika kumpa rufaa ya kwenda hospitali ya mkoa wa Mtwara (Ligula) kwa matibabu zaidi, ila nao madaktari wa Ligula walishindwa kutatua tatizo lililomkabili mama huyu hivyo waliamua kumsafirisha hadi hospitali ya Taifa yaani Muhimbili.

Aliendelea kupata tiba hapo Muhimbili kwa siku nne na ilipofika siku ya tano yaani usiku wa kuamkia tarehe 7 Julai 2020 huyu mama aliaga dunia huku akimwachia mumewe mtoto mchanga wa wiki mbili. Na baada ya hapo ndipo kijana Shaaban Mtepa alipoanza kufuatilia maiti ya mkewe ili akaihifadhi kwenye makazi ya milele lakini akakutana na kigingi cha kutakiwa alipe fedha Tsh. 1,470,800 huku mfukoni akiwa hana japo senti tano.

Amehangaika kuomba kupatiwa maiti hiyo tangu tarehe 7 Julai hadi tarehe 9 siku ya Alhamisi lakini hakufanikiwa kuipata maiti hiyo ya mpendwa wake.

Kuna wasamaria wema walimsaidia kuandaa kaburi kwa ajili ya maziko kwenye Makaburi yaliyopo Buza kwa mama Kibonge tangu siku ya Jumatano tarehe 8 Julai lakini ilipofika Alhamisi tarehe 9 Julai waliamua kufukia kaburi hilo baada ya jitihada za kuupata mwili wa marehemu kugonga mwamba.

Hivyo wasamaria hao wakachanga pesa kidogo ambazo zimemwezesha bwana Shaaban kukata tiketi ya basi kwa ajili ya kurejea Mtwara siku ya Ijumaa 10 Julai huku akimwacha mkewe akiwa amelala kwenye chumba cha maiti cha hospitali ya Taifa, Muhimbili.

Napenda kutoa wito kwa Uongozi wa hospitali pamoja na serikali ya mheshimwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli kuingilia kati suala hili ili kijana huyu mnyonge na mlala hoi aweze kukabidhiwa mwili wa mpendwa wake ili akauhifadhi mahala panapostahili. Lakini pia kwa aliyeguswa anaweza kumsaidia kijana huyu kwa kuwasiliana naye kwa simu No 0778140361.

Ahsanteni.

Pia Soma
> Wabunge waitaka Serikali kuacha tabia ya kushikilia maiti ndugu wanaposhindwa kulipa gharama za matibabu

> Hili la maiti kulipishwa madeni Hospitali za Serikali limekaaje?

> Waziri Ummy Mwalimu, hili la kuzuia maiti ni unajisi wa mila zetu za kiafrika. Litazameni vizuri
 
Watu wenye uwezo Mjipange muwe mnatembelea mahospital na kuwalipia bili wagonjwa. Watu wanateseka mno..
Mungu anisaidie aisee
Inauma mno
Hiyo ni Hospital ya Dr John Pombe Joseph Magufuli, ya Serkali ya Dr John Pombe Joseph Magufuli wa Tanzania ya Dr John Pombe Joseph Magufuli Rais wetu Mpendwa wa wanyonge, Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha CCM Mpya Cha Dr John Pombe Joseph Magufuli, Amiri Jeshi Mkuu. Pole sana kijana tunza mtoto wako ndo pekee atakuja akusaidie. Tanzania ndo tumefikia!
 
Hiyo ni Hospital ya Dr John Pombe Joseph Magufuli, ya Serkali ya Dr John Pombe Joseph Magufuli wa Tanzania ya Dr John Pombe Joseph Magufuli Rais wetu Mpendwa wa wanyonge, Mwenyekiti wa Chama Tawala Cha CCM Mpya Cha Dr John Pombe Joseph Magufuli, Amiri Jeshi Mkuu. Pole sana kijana tunza mtoto wako ndo pekee atakuja akusaidie. Tanzania ndo tumefikia!
Ngoja nimstue mkuu Zitto anaweza akasaidia kitu
 
Inasikitisha, mbunge wetu Joseph Mbilinyi aliwahi kusema matukio haya yapo lakini serikali ya CCM Mpya walikanusha. Sasa tunapata taarifa hii ya huzuni kuhusu mtanzania mwenzetu.

Toka maktaba :

Bungeni Dodoma
7 February 2020
Mbunge Sugu 'amchana' Waziri Ummy kuzuia maiti, mawaziri na wabunge wa CCM Mpya hawaelewi !


Source : Mwananchi digital
 
Angefuata utaratibu amgepatika..huenda na yete alijimwambafai..Kuna dawati maalumu libalosikilza hizo case
 
Serikali ilitoa majibu baada ya wabunge wa Chama chetu CCM kulala fofofo akatokea mbunge wa upinzani kutetea wanyonge mauti zao kukataliwa na hospital za serikali. Kwa sababu mauti eti inadaiwa!!

kweli serikali inazdai maiti pesa?maiti inaweza kulipa kweli?hvi unaidaije maiti? Serikali ni chombo cha kulinda group fulani la wanyonge sasa hapa inafanya nini?

Inauma Sana Ndugu zangu!!
 
Back
Top Bottom