Muhimbili wakataa kumpatia kijana maiti ya mkewe kwa kushindwa kulipa deni

Hiyo muhimbili yakataaa ndiyo mbaya!
Inabidi muhimbili watoe ufafanuzi kuhusu hilo

Ova
 
Una umri gani kwanza?
Unadhani Kila mtu Ana uwezo Kama wewe? Hata dini yako haikufundishi Kama Kuna wenye uwezo na wasio na uwezo?
Serikali hii ni ya kilaghai sana. Yaani gharama za huduma za afya kwa sasa ziko juu sana.
Lakini bado CCM inaendelea kuwadanganya watanzania kwamba huduma za mama na mtoto ni bure wakati huduma za kujifungua pekee ni LAKI MBILI.

Yaani hiki chama kimekuwa kikitunyonya tangu uhuru..
 
Nimetoka kumpigia simu huyu kijana. Kwa kweli anaongea kwa uchungu hadi nimedondosha chozi. Anasema amepewa taarifa kwamba huko kwao kuna kilio kijiji kizima.

Mheshimiwa Magufuli si amekuwa akisisitiza kila mara kwamba hii ni serikali ya wanyonge, sasa kulikoni wanyonge wananyongwa?

Hii ni AIBU na FEDHEHA kwa CCM. Muoneeni huruma huyu mvuja jasho.
So sad

Ova
 
Inaiskitisha kweli' kwa upande wa kodi naona sheria imeliangalia hilo' mfn kama mali ilikua ya marehemu(deceased) na inauzwa huwa hailipiwi kodi( ina exemption) sasa sijui ni kwanini kwa upande wa afya isiwe ivi.
Serikali ilitoa majibu baada ya wabunge wa Chama chetu CCM kulala fofofo akatokea mbunge wa upinzani kutetea wanyonge mauti zao kukataliwa na hospital za serikali. Kwa sababu mauti eti inadaiwa!!

kweli serikali inazdai maiti pesa?maiti inaweza kulipa kweli?hvi unaidaije maiti? Serikali ni chombo cha kulinda group fulani la wanyonge sasa hapa inafanya nini?

Inauma Sana Ndugu zangu!!
 
Tatizo Ni mfumo wa ulipaji wa fedha kwa njia ya POS amepelekwa akahudumiwa bili inasoma. Hivyo huo mfumo waubadili.
 
mtalazimika kuingia gharama wenyewe maana marehemu sasa atazikwa na manispaa ya jiji.
maiti inaenda kuwa cadaver ya kufundishia medical school, hakuna hasara kwa serikali

na si huyo mmoja mwenye madeni hayo, serikali haifanyi kazi kwa huruma za mtu mmoja mmoja kwa vile kasikika Jamiiforums au katoka Tandahimba

suluhisho la serikali kwa jamii katika ujumla wake ni bima ya afya, tuiizingatie

hakuna mfiwa ambae yeye eti hana majonzi au ana mahela mengi ya kulipia maiti na msiba halafu wengine ndio wana majonzi sana wasilipe...

watu wote ni sawa mbele ya serikali, lakini hata ungesema unatoa special dispensation kwa wanyonge na masikini, hayuko huyo maskini wa Tandahimba mmoja peke yake
 
maiti inaenda kuwa cadaver ya kufundishia medical school, hakuna hasara kwa serikali

na si huyo mmoja mwenye madeni hayo, serikali haifanyi kazi kwa huruma za mtu mmoja mmoja kwa vile kasikika Jamiiforums au katoka Tandahimba

suluhisho la serikali kwa jamii katika ujumla wake ni bima ya afya, tuiizingatie

hakuna mfiwa ambae yeye eti hana na majonzi au ana mahela ya kulipia halafu wengine ndio wanq majonzi sana wasilipe...
Siku maiti ya babako itakaposhikiliwa ndipo utakatambua kwamba serikali ya CCM ni ya kihuni.
 
Serikali hii ni ya kilaghai sana. Yaani gharama za huduma za afya kwa sasa ziko juu sana.
Lakini bado CCM inaendelea kuwadanganya watanzania kwamba huduma za mama na mtoto ni bure wakati huduma za kujifungua pekee ni LAKI MBILI.

Yaani hiki chama kimekuwa kikitunyonya tangu uhuru..
Hii habari imenisikitisha sana, pole sana kwake kijana.
Suluhisho la kudumu kwa matukio ya aina hii, ni kuwezesha huduma za afya kupatikana bila mwananchi kutumia pesa yake "out of pocket", yaani kutoa pesa yake mfukoni pale anapokua anaumwa, kwa sababu mfumo wa aina hii umeshaonyesha kuwa mara nyingi wananchi hawaumudu, kwani gharama za afya ni ghali sana sana, na mara nyingi huweza kupelekea kuzidi kusukumiza familia kwenye lindi la umasikini na kuendeleza wanachoita "duara la umasikini". Ili uwezeshe kuondokona na mwananchi kutoa pesa yake mfukoni moja kwa moja pale anapokua anaumwa, ni eidha utumie mfumo wa BIMA YA AFYA, au serikali iwe inalipia hizo huduma za afya, na wananchi wao wanazitumia tuu.
Mifumo ya Bima ya afya angalau imeonyesha kufanya kazi vizuri nchi kadhaa pale panapokua na usimamizi makini; kwa bahati mbaya sana, kwa Tanzania hii wananchi ambao wana bima za afya, hawavuki hata asilimia 10. Kwa mawazo yangu, serikali ingeweka nguvu zaidi katika kuboresha mifumo ya bima ya afya nchini na kuangalia namna ya kuweza kuwasaidia wananchi wasio na vipato rasmi kuweza pia kuingia kwenye mifumo ya bima ya afya, ambao utawawezesha wananchi hawa pia kuweza kupata hata huduma za kibingwa na kibobezi kutoka hospitali kama Muhimbili (Natambua juhudi za serikali hivi karibuni, katika kinachoitwa "Bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa", ni hatua sahihi, lakini maboresho yanahitajika zaidi,kwani kwa sasa kuna vizuizi vingi sana vya kupata huduma za kibingwa na vipimo vya maabara kwa kutumia bima hii-huduma zake zinaishia sana sana hospitali za wilaya-na bado vipimo vingi vya maabara havilipiwi na bima hii).
Mfumo wa serikali kulipia huduma za afya na wananchi kuzipata bure, uliwahi kufanyika hapa nchini lakini malalamiko yalikua mengi na ufanisi wake ulikua ni mdogo, mwisho wa siku ulisababisha kudorora kwa ubora wa huduma za afya za serikali.
Tatizo ni kwamba, hili suala linaingiliwa na siasa nyingi mno. Wanasiasa wakiwa majukwaani huko hawasemi ukweli unaotakiwa kusemwa, kwa sababu wanajua wao kama serikali hawawezi au sio kipaumbele chao kubeba gharama za afya za wananchi wao; na pia wanajua kuwa huduma bora za afya ni gharama sana, na wananchi wao hawawezi kumudu hizo gharama (wanasiasa wanajua hili,maana wao bima zao zinawaruhusu kutibiwa hospitali za level kama Muhimbili, na Aga Khan, na huwa wanaona bili ambazo bima zao zinatozwa wanapotumia huduma hizo), basi wanachoamua wanasiasa ni "kupiga porojo" wakiwa majukwaani kama ambazo alizipiga Ummy Mwalimu juu ya suala hili; alitoa majibu mepesi mno kwa swali gumu sana.... Suluhu ya hili, sio kutoa maagizo kwamba, "wananchi watibiwe kwanza, na kama mtu amefariki, ndugu wapewe maiti wakazike, waje kulipa baadae". Na hata yeye mwenyewe (Ummy Mwalimu) analijua hili.
Ben Bella
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom