Muhimbili tusaideni hili la dawa ya tezi dume

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,081
5,061
Facebook kuna clip inayotangaza dawa ya kutibu tezi dume bila upasuaji wala vidonge. Tangazo linajinasibu ya kuwa dawa hiyo inatoka Muhimbili. Ukiangalia anayetangaza kavaa Tshirt yenye nembo zinazohusiana na serikali.

Ukijaribu ku-chat ili kujua bei majibu yanakuwa si ya wazi sana.

Kwakuwa kuna watu ambao wanateseka na shida hiyo ya tezi dume niaomba Muhimbili watusaidie
  1. Kukiri au kukataa kuhusika na dawa hiyo
  2. Kututolea angalau takwimu za mafanikio ya dawa hiyo
  3. Kuweka wazi bei na namna ya upatikanaji wake.
 
nashauri wagonjwa kufika hospital , na siyo facebook

Haujui kwamba sio kila mgonjwa anataarifa sahihi za tatizo?

Kuna watu wana ndugu zao wataona hilo tangazo na kuwataarifu wagonjwa wakapate matibabu.

Lakini pia kwakuwa tangazo linahusisha taasisi ya serikali, ni vizuri wakalitolea ufafanuzi kuepusha utapeli na upotoshaji.
 
Tezi dume huwa inafikia hatua ya kuwa kansa ambayo inaweza kusambaa, kama hiyo dawa ina uwezo wa kutibu tezi dume bila shaka itakuwa na uwezo wa kutibu magonjwa mengine ya kansa. Kwa hiyo kwa case ya tezi dume matibabu yatategemea hatua iliyofikia baada ya kufanya vipimo na yanapatikana hospitalini......
 
Ukiingia Muhimbili Kuna banda la tiba mbadala halihusiani na hospital kuu, labda ni sehemu ya utafiti
 
Haujui kwamba sio kila mgonjwa anataarifa sahihi za tatizo?

Kuna watu wana ndugu zao wataona hilo tangazo na kuwataarifu wagonjwa wakapate matibabu.

Lakini pia kwakuwa tangazo linahusisha taasisi ya serikali, ni vizuri wakalitolea ufafanuzi kuepusha utapeli na upotoshaji.
taarifa sahihi zinapatikana wapi sasa mkuu
 
Back
Top Bottom