wakatanta
JF-Expert Member
- Feb 5, 2018
- 2,593
- 3,148
Rais John Magufuli, amewatembelea majeruhi walionusurika na ajali ya moto uliotokana na lori la mafuta kupinduka na kulipuka mkoani Morogoro jana Agosti 10, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Majeruhi hao walifikishwa hospitalini hapo jana saa nne usiku.
AJALI YA MOTO MOROGORO: RAIS MAGUFULI AWATEMBELEA MAJERUHI, AWAPA 500,000 KILA MMOJA
Majeruhi hao 43 wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili walipopelekwa kutoka hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Kati ya 46 waliofikishwa jana, watatu wamefariki dunia leo
Aidha, Rais Magufuli amewashukuru wauguzi pamoja na madaktari kwa huduma nzuri na kuwazawadia Tshs. milioni 1
Amewaagiza kuwahudumia majeruhi hao na kuwapatia mahitaji yoyote wanayohitaji kwa gharama ya Serikali

Rais wa wanyonge Dr. John Pombe Magufuli tunashukuru kwa upendo wako,kwa faraja uliyowapa wagonjwa hakika waliokata tamaa ya maisha sasa wamepata ahueni kwa ujio wako hapa Hospitali ya Muhimbili..
Wagonjwa wanapokea laki tano taslimu, wagonjwa waliopo ICU wanapewa milioni moja wagawane kwa ajili ya mahitaji
Madaktari wanapewa milioni moja kwenye chumba wagawane kama motisha
Asante mzee