Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,937
25,279
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mloganzila zimefunga mashine nne za kujifukiza.

Wakati Muhimbili zikifungwa mashine tatu, Mloganzila imefungwa moja. Gharama ya kila mashine ni Sh7.5 milioni na kila moja ina uwezo wa kuhudumia watu sita kwa wakati mmoja wanaopaswa kukaa kati ya dakika tano hadi 10.

Ili mtu aweze kujifukiza katika mashine hizo anapaswa kulipia Sh5,000 na yeyote anaruhusiwa hata wapita njia.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo zilizopewa jina la Bupiji Sauna leo Alhamisi Machi 4, 2021 mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kuanzishwa kwa mashine hizo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya kujifukiza kwa watu wote wanaohitaji.

“Kujifukiza huku kunaenda sambamba na matumizi ya dawa za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa na zimeonyesha kusaidia, mashine hii inatumia dawa ya Bupiji inayowekwa katika maji ya mvuke na mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika tano hadi 10,” Profesa Museru.

Profesa Museru amesema uwepo wa mashine hizo kutawawezesha madaktari kujua kama njia hiyo inasaidia kwa kiwango gani vita dhidi ya corona.

Mwananchi

---

PICHA ZA MUONEKANO WA MASHINE YA KUJIFUKIZA
1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
 
msiojua hii ni sauna ipo toka zamani ,hakuna hoteli kubwa isiyokuwa nayo,kazi yake kutoa sumu mwilini nk ,inasaidia sana hata magonjwa nyemerezi ngumu kupata anayefanya sauna
Sauna za wazungu ni sawa sawa na nyungu ? Maana wao walisema hazifai katika kipindi hiki cha kovidi, labda wataalamu watakuwa wameweka vya ziada ili kuzifanya salama na tofauti na hizo za wazungu
 
Haya ndiyo mambo yanayotufanya Watanzania tuonekane ni kituko huko nje. Ni aibu!!

 
Kuna watu wanadhihaki ila wakileta nyuzi za confession ya kuugua corona lazima wataje nyungu na mchanganyiko wa malimao

Corona imetuonyesha rangi halisi ya waafrika wale wa enzi za ukoloni

Binadamu sisi basi tu. Mungu Baba walimshindwa hadi akawaangamiza sodoma na Gomora sembuse Mwanadam mwenzao
 
Back
Top Bottom