Kama sio loliondo, twalazwa ka mitumba,
Usidhani ni uhondo, hatulali kwenye nyumba
Drip kwenye mipodo,zahanati kwa kuyumba,
Miaka 50 ya Uhuru, hakika tumesonga mbele
Wamama na yao matumbo, bajaji wazipakia
Kweli hawana tambo, sakafuni wajifungulia,
Matabibu huwa jambo, wagonjwa kuangaliia,
Miaka 50 ya Uhuru, hakika tumesonga mbele
Jamani hizi picha ni miss-leading sana!! Wakati wa kupiga deki wodini wagonjwa hutolewa nje, na hizi picha zilipigwa wakati huo. Aliyezipiga asiwalaghai watu bure!!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.