Muhimbili: Madaktari wadai posho, wao si kituo kupitishia vigogo kwenda India | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimbili: Madaktari wadai posho, wao si kituo kupitishia vigogo kwenda India

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 15, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya

  MADAKTARI BINGWA WATEMA CHECHE POSHO ZA WABUNGE

  Madaktari Bingwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wametapika nyongo na kuieleza Serikali wanapinga vikali nyongeza ya posho ya vikao kwa wabunge kutoka Sh. 70,000 hadi Sh. 200,000 kwa siku, pamoja na kuigeuza hospitali hiyo kuwa kituo cha kusafirishia vigogo kwa ajili ya kwenda nje ya nchi kutibiwa.

  Madaktari hao ambao waliungana na wafanyakazi wengine wa hospitali hiyo, walisema hayo jana mbele ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, ambapo walisema wao kama Madaktari Bingwa wanaona vitendo hivyo ni udhalilishaji mkubwa wanaofanyiwa na serikali. Dk. Nkya alikuwa na ziara ya kutembelea hospitali hiyo na kuzungumza na wafanyakazi wakati akitekeleza ratiba yake ya kutembelea hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuangalia utendaji wa kazi.


  Akizungumza kwa niaba yao, Dk. Prim Saidia, alisema kwa ujumla wafanyakazi wa hospitali hiyo hasa Madaktari Bingwa hawakubaliani na hatua ya kuwarundikia posho wabunge, huku wao wakiendelea kutaabika. Alisema kitu cha kusikitisha ni kwamba daktari ambaye amesoma na kupata shahada zaidi ya mbili anaendelea kupata posho ya Sh. 10,000 wakati katika ustawi wa nchi ndiye mtu muhimu na anayepaswa kuangaliwa kwa makini. “Mheshimiwa Waziri, leo tutakwambia ukweli, sisi madaktari tumechoshwa na hali hii, kama hali ngumu ya uchumi ni wote na hakuna kundi la watu. Haiwezekani Daktari Bingwa analipwa posho shilingi elfu kumi eti wabunge wameongezewa maradufu,” alisema Dk. Saidia.


  Aliongeza kuwa kitendo cha kuwapa wabunge Sh. 200,000 huku madaktari na wafanyakazi wa hospitali wanalipwa kiasi kidogo na wengine hawalipwi kitu, ni kitendo cha kuwadharau. Alieleza kwa ujumla madaktari wanaofanya kazi kwenye hospitali hiyo wanafanya kazi kwa ukwasi mkubwa kwani wengi wao wanashindwa hata kufika hospitalini hapo kutokana na kukosa pesa ya usafiri. “Hapa Muhimbili hatuna posho ya usafiri wala ile ya nyumba, daktari akihitajiwa inambidi atumie usafiri wake ili afike hapa, lakini Serikali haimjali na kuona wabunge ni bora zaidi ya wengine, huu ni udhalilishaji mkubwa,” aliongeza Dk. Saidia.


  Dk. Saidia alieleza kuwa kitu kingine wanachokipinga ni kitendo cha Serikali kutumia hospitali hiyo kubwa nchini kuwa kituo cha kuwapumzisha viongozi wanaopata matatizo ya kiafya kabla ya kuwapeleka nchini India kupatiwa matibabu. Alisema hakuna maana kwa Serikali kuendelea kutumia pesa nyingi kwa ajili ya kuwasomesha wataalamu wa tiba ikiwa haiwaamini na badala yake inawapeleka nje viongozi kutibiwa hata kama magonjwa yao yangeweza kutibiwa nchini.

  Alieleza jambo hilo linawasikitisha kwa kiasi kikubwa na kwamba viongozi wengi sasa wanaona hospitali hiyo ni kama sehemu ya kufanyiwa uchunguzi wa awali tu, kisha matibabu yote yanafanyika India, kitu ambacho alisema kinakatisha tamaa. “Serikali inawasomesha wataalamu wengi nje ya nchi, wengi tumesoma ili kuwatumikia wananchi, sasa kama viongozi wetu hawatuthamini wanatudharau na kuona hatufai kuwatibu kuna maana gani ya kutusomesha?” alihoji huku akishangiliwa na wafanyakazi wenzake.
  Aliendelea: “Tunachotaka wao wawe watu wa mfano kwa kupenda kutibiwa hapa hapa Muhimbili, uwezo tunao wa kutoa tiba.”


  Mfanyakazi mwingine, Amisita Lungu, alisema wakati umefika kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuangalia utaratibu wa kuwaruhusu wafanyakazi hao kutafuta mfuko wa hifadhi ya jamii wenye mafao mazuri kutokana wengi wao waliostafu kuwa masikini kutokana na kupata mafao madogo. Alisema wakati wanafanyakazi kwenye mazingira magumu, wanatarajia wanapomaliza muda wao wa ajira kuwa na maisha mazuri, lakini ndoto hiyo imeyeyuka baada ya uongozi wa hospitali kushindwa kufanyia kazi. Aidha, kitu kingine ambacho wafanyakazi hao wamelalamikia ni tofauti za mishahara kwa baadhi ya wafanyakazi ambao wanafanya kazi ya aina moja pamoja na kupewa huduma duni ya Bima ya Afya ambayo walieleza kuwa hailingani na michango wanayotoa.


  IPPMedia
   
 2. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Naona sasa viongozi wanaweza kujenga chuki kiasi kwamba watakapokwenda kwelnye uchunguzi wa awali kuelekea India, wanaweza kuishia kuchomwa sindano za sumu ili wafie mbele ya safari. Ndio, sasa kama hawa wamesomeshwa ili watoe tiba na hawaaminiki, si bora tu kubadilisha matumizi? Hata mganga na mchawi hawana tofauti kiufundi, ila mmoja anaamua kuwa kwenye upande wa ku-attack na mwingine wa kuzuia.

  Viongozi wabadilike na tushirikiane kuijenga nchi yetu pamoja. Tukitumia kidogo tulichonacho pamoja na sio tu kuwapa wachache wenye meno kutafuna kwa ajili yetu.
   
 3. c

  cutienoe Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani bora leo wameamua kusema ukweli lakini wamesahau kuiomba serikali iwaongezee posho kutoka elfu kumi hadi laki moja.....ikishindikana wafanye kama kenya.
   
 4. k

  kingukitano JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,971
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Madaktari wetu nawaunga mkono lakini kwa hili la kupeleka watu India nawapinga,wengi wa madaktari wetu hawako serious na kazi,hawafanyi kazi kwa weledi na kusababisha mauti kwa wagonjwa wengi nchini.

  kiongozi kama waziri ni kiongozi wa kitaifa lazima apate huduma ya uhakika ili kulitumikia taifa, angalia kipindi wamempasua kichwa mgonjwa wa mguu na wakichwa hali kadhalika,utasema una madaktari serious na kazi,tuache unafiki taifa limejaa wataalamu wasiojituma wanalilia hela tuu, hatuna uzalendo kwa watu wetu na kazi tunaona kama upuuzi fulani.

  kuna wakati moja ya mtu wa karibu alifanyiwa upasuaji wa mguu. Mguu ukapinda akawa hawezi kutembea baada ya kupelekwa India wahindi wakamtibu wakagundua madaktari wetu walishindwa kuunga mfupa sawasawa na kumsababishia ulemavu, hawa wa India wakamtibu na hadi sasa anadunda kama kawaida, hawana utaalamu hilo walikubali, Moi wamepewa nyenzo zote lakini hakuna kitu pale.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Madaktari bingwa wameanika ukweli, maana ninachokisoma sikiamini kwamba posho ya daktari ni elfu kumi tu na majukumu mazito aliyo nayo na halafu mbunge kwenda kulala uzingizi bungeni alipwe ziada ya malakini ya pesa kutoka jasho la walipa kodi, ni aibu kubwa sana kwa serikali yetu.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe, katika utendaji wa madaktari wetu ovyo kabisa. Matbabu pale ukiona hata vigogo wanakimbilia nje, je itakuwje kwa mlala hoi?
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hawa madaktari wana haki ya kudai malipo bora lakini jambo ambalo limekuwa linanipa shida kuelewa ni matumizi ya neno 'bingwa'. Kama wao ni madaktari bingwa kwa nini wagonjwa (kiongozi mgonjwa ni mgonjwa tu) wanapelekwa India? Ubingwa wao ni kwenye nini hasa? Tanzania tumezidi tamaa ya kutaka vyeo vya mng'aro. Daktari bingwa?
   
 8. G

  Galinsanga Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni sawa kundi la afya ni dogo sana na yet mhimu sana waongezewe pia posho.
  Ni rahisi kupandisha posho/mshahara wa kundi dogo la watumishi kuliko kundi kubwa e.g waalimu.
  Hii ni kwa kuzingatia kuwa unapokuwa umepandisha ni irreversible, mtumishi hawezi kukuelewa katika mazingira ya kawaida kumwambia kuwa umeshusha rate ya pay aina yoyote ile.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Daktari ni daktari tu hakuna cha ubingwa katika madaktari tunaowaona kila siku. Wote wamevaa pima joto shingoni kama kila daktari anavyofanya.

  Bingwa ni yule anayepambanishwa na wengine na kisha kuibuka kuwazidi wenzake na hivyo kuwa bingwa kama timu za mpira zinavyochezwa katika ligi kupata bingwa. Sasa hawa madaktari kujiita mabingwa ni kwa itikadi gani? Na walimu wajiite mabingwa kwa vile ndio waliwafundisha somo la sayansi lililowapatia udaktari? Kila mmoja sasa atajiita bingwa kama wanasiasa wanavyojipachika hadhi ya Dr .....
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  wakomae kwa sana tu
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwakuwa wanafikia MoI,if i were a dr ningekua napendekeza wakatwe miguu tu!
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nachofikiri tatzo ni MASLAH,hawa jamaa wanawahudumia watu wengi,kuliko kipato chao
   
 13. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  hivi na wewe kweli ni great thinker?
   
 14. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #14
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  laiti ungejitambua ungejisalimisha muhimbili national hospt,psychiatric unit!!!!!!unaumwa!!!
   
 15. Kinyengeli

  Kinyengeli JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ila kwa kweli inasikitisha sana posho ya Daktari Bingwa Tshs 10,000 wakati Mb hata asiposema lolote bungeni ili mradi asaini tu anabeba kilo 2. Kweli nimeamini maisha bora kwa kila Mbunge yanawezekana
   
 16. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  bingwa= specialist dr, mambo ya kiswahili hayo. Wagonjwa kupelekwa nje ni kutokana na ukosefu wa vitendea kazi vya kisasa ktk hospital zetu.. kuna madaktari bingwa wengi sana lkn kutokana na mfumo uliopo [lack of departmentalization] wanajikuta wanafanya kazi zisizowahusu [eg; cardiologist anatibu mifupa, malaria, anazalisha etc]. viongozi kutibiwa nje ni ubinafsi wa wateule wenyewe kwakuwa hawalipii hizo gharama wenyewe mfano ni yule mama waziri aliyekwenda kujifungua USA
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sio kila bingwa anatokana na mashindano dogo... Wao ni specialists na kiswahili fasaha kimeamua hivyo. Hata conrad murray ni bingwa pia

  thanks dr. Saidia, sasa ni zamu ya all professions kusimama na kuhesabiwa
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Dec 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks
   
 19. u

  utantambua JF-Expert Member

  #19
  Dec 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe kama ni mmoja kati ya hao mawaziri ama viongozi wakubwa wa kiserikali tuachieni Muhimbili na wataalamu wetu sisi tunawaamnini na ndio kimbilio letu. Endelea kwenda india ukatibiwe na kina kanjibai sisi tutaponea hapa hapa Muhimbili
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  Dec 15, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Oya HAKUNA cardiologist anayezalisha. Niambie ni kwenye hospitali gani imetokea hivyo?
   
Loading...