Muhimbili kumenikumbusha kuwa kuna kifo

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,646
Habarini wapendwa,

Poleni kwa wale wote ambao wamepoteza ndugu zao kutokana na ajali ya moto ya morogoro(msamvu)
Niende kwenye mada.

Naweza kusema kuwa hakuna ajali ambayo ilinigusa moyo katika maisha yangu kama hii ya gari la mafuta ya morogoro.Toka siku tukio linatokea nilikuwa nikifatilia kila hatua,kiasi kilichonifanya jana niende muhimbili na kujitolea damu kwa mara ya kwanza katika maisha yangu,

Baada ya kujitolea damu nilipita kidogo wodi ya sewa haji kuwaangalia ndugu zetu ambao waliungua na huo moto hakika machozi hayakuwa yanakauka,baada ya hapo nikajikaza kisabuni nikajichanganya na bimkubwa mmoja kwa kujifanya kuwa huyo mwanake ni rafiki yangu,huku dhumuni kubwa likiwa ni kuingia (ICU)

Bahati nzuri bimkubwa akanielewa tukaandika pale kuwa mimi ni mdogo wa mgonjwa na yule ndo mama yake basi tukavua viatu then tukapewa kama vindala flani hivi ambavyo havitoi sauti hakika niliyoyashuhudia yanatisha hakika kuna watu wameungua kuanzia unyayo mpka nywele,ilifkia hatua mpka baadhi ya ndugu wakawa wanasema ni bora ndugu yao afe kutokana na jinsi alivyoungua maana asilimia za kupona unaona kabisa huyu mtu uwezo wa kupona ni 10%,hali inatisha mno.

Pongezi
hakika nitoe shukrani zangu za dhati kama mwananchi kwa serikali na hata madaktari kwani walikuwa hawapishani wodini kuwahudumia na kutokuchoka kabisa kuwahudumia hakika tungekuwa ni sisi hakika tungekuwa tunawaacha na kuwaangalia tu tusubiri muda.Nilijiskia pia faraja mno kwa kuwakuta ndugu zangu wa dar waliokuja kujitolea damu hakika kwa hali waliyokuwa nayo wenzetu unaweza kuomba utolewe hata damu nusu ya iliyopo mwilini mwako uchangie.

Kwa wale ambao hamjafanikiwa kujitolea damu kama mchango kwa wenzetu ni ombi langu kwenu kujitokeza na kwenda kuwachangia wenzetu kwani japo tumejitokeza baadhi kuchangia lakini damu bado haitoshi.

Hakika ukitaka kujua kuwa kuna kifo na kifo kipo tembelea muhimbili

JB
 
Chanzo cha ajali ile ni umaskini na ukosefu wa elimu....
 
Sipendi kabisa kwenda hospitali kuwaona wagonjwa. Wagonjwa wengi wako mahututi ama wana majeruhi ya kutisha. Huwa inanikosesha raha sana kuwaona binadamu wenzangu katika hali hiyo, lakini hakuna jinsi ni lazima uende tu kama kuna ndugu, jamaa au rafiki kalazwa huko. Hongera sana kwa kujitolea.
 
Back
Top Bottom