Muhimbili kulikoni mnamtangaza mtu marehemu wakati amezimia tu!

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,358
349
Jana asubuhi muhimbili wamefanya kituko kingine kwa ku declare bint mmoja wa kichaga kuwa mfu, mume wa marehemu akaachwa hoi na breaking news hiyo. Kijana akawaarifu wafanyakazi wenzake na wazazi wa marehemu mkewe na safari ya kuanzisha maombolezo nyumbani ikatimu huku akimwacha ndg yake na rafiki mkubwa akiendelea na kuratibu utunzaji wa mwili.

Mwili ukachukuliwa kwa mujibu wa taratibu za mogue operators wa muhimbili huku shemejie akiongozana na wadau wa mogue ghafla shemeji akahisi life fighting ktk mchakato wa uhifadhi.

Akahoji na kuidadisi hali hiyo, lucky enough wadau wa mogue wakaikubali hoja ya shem, mdada kumbe yu hai @@. Je ni muujiza au bahati kwa huyu bint?

Kama shem asingelikuwapo nini kingejiri? Je dr muhusika amelihandle vipi jambo kabla na baada, Muhimbili kulikoni?
Acheni mungu aitwe Mungu
 
Unajua tunaishi kwa neema tu. Ukiona umeamka asubuhi umeenda unakoenda na kurudi salama si kwa uweza wako ni NEEMA. Hiki ni kituko cha karne! pole kwa familia.
 
Bora ingekua valuuu,na zile zakutengenezewa lab. Mana ndo wanazipenda wanahic zina walaishia kazi kumbe ndo wanabugi nakutupotezea watoto wetu full shame jombaa
 
Sijui watajifunza lini hao watu wa muhimbili....Lile sakata la mtukupasuliwa kichwa badala ya mguu nikilikumbuka linanipa hasira sana. Huyo dada kama angekurukupuka hao jamaa wa mostuari wako peke yao wangempiga kabali ili azimike kisha wanampeleka. Dah!! Kweli bongo utata mtupu!!
 
Na vile c unawajua walivyochoka hapa unaweza kukuta kabali inge husika ili kupunguza ushaidi na wakisha bwia nyagi zao ndo kabsaaaa!!
 
Tuna mahali pakusemea hili likasilizwa kwa haraka kama masaa ishirini na nne (24) ya mafuta? Hapo Muhimbili pana majambo
 
Msilaumu hao madakitari bwana, maisha magumu mpaka hakumbuki kitu, Nyumbani hajaacha posho ya msosi, mtoto karudishwa shule hajamaliza ada, mwenye nyumba anadai kodi ya nyumba ya miezi 2 kamwambia kesho anakuja na yeye hana hata pee mfukoni, mkweche alionao alinunua kwa mkopo marejesho ya mwisho wiki ijao, bado mkweche wenyewe upo gereji, mafundi wanadai chao wiki ya pili sasa, wanadai asipolipa watalipiga sell wachukue chao wamrudishie chenchi yake, nyumba ndogo bibie ana mimba miezi 8 sasa, kujifungua mwezi ujao, hakuna maandalizi, TOBA YALAH
 
Source........
<br />
<br />
NENDA MUHIMBILI ULIZIA NINI KILIMTOKEA BI NGOWI ASUBUHI YA ALHAMIS, NILIPENDA KUFAHAMU MEDIA INDUSTRY YETU IKO ACTIVE KIASI GANI JUU YA JAMBO LA HATARI KAMA HILI, TAARIFA SIYO TETESI MOD NI UKWELI MTUPU. FATILIENI MJE NA MABORESHO
 
Media yetu imelala kama tyson bungeni!!! Pengine shigongo & team watalifuatilia kwa kina. Nawapa changamoto ya hili na uwajibikaji kwa manufaa ya umma wetu
 
NENDA MUHIMBILI ULIZIA NINI KILIMTOKEA BI NGOWI ASUBUHI YA ALHAMIS, NILIPENDA KUFAHAMU MEDIA INDUSTRY YETU IKO ACTIVE KIASI GANI JUU YA JAMBO LA HATARI KAMA HILI, TAARIFA SIYO TETESI MOD NI UKWELI MTUPU. FATILIENI MJE NA MABORESHO

mkuu hii habari ni ya kweli kabisa maana ilikuwa itokee taharuki kati ya madokta vs ndugu na jamaa waliomsindikiza mfanyakazi mwenzao, wakawaambia ndugu yao wamemuona ni mzima na ole wao wamkute marehemu!
MUHIMBILI HII AIBU SANA.
 
wangeshughulika na huyo dr aliye certify death! kuna issue ilitokea internally lakini, dr wa usiku ka-sign kabisa death certification ili asiamshwe halafu mgonjwa hakufa. asubuhi round inakutwa. yaani huku 3rd world odds ration ya kufa ni 1000 times aisee! yakikukosa magonjwa na ajali,kuna uchawi na uzembe! kha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom