Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia msemaji wake bwana Aminieli Bubelwa Eligaesha, imesema kufuta utaratibu wa ndugu kutembelea wagonjwa muda wa mchana kuanzia saa sita mpaka nane mchana, badala yake Hospitali ya Taifa imetangaza utaratibu mpya wa kulisha wagonjwa.
Utaratibu huo umefutwa kutokana na kuingiliana na shughuli za kitabibu kwa wagonjwa muda huo wa mchana.
Muda wa kuona wagonjwa utabaki kuwa asubuhi saa 12 na jioni saa 12.
========
Hatimaye hospitali ya taifa Muhimbili yazidi kuboresha huduma zake kwa wagonjwa kwa kuingia ubia na mzabuni ili kutoa huduma ya chakula kwa wagonjwa wote waliolazwa hospitalini hapo.
Uboreshwaji wa huduma hii ni kutaka hospitali kujikita katika majukumu yake ya msingi na kuondokana na msongamano wa watu ndani ya hospitali toka asubuhi saa 12 mpaka saa 12 jioni kwani huingiliana na utoaji huduma hasa kwa saa za mchana huku ikisisitiza utaratibu huo kuanza kutumika kuanzia julai mosi mwaka huu.
Baadhi ya ndugu wa wagonjwa wameliunga mkono suala hilo na wengine wakisema kuwa huduma hiyo itawaondolea gharama kubwa hususani za usafiri wa kuja hospitalini mara tatu kwa siku na baadhi ya ndugu wamekuwa wakishindwa kuwaletea chakula wagonjwa wao hususani wagonjwa wanaotoka mikoani na wasio na ndugu hapa Dar es Salaam.
Chanzo: ITV
Maoni Yangu
Ni vyema utaratibu huo lakini bado nina mashaka kama wataweza kuhudumia wagonjwa wote kwa huduma iliyo bora kabisa.
Muhimbili ina wagonjwa wengi sana kuanzia wazazi,watoto,walopata ajali,waathirika wa VVU.
Tunajua huduma zilivyo mbovu,miundombinu hovyo na sasa wanajitishwa hili la kulisha wagonjwa, si ndio mwanzo wa kulishana Ugali na Maharage!! Kumbuka kila mgonjwa kuna chakula anachokipenda pindi aumwapo, nafikiria itakuwaje.Hakika nina mashaka.