Muhimbili Health Check.

Dec 5, 2011
78
93
Kuna rafiki yangu aliniforwardia hili tangazo la health check muhimbili kama miezi sita iliyopita.
Jumamosi iliyopita nilienda kwa kweli nilifurahia sana huduma zao.
Nimeona sio vibaya kuliweka hili tangazo hapa kwa wana JF wenzangu nao wakalisoma na kwa wanaoweza kufanya hii check up angalau mara moja kwa mwaka wakajua sehemu ya kwenda kufanyia, hii kitu ni muhimu sana katika maisha. Tusiwe tunafanya service za magari tukasahau za miili yetu pia! Jisomee mwenyewe hilo Tangazo!

TANGAZO KWA WANANCHI WOTE KUHUSU UCHUNGUZI WAAFYA
Hospitali ya Taifa Muhimbili inafurahikuwakaribisha wananchi wote kwenye huduma za upimaji wa afya kwa gharama nafuu.Baadhi ya magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu (high blood pressure) nasaratani (cancer) hayana dalili zozote hadi yanapokuwa yameadhiri sehemu nyingiza mwili na kuleta madhara makubwa. Kwa mfano, wagonjwa wengi wa kisukari(Diabetes) hugunduliwa kwa sababu ya kupoteza fahamu ambayo hutokea ghafla baadaya ugonjwa kuanza. Shinikizo la damu (high blood pressure) inaweza kugundulikakwa mara ya kwanza mgonjwa anapopata kiharusi (Stroke) au anapogunduliwa kuwana ugonjwa wa figo, moyo kushindwa kufanya kazi, n.k. Hali hii inathibitishwa na takwimu mbalimblihapa hospitalini ambazo zinaonyesha kuongezeka kwa idadi kubwa ya wagonjwaambao wanaletwa wakati wameshaathirika sana kiasi cha kuwa ngumu kwa madaktarina wahudumu wa afya kuwasaidia kurudikatika hali yao ya awali kitu ambacho kingeweza kuzuiwa kama hali hioingejulikana mapema Huduma zinatolewa saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana kila siku za jumamosi katika jengola wagonjwa wa nje (cold clinic) ambalo ni jengola kwanza upande wa kushoto unapoingia kupitia geti la kuingilia magari Hospitali ya Taifa, Muhimbili. Huduma hii inatolewa na wataalamu bingwa waliobobea kwenyefani zate za afya katika hospitalai hii ya Taifa. Huduma zinatolewa katika mfumo wa vifurushi(packages) zinazojumuisha mahojiano katiya mteja na mhudumu wa afya kwa kina, upimaji wa mwili kitabibu vipimo vyamaabara (FBP,Lipid profile, VDRL,Hepatitis, Blood Glucose, Renal profile, Liverenzymes, PSA, Urinalysis, Stool analysis), radiologia (Chest X­-ray,mammography) na kipimo cha moyo ECG. Vipimo kama Ultrasound,ECHO, CT-Scan naMRI vitafanyika vinapohitajika na sio sehemu ya vifurushi hivyo. Huduma hii ni ya kulipia lakini bei yake ninafuu ulikinganisha na huduma ya kibingwa itakayotolewa kwa mteja. Gharama yauchunguzi huu kwa kifurushi ni Tsh.188,000 kwa mwanaume na Tsh.193,000 kwa mwanamke. Mwisho wa huduma ushauri wa kitaalamu utatolewakwa tatizo lolote litakaloonekana na mgonjwa ataingizwa katika clinic zahospitali za madaktari bingwa kutokana na tatizo lake. Kama hakuna tatizolililoonekana ushauri utatolewa namna ya kujikinga au kuepuka magonjwambalimbali na jinsi ya kuishi kwa afya njema. Kwa mawasiliano na kuweka appointment wasiliana na afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Barua pepe (Email) healthcheck@mnh.ac.tz au mnhhealthcheck@gmail.com Pia unaweza kutembelea Website yetu www.mnh.ac.tz
KUMBUKA, KINGA NI BORA KULIKO TIBA
 
Tafadhali kaka naomba namba zao za simu kama unazo sababu nimejaribu kutuma email bila kupata jibu kutoka kwao.Asante
 
Back
Top Bottom