Muhimbili: Aliyepasuliwa kichwa MOI apooza upande

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Posted Date::11/19/2007
Muhimbili: Aliyepasuliwa kichwa MOI apooza upande
Na Jackson Odoyo
Mwananchi

MGONJWA Emmanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu Novemba Mosi, mwaka huu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) amepooza upande mmoja wa mwili wake.

Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi ndugu wa mgonjwa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa kuwa si msemaji wa familia, alisema licha ya kuwa ndugu yake hajaanza kuzungumza, kukaa wala kutembea pia hivi sasa amepooza upande mmoja, suala ambalo pia lilithibitishwa na baadhi ya madaktari bingwa wa upasuaji katika taasisi hiyo.

Alisema baada ya kugundua hali hiyo walimuuliza daktari anayemuhudumia aliyemtaja kwa jina moja la Dk Kinasha ambaye alikiri kwamba hali hiyo haiwezi kutibiwa kwa sasa, badala yake wanajaribu kumfanyia uchunguzi wa kina ili aweze kurudia hali yake ya kawaida.

Pamoja na matatizo aliyonayo ya kutoweza kuzungumza, kukaa wala kutembea pia amepooza upande mmoja hali hiyo inazidi kutupa wasiwasi kama kweli ataweza kupona, kwa sababu kila kukicha kuna matatizo mapya yanaibuka, na tukiwauliza madaktari hawatupi majibu ya uhakika,? alisema ndugu wa mgonjwa huyo.

Alifafanua kwamba hivi sasa wana mikakati ya kumuona Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa kwa mazungumzo ya kina kuhusiana suala hilo, ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalam.

Aliongeza kwa sasa wanafamilia hawajaamua la kufanya kwasababu uongozi wa taasisi hiyo uliwaomba wasubiri mpaka tume iliyoundwa na Mkurugenzi wa MOI, Profesa Laurent Museru kuchunguza tukio hilo itakapotoa taarifa yake.

Mbali na madai hayo ya ndugu, mwandishi wa habari hizi pia alizungumza na baadhi ya madaktari bingwa wa upasuaji katika taasisi hiyo (majina yamehifadhiwa) ambao walithibitisha kwamba mgonjwa huyo kapooza.

Mbali na mgonjwa huyo pia mwenzake Emmanuel Mgaya ambaye alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa alitegemewa kufanyiwa upasuaji wa kichwa jana ili kutibu tatizo linalomsumbua.

Kwa mujubu wa ndugu wa karibu wa mgonjwa huyo aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi, Mgaya alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa jana.

Taarifa hizo zilizotolewa na baadhi ya madaktari wa taasisi hiyo zinasema kuwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo aliwatangazia kwenye kikao chao cha utendeji cha asubuhi kwamba mgonjwa huyo alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa jana.

Alisema kwamba mbali na tangazo hilo pia alitangaza kuwasimamisha kazi watu wawili ambao ni daktari aliyetakiwa kumfanyia Emmanuel Didas upasuaji wa mguu kwasababu mgonjwa huyo hakuwa kwenye orodha ya wagonjwa waliotakiwa kufanyiwa upasuaji siku hiyo.

Mwingine aliyesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana ni mwandaaji wa orodha ya wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji kwakutoingiza jina la mgonjwa huyo katika orodha.

Upasuaji huo tata, ulilazimisha Bodi ya MOI, kuagiza uongozi kuunda Tume kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo. Tayari Tume imeshamaliza kazi na kuwasilisha ripoti yake kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya hatua zaidi.
 
duhh Mungu amsaidie mgonjwa apate nafuu haraka na familia yake pia ifarijiwe na Mungu...mtanzania mwenzetu huyuuu
 
duhh Mungu amsaidie mgonjwa apate nafuu haraka na familia yake pia ifarijiwe na Mungu...mtanzania mwenzetu huyuuu

Ingekuwa ni jambo la busara kama kungeanza taratibu za kisheria kuifikisha mahakamani serikali, naona kama ujanja ujanja umeanza kufanyika ili kuifunika issue hii. Uchunguzi unaofanyika hapa bongo ni vigumu sana kuuamini, hata ukiwa na matokeo mazuri utekelezaji wake unafanyika baada ya waathirika kufa.
Iko wapi kesi ya Dito, iko wapi kesi ya Zombe, walioathirika ndio wameliwa, hakuna haki watakayopata.
 
Poleni sana Ndugu wote wa mgonjwa. Bahati mbaya Mwenyezi Mungu akichukua roho yake muende Mahakamani kwa uzembe mkubwa ulifanywa na Madaktari waliomtibu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom