Muhimbili: Aliyepasuliwa kichwa MOI apooza upande | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimbili: Aliyepasuliwa kichwa MOI apooza upande

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zee la shamba, Nov 19, 2007.

 1. Zee la shamba

  Zee la shamba Member

  #1
  Nov 19, 2007
  Joined: Oct 17, 2007
  Messages: 55
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Na Jackson Odoyo

  MGONJWA Emmanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu Novemba Mosi, mwaka huu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) amepooza upande mmoja wa mwili wake.


  Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi ndugu wa mgonjwa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa kuwa si msemaji wa familia, alisema licha ya kuwa ndugu yake hajaanza kuzungumza, kukaa wala kutembea pia hivi sasa amepooza upande mmoja, suala ambalo pia lilithibitishwa na baadhi ya madaktari bingwa wa upasuaji katika taasisi hiyo.


  Alisema baada ya kugundua hali hiyo walimuuliza daktari anayemuhudumia aliyemtaja kwa jina moja la Dk Kinasha ambaye alikiri kwamba hali hiyo haiwezi kutibiwa kwa sasa, badala yake wanajaribu kumfanyia uchunguzi wa kina ili aweze kurudia hali yake ya kawaida.


  ?Pamoja na matatizo aliyonayo ya kutoweza kuzungumza, kukaa wala kutembea pia amepooza upande mmoja hali hiyo inazidi kutupa wasiwasi kama kweli ataweza kupona, kwa sababu kila kukicha kuna matatizo mapya yanaibuka, na tukiwauliza madaktari hawatupi majibu ya uhakika,? alisema ndugu wa mgonjwa huyo.


  Alifafanua kwamba hivi sasa wana mikakati ya kumuona Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa kwa mazungumzo ya kina kuhusiana suala hilo, ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalam.


  Aliongeza kwa sasa wanafamilia hawajaamua la kufanya kwasababu uongozi wa taasisi hiyo uliwaomba wasubiri mpaka tume iliyoundwa na Mkurugenzi wa MOI, Profesa Laurent Museru kuchunguza tukio hilo itakapotoa taarifa yake.


  Mbali na madai hayo ya ndugu, mwandishi wa habari hizi pia alizungumza na baadhi ya madaktari bingwa wa upasuaji katika taasisi hiyo (majina yamehifadhiwa) ambao walithibitisha kwamba mgonjwa huyo kapooza.


  Mbali na mgonjwa huyo pia mwenzake Emmanuel Mgaya ambaye alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa alitegemewa kufanyiwa upasuaji wa kichwa jana ili kutibu tatizo linalomsumbua.


  Kwa mujubu wa ndugu wa karibu wa mgonjwa huyo aliyezungumza na mwandishi wa habari hizi, Mgaya alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa jana.


  Taarifa hizo zilizotolewa na baadhi ya madaktari wa taasisi hiyo zinasema kuwa Mkurugenzi wa taasisi hiyo aliwatangazia kwenye kikao chao cha utendeji cha asubuhi kwamba mgonjwa huyo alitakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa jana.


  Alisema kwamba mbali na tangazo hilo pia alitangaza kuwasimamisha kazi watu wawili ambao ni daktari aliyetakiwa kumfanyia Emmanuel Didas upasuaji wa mguu kwasababu mgonjwa huyo hakuwa kwenye orodha ya wagonjwa waliotakiwa kufanyiwa upasuaji siku hiyo.


  Mwingine aliyesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana ni mwandaaji wa orodha ya wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji kwakutoingiza jina la mgonjwa huyo katika orodha.


  Upasuaji huo tata, ulilazimisha Bodi ya MOI, kuagiza uongozi kuunda Tume kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo. Tayari Tume imeshamaliza kazi na kuwasilisha ripoti yake kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya hatua zaidi.

  Source: mwananchi Newspaper
   
 2. D

  Dotori JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2007
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  I see it as a system problem, rather than individual health worker problem.
   
 3. ViciousRecklessSavage!!!

  ViciousRecklessSavage!!! Senior Member

  #3
  Nov 21, 2007
  Joined: Jun 23, 2007
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Simply mind boggling! This tragic case elevates Bantu incompetency and inefficiency to a whole new level!! Even pissy nursery school kids could have come up with a better diagnosis. Never ever put your life under trust of these insane Bantu daktaris.
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Una Uhakika Wote Ni Bantus Hao Daktaris ?
   
 5. ViciousRecklessSavage!!!

  ViciousRecklessSavage!!! Senior Member

  #5
  Nov 21, 2007
  Joined: Jun 23, 2007
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I've just received a warning so no more talk about "Bantus".
   
 6. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2007
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,612
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Hii kitu nchi zenye sheria za maana, muda kama huu kunakuwa na law suit kama tano hivi.
  Blanda katika udaktari ipo duniani kote, sema law suit inapunguza huu ushenzi. Yaani mnasue kiasi kwamba huyo dk kila cent anayo make mpaka anakufa familia inachukua 70%.
   
 7. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  mtanganyika umenena,ila bongo ndio imetoka ni sawa na ajali kazini.
  nilisoma kwenye md,kuwa ripoti itawekwa adharani leo je kunaaliye pata kunusa au ndio bado siri ya sirikali
   
 8. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2007
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Katibu tarafa, nani alikwambia Tanzania tunatoaga riport hadharani? labda hii ya madini kwa sababu Zitto yumo! Just thinking loud!!!!!!!!!!!
   
Loading...