Muheza,Tanga; Dc awataka wanaume wanaochezea kichapo kutoka kwa wake zao kutoa taarifa kwenye vyombo vya Sheria

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Serikali wilayani Muheza mkoani Tanga imewataka wanaume ambao wamekuwa wakinyanyaswa kwa kupewa vipigo na wake zao kutonyamaza, badala yake watoe taarifa kwa vyombo husika, ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Muheza, Halima Bulembo, wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji Cha Magoda kata ya kisiwani, wakati akikamilisha ziara ya vijiji 29 Kati ya 126 vilivyomo katika Tarafa ya amani.

"Wanaume wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na msongo wa mawazo, kwa upande wa wanawake Wana uwezo wa kusema matatizo yao, kwa ndugu na jamaa zao, lakini wanaume Wana aibu, msione haya, nipigieni simu nitamwita mwanamke husika ili nimwonye" alisema

______________________________________________________________________

Ushauri wangu!
Kama wewe Ni mwanaume na unatembezewa kichapo na mkeo, basi wewe ni dume Suruali! Badilika
 
Wanasema mapenzi yamezaliwa Tanga, hata kama mwanaume wa Tanga si kurendemka kiasi hiko hadi unakung'utwa na mkeo...KAZA


Kibongo bongo ukiwapa kipondo/kichapo/kisago wanawake ni habari kubwa na utafuatiliwa na mapolisi, wanaharakati wa haki za binadamu na watoto na wanajamii... ila nakuhakikishia kwamba story za wanaume kupigwa na wake zao SIO HABARI KUBWA

SASA NDIO NAJIULIZAGA WANAUME NA SISI SIO BINADAMU? NA HAO WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU MBONA HUWA HAWAPAZI SAUTI KWA UKALI KAMA AMBAVYO WANAWAKE WAKIPIGWA? NA HAPO HAPO WANATAKA USAWA WA KIJINSIA, utakujaje usawa na wakati haki sawa haipo?
 
watasema umefanya unyanyasaji/uonevu wa kijinsia
Hahahah' wanasema Kama mbwai na iwe mbwai, Yan kupigwa na mke wangu kabisa!!? Hata kunifokea TU hlo n kosa la jinai, maana hata Mimi kumfokea ctak namweleza kwa lugha ya upole !
 
Mwanamke hapigwi,akikupiga we kunako usiku
Mpe shuguli nzito kunako kwenye bed tu

Ova
 
Mwanamke hapigwi,akikupiga we kunako usiku
Mpe shuguli nzito kunako kwenye bed tu

Ova
Assume amekupa kichapo mida ya jion, afu night utaanza kumwomba unyumba au itabidi akubake !

# siku hizi wanaume wanapigwa na kubakwa!
 
Back
Top Bottom