Muheshimiwa Zungu,mkurugenzi NEMC plastic bags ziko mtaani kama kawaida

kidumba

Member
Aug 16, 2013
54
125
Nilishangazwa siku moja kumuona muheshimiwa Zungu akishangaa kwenye vyombo vya habari kwamba kanunua bidhaa akafungiwa kwenye mifuko iliyopigwa marufuku bila muuzaji kuogopa,badala ya waziri Zungu kushangaa nilitegemea angesema keshamchukulia hatua muuzaji na tayari kalipa faini au yuko ndani ila haikuwa hivyo.

Tanzania ndo nchi pekee ambayo waziri anashangaa,mwananchi wa kawaida anashangaa na kila mtu anashangaa asijue cha kufanya juu ya jambo kama hili lililopigwa marufuku.

Mkuu wa nchi siku moja akipokea ripoti ya Takukuru alishangaa kwamba jambo linafanyikaje wilayani ambako uongozi mzima wa wilaya upo kuanzia mkuu wa wilaya,mpaka mtendaji wa mtaa,mifuko hii ilipigwa marufuku kisheria lakini ipo kwa wingi huku mtaani nikiwa Ikungulipu kule kwetu nimekutana na hizi PLASTIC BAG zinauzwa bila hofu mnadani.

Mimi nawakumbusha tu wenye dhamana msisubiri mkuu wa nchi akakutana na hizi plastic bag mtaani awaite mshindwe cha kujibu muombe msamaha kama waziri wa ujenzi msisubiri hatua hiyo maana huenda isiwafikie.

Hauhitaji kwenda mbali njoo hapa sokoni Afrika sana mifuko ya NON WOVEN iliyo chini ya kiwango ipo kwa sanaa ndo tunayofungiwa bidhaa wakazi wa eneo hili,PLASTIC BAG ndo tunafungiwa nyama,kuku,mchele,unga bila hata aibu.mimi nashangaa hizi taasisi hazina watu wanaoishi mazingira yetu waone hivi vitu na kuripoti kwa wakubwa wao?

Mifuko ya plastic huhitaji hata kutumia nguvu weka sheria ndogondogo za faini kuanzia ofisi ya mtaa atakayekamata plastic bag atalipwa nusu faini atakayotozwa mtuhumiwa uone kama utakutana na plastic bag au mfuko ulio chini ya kiwango mtaani.
2thumbnail.jpe
thumbnai.jpe
thumbnail.jpe
thumbnail2.jpe
 

Attachments

  • 3thumbnail.jpe
    File size
    105.6 KB
    Views
    0

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
777
1,000
Kumbe Mh Zungu ndio Waziri mwenye dhamana na Mazingira, mbona yupo kimya, atembelee masoko akutane na hizo 'mbanga'
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom