Muheshimiwa Jussa, siasa zako zimepitwa na wakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muheshimiwa Jussa, siasa zako zimepitwa na wakati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Apr 18, 2012.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  haya ndio wanayosema wazanzibari, kwa kweli ni maneno mazito na yenye ukweli wa kutosha kwa ndugu yetu hyu na baadhi ya wachache wenziwe


  MUHESHIMIWA JUSSA SIASA ZAKO ZIMEPITWA NA WAKATI

  Tunajuwa kila Mzanzibari angependelea kuona kuna mabadiliko katika Muungano,wengine wanapenda kuona kuna serikali tatu na wengine wanataka muungano uvunjike kabisa,na hi ndio maana ya demokrasia kuwa kila mtu awe na uhuru wa kuchaguwa.

  Kila unapopita kwenye maskani mazungumzo ni Muungano hakuna habari nyengine,na baadhi ya viongozi wameona watumie muda huu kwa kujipa umaarufu kwa manufaa yao wao wenyewe na sio kwa manufaa ya wananchi.

  Muheshimiwa Jussa wewe ni mmoja kati ya watu ambao tunakupa heshima ya juu kwa vile una elimu kushinda wawakilishi wengi lakini kitendo chako cha kutunga mswada wa kuwataka Watanganyika wasiajiriwe katika sekta ya utalii kilikuwa ni kitendo cha kijinga na upumbavu,mtu yoyote yule anaejuwa ukweli basi anajuwa kuwa huu ulikuwa mswada wa kujitafutia umaarufu kwa sababu hata wewe mwenyewe ulikuwa unajuwa kuwa mswada hauendi popote na ndio maana hata baadhi ya viongozi wenzako wa CUF pia hawajakusaidia kwa sababu walijuwa ni mswada wa kipuuzi na wa kijinga.

  Japokuwa umepata waafuasi wengi ambao wamependa ulichokifanya lakini watu hao ni wale mambumbumbu ambao kutwa wanakaa maskani na wako tayari kudanganywa na viongozi kama nyie,na watu hawa wa maskani hata uwape kazi hawatofanya kwa sababu kazi kwao sio kitu wanachokijuwa,na wewe Jussa baada ya kufahamu hivi ndio umeona uwaingie katika vichwa vyao kwa manufaa yako ili uonekane kwamba unafanya la maana.

  Hata kama hatukubaliani na Muungano lakini kwa sasa Muungano umedumu na hii ni nchi moja,sasa inakuwaje umwambie mwananchi asiweze kuajiriwa?Wewe huoni kitendo hicho kinaweza kusababisha madhara makubwa,umefikiria kama watu wa Bara wakisema na Wazanzibari wasiajiriwe katika kazi fulani je hali hii itakuwaje, je wewe utakuwa tayari kuchukuwa majukumu ikiwa kutatokea fujo kwa chuki za kijinga unazozipandikiza? La ukweli tuseme Bara kuna Wazanzibari wengi wenye biashara na wanaofanya kazi kuliko watu wa Bara wanaofanya kazi Zanzibar, tembelea kariakoo katizame nani anamiliki maduka wengi wao ni wageni tukiwamo sisi Wazanzibari.

  Muheshimiwa kama unataka kuwasaidia Wazanzibari basi kuna mengi ya kuwasaidia la kwanza waambie wasikae na kudehenyeka maskani waambie wakatafute riziki, Kuna vijana wengi wana vipaji vikubwa vya kutumia mikono yao,kwa nini serikali haiwaendelezi, unaonaje ukapitisha mswada wa kuwabana wizi na wabadhirifu wa mali ya umma katika serikali, unaonaje ukapeleka mswada wa kuimarisha kiwango cha elimu Zanzibar vijana wakanufaika, Au unaonaje ukapitisha mswada wa kuweza kuwakamata wala rushwa na wafanya biashara ya madawa ya kulevya?

  Lakini yote haya wewe hujayaona umeona upeleke ule muswada wa kipumbavu, tunakuomba usianzishe siasa za chuki kwani mwisho wa chuki ni fitna na baada ya fitna ni kuingiana mwilini,wewe umesoma kwa hiyo weka siasa pembeni na wasaidie wananchi kama kweli unataka usaidie na kama huna nia ya kusaidia basi tunakushauri ukae kimya,la mwisho Zanzibar inategemea utalii mpaka leo hakuna website ya serikali inayotangaza utalii unaonaje ukapeleka mswada huu ili ianzishwe website ya kuitangaza Zanzibar?

  Na sisi wananchi lazima tukae macho na kujuwa na kupambanuwa lipi zuri na lipi baya tutumie akili zetu sio unakubali na kupiga makofi kila unaloambiwa na kukaa maskani tupunguzeni! Mwenyezi Mungu anampa kila mja wake riziki lakini lazima hiyo riziki uitafute


  source: Group ya FB ya Wazanzibari "VOICE OF ZANZIBAR "
   
 2. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KUHUSU JUSSA:

  HIVI KWELI NI MZANZIBAR AU NI UNAFIKI TU HUO UNAOUFANYA? KAMA UMZANZIBAR BASI UNAENDELEZA SIASA ZA MAGAMBA (ccm). kama kweli humnafiki basi waambie watanganyika walitoe suala la mafuta. Sasa kama JUSSA anataka wazanzibar wapewe kipaumbele kwa suala la ajira, hilo kwani ni baya? mbona wao tanganyika wanapewa kipaumbele suala la ajira
   
 3. K

  Keil JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ukereketwa na Ufurukutwa ukizidi mwisho unakuwa mpumbavu. Huyo ndo Jussa, maana amesifiwa sana kwamba yeye ni mpambanaji stadi kichwa kikavimba. Matokeo yake ndo hayo!
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sasa mnabomoana wenyewe kwa wenyewe!!

  Mlimsifu sana huyo **** sasa anawaonyesha true colour
  Mbaguzi mkubwa
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  its seems like Jussa kuna kitu anajaribu kukipanda....tena anajaribu kwa nguvu kubwa
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Ntashangaa kama ataendelea kubaki salama akiendeleza hizi siasa za maji taka anazofanya. Atajichimbia shimoni soon
   
 7. a

  akelu kungisi Senior Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukimtizama na kumchunguza vizuri huyu jamaa ni mbaguzi asiye na mfano! Nina amini iwapo Nyerere angekuwepo kingempata kilichomkuta Aboud Jumbe.
  Ana mawazo ya kizamani, ni hatari kwa maendeleo ya taifa letu, amejionyesha hivyo kwa muda mrefu sana, cha kushangaza viongozi wakitaifa wanamfuga bila kumkemea!
  Infact, hata yeye kwanza sio Mzanzibari, yeye ni gabachori. Huyu jamaa anapashwa anyang'anywe nyadhifa zote alizonazo kwa ujinga wake wa kibaguzi.
   
 8. k

  kagame Senior Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 6, 2008
  Messages: 159
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mnaweza kudhania kuwa Jussa ana uwezo wa kuona mambo kama akina wengine, hapana, nawaomba msidhanie tena hivyo. Mwanasiasa huyo nilianza kumdharau baada ya kutoa mawazo yake baada ya uchaguzi mdogo wa Uzini, alionesha siyo ubaguzi tu bali chuki ya wazi aliyonayo kwa watanganyika, hivi bila muungano Znz ina nini cha kujivunia? Anajua athari za kuvunja muungano huu tulionao zitakuwa kubwa Znz kuliko Bara? Ana takwimu za idadi ya waznz walioko bara akilinganisha na wabara walioko znz? Ila kiburi alichonacho kinajengwa na viongozi waoga tulionao katika uongozi wa nchi, huyu alistahili kuwa matatizoni saizi kutokana na hizo kauli zake. Ukimwangalia Jussa mara moja unayaona makengeza aliyonayo ila kuna uwezekano makengeza yale hayajaishia machoni tu yamekwenda hadi kwenye ubongo. Poleni wananchi wa Mji mkongwe
   
 9. a

  akelu kungisi Senior Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kagame nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Kweli kabsa kwenye uchaguzi wa Uzini alitamka kauli moja ya kibaguzi na yenye udini ambayo hadi leo hii hakuna kiongozi yeyote aliyejitokeza hadharani kumkemea. Nanukuu ile kauli "CUF wameshindwa uchaguzi jimbo la Uzini kwa sababu wakristo ni wengi katika jimbo la Uzini". Tayari huyu jamaa kwa kauli hiyo ya kishenzi alipashwa ajambishwe na wakuu wake!
  Sure, makengeza aliyonayo hayajaishia machoni kwake, yameenda mpaka kwenye ubongo wake! Hatuhitaji kuumiza vichwa kufikiria kuhusu ukubwa au udogo wa Zanzibar, sisi tumeunganishwa na uzalendo uliokuwa na muingiliano wa damu pamoja na tamaduni zinazofanana bila kujali ukubwa wa Tanganyika na udogo wa visiwa vya Zanzibari.
  Tumkatae gabachori na upimbi wa makengeza yake!
   
 10. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Duh! Leo mtu wa pwani umeleta mnakasha murua sana.

  Huyo muhindi mbaguzi sana, tukisema na sisi watanganyika tuwabague ninyi huko kisiwani kisiwa kitazama.

  Msituchukulie poa kwa upole wetu!!
   
 11. a

  akelu kungisi Senior Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amejipambanua na kuonyesha asili yake, maana asili yake ndivyo walivyo, Wazanzibari wa asili na wenye nchi hiyo hawana upimbi wa fikra mfano wa huyu gabachori!
  Chuki aliyonayo dhidi ya Wabara anajitahidi aipandikize kwa Wazanzibari kwa malengo mahususi. Jusa, lengo lako tunalijua, lakini uelewe kuwa kabla hujaanza mikakati hiyo na baadhi ya wakubwa zako ambao wanakutumia kama vuvuzela tumejiandaa vilivyo kukubaliana nawe! Andika maumivu tu! Uko viganjani mwetu, sahau lengo lako na kundi lako!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  wamemuendekeza sana kiasi kwamba anaamini anazungumza kwa niaba ya "Wazanzibari" wote!! Hivi kilimshinda nini kuwahamasisha wazanzibari waende kutafuta kazi bara sehemu ambayo ni nchi yao? hawahitaji passport, hawahitaji n.k wanahitaji uamuzi tu wa kutoka visiwani? mbona miaka mingi wengi wamefanya hivyo? Hivi Wamasai si wametoka Arusha na wako karibu kila kona kutafuta "malisho" mema (pun inteded)? Wakusuma vile vile? Wakinga? kwanini Wazanzibari waone vibaya kutafuta na kufanya biashara bara?
   
 13. a

  akelu kungisi Senior Member

  #13
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji, anachokifanya Jusa ni mision ya wakubwa wachache wenye malengo mahususi, huyu jamaa ni vuvuzela tu. Wamemtumia huyu jamaa kwa kuwa hana uchungu na si mzalendo wa asili wa visiwani, hivyo anaropoka lolote ili muradi atimize matakwa ya wakubwa hao!
  Hatuna haja ya kuielezea historia na asili yetu wabara na wanzibari kwa muingiliano wa damu na tamaduni zetu, hii ni kuwa hata yeye Jusa na wakubwa hao anafahamika vizuri ila wamevimbiwa matumbo na ninahisi mapua yao yanapenda kunusa harufu ya damu! Tafsiri ya mambo na uchochezi wa kibaguzi wa kidini, siasa na kikanda anaoendelea kuufanya huyu jamaa ni kuwa anataka Tanzania yetu iwe kama Haiti ya zamani!
  Tumkatae na kumrudisha huyu gabachori kwenye tamaduni zetu Watanzania na umoja wetu wa asilia, kama ataendelea na ujinga wake njia nyeupe India!
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Kwa mtu makini ni lazima upembue jambo kabla kulitolea maamuzi.

  Nimepata bahati ya kuwauliza watu mbalimbali kule Unguja na hata Pemba kuhusu article hii ya Group ya FB ya Waznz lakin kila mtu alishangaa sana na nikapoteza tena muda kuwasiliana na Mh Jussa kwa simu na alisema hakuna kitu.

  Sasa labda mtoa mada tuweke wazi umeitoa wapi? ili ututoe kiu ya kuona kama umeitunga na kutaka kuifurahisha barza na wale wachache wasioipenda na kuitakia mema Znz na wa Znz.

  Na ukithibitisha hilo naomba uiweke kule Mzalendo ili waZnz waijadili kwa kina sana kwani hata Jussa mwenyewe yupo kule.

  Nashauri tuwe makini sio kuandika mambo wenyewe na kusingizia watu wengine kwa nia ya kuchafua watu na jamii zao.
   
 15. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kabla kuhukumu ni lazima tupate uhakika na usahihi wa habari yenyewe na chanzo chake.

  Kuwa na subra.

   
 16. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  Sitoshamshangaa akija na muswada wa kuyachoma moto Makanisa, huyu mtu ni mpumbavu wa viwango vya hali ya juu.
   
 17. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hypothetically by global warming protocol, zanzibar is one of those islands which are going to be submerged under sea level in the next 100 years.by the way i think these incitings from jussa are antagonistic to the motives which would be expected from the would be victims including jussa descendants. suppose mainlanders would become selfish and relactunt to let victims seek refuge from our descendants in our land as jussa behaves now, will they not be judged negatively and pleaded to calm down?
   
 18. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  Habari ni ya uhakika na huo muswada ni kweli ulikuwepo sasa wewe unataka subra hipi tena Sheikh wangu? nenda facebook kwenye Zanzibar group ndio source, na tafuta hansard kwenye baraza la wawakilishi utakutana na hii kitu. ni kwa nini unataka kumtetea huyu mwehu?
   
 19. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Baburubaru bana,
  Unachekesha kweli!!
  Huyo jusa and co hawezi kuja hapa kujadili?
  Au jf haipatikani zenji!!
   
 20. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mkuu Barubaru, unamaanisha chanzo cha hii "article" au mjadala wa Watanganyika kunyimwa kazi ZNZ?
   
Loading...