Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,183
- 10,654
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema marehemu Muhammad Ali aliongoza harakati za kutetea usawa wa watu wa rangi zote na alipigania haki za watu wenye asili ya Afrika.
Hossein Jaberi Ansari katika taarifa amesema Muhammad Ali aliamsha hisia za wanadamu kuhusu ubaguzi ulio dhidi ya ubinadamu.
Katika salamu za rambi rambi kufuatia kuaga dunia bingwa wa ndondi Marekani mwenye asili ya Afrika, Muhammad Ali siku ya Ijumaa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Muhammad Ali si tu kuwa alikuwa bingwa mashuhuri na wa kipekee katika masumbwi, bali pia alikuwa mwanamichezo mwenye heshima na jina lake litadumu." Amemtaja Muhammad Ali kwa sifa ya 'Pahlavan" ambayo katika utamaduni na mila za Kiirani ni mwanamichezo shujaa, mwenye heshima na mkarimu.
Msemaji wa Wizara ya mambo ya Nje ya Iran amesema jina la Muhammad Ali linakumbusha upinzani dhidi ya vita vinavyochochewa na madola ya kibeberu na kikoloni.
Bingwa huyo wa ndondi raia wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Muhammad Ali, akijulikana kama Cassius Clay kabla ya kusilimu, aliaga dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 74.
KULLU NAFSIN ZAIKATUL MAUT *R.I.P