Uchaguzi 2020 Muhambwe, Buhigwe sasa kuchagua wabunge Mei 16

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa wabunge katika majimbo ya Muhambwe na Buhigwe mkoani Kigoma pamoja na uchaguzi wa madiwani katika kata 18 za Tanzania Bara, utafanyika Mei 16, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Wilson Mahera kwenye mkutano wake na vyombo vya habari.

Dk Mahera alisema upigaji kura katika Jimbo la Muhambwe ulipangwa kufanyika Mei 2, mwaka huu, lakini kutokana na Jimbo la Buhigwe pia kuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Dk Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais, NEC kutokana na mamlaka iliyo nayo kisheria imeamua uchaguzi katika majimbo hayo ufanyike siku moja.

Alisema Machi 27, mwaka huu NEC ilitangaza ratiba ya Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Muhambwe ambapo uteuzi wa wagombea ulipangwa kufanyika Aprili 3 na upigaji kura ulipangwa kufanyika Mei 2, mwaka huu, hivyo licha ya uteuzi wa wagombea kufanyika lakini upigaji kura umesogezwa mbele.

Jimbo la Muhambwe liko wazi kutokana na kifo cha mbunge wake, Atashasta Nditiye aliyefariki dunia kwa ajali jijini Dodoma, Februari 12, mwaka huu.

“Kwa mujibu wa Kifungu cha 46(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343, Tume inayo mamlaka ya kufuta siku ya uchaguzi iliyopangwa awali na kupanga siku nyingine endapo kuna sababu yoyote ya msingi au kutatokea tukio ambalo litazuia uchaguzi kufanyika kwa tarehe ya awali, kwa sababu hiyo, Tume imefuta siku ya kupiga kura katika Jimbo la Muhambwe na upigaji kura huo utafanyika Mei 16 mwaka huu,” alisema Dk Mahera.

Alisema hata kampeni za ubunge katika jimbo hilo zimesitishwa hivyo zitaanza tena Mei Mosi hadi Mei 15, mwaka huu kama itakavyofanyika kwenye Jimbo la Buhigwe.

Kwa mujibu wake, hadi sasa tayari uteuzi wa wagombea umeshakamilika katika jimbo hilo, ambao wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT-Wazalendo na Democratic Party (DP) wamekidhi vigezo na kuteuliwa.

Aliwataja wagombea ubunge katika Jimbo la Muhambwe kuwa ni Dk Florence Samizi (CCM), Philipo Fumbo (DP) na Masaba Joseph (ACT-Wazalendo).

Kuhusu Jimbo la Buhigwe, Dk Mahera alisema NEC imeshapokea taarifa ya kimaandishi kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai akitaarifu kuwepo kwa nafasi wazi katika jimbo hilo.

Alisema tume pia ilipokea barua kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuhusu kuwapo kwa nafasi wazi za udiwani katika kata 18 Tanzania Bara.

Dk Mahera alisema uchukuaji fomu kwa wagombea wa ubunge katika Jimbo la Buhigwe na wagombea udiwani katika kata 18 utaanza Aprili 24 hadi 30 mwaka huu, uteuzi wa wagombea utafanyika Aprili 30, mwaka huu na kampeni zitaanza Mei Mosi hadi Mei 15 na uchaguzi kufanyika Mei 16, mwaka huu.

Alisema rufaa iliyokatwa na mgombea ubunge wa CCM, Dk Samizi katika Jimbo la Muhambwe dhidi ya wagombea wenzake akiwamo Fumbo (DP) na Masaba wa ACT-Wazalendo kwamba hawakukidhi vigezo, tume imekataa rufaa hiyo na kuagiza uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi ubaki kama ulivyo.

Chanzo: Habari Leo
 
ccm(siyo tume) waone aibu katika hili.

uchaguzi huwe wa haki,apatikane.

wangewaachia wananchi waamue.

najua hakuna namna ya ccm kwa haki kushinda hayo majimbo.

wakishinda act wapewe.
 
Back
Top Bottom