Mugumu, Mara: Watu 7 wauawa kikatili kwa kupigwa risasi ndani ya shimo

Askari wa wanyamapori akiwekwa binadamu na swala mbele yake halafu aambiwe shuti kimoja atamshuti binadamu bila kujiuliza.

Sijui wanapewa mafunzo ya aina gani huko vyuoni kwao.
 
Askari wa wanyamapori akiwekwa binadamu na swala mbele yake halafu aambiwe shuti kimoja atamshuti binadamu bila kujiuliza.

Sijui wanapewa mafunzo ya aina gani huko vyuoni kwao.
Wamejifunza kwamba akionekana binadamu kwenye hifadhi ya taifa wanaamini ni kiumbe kipya kimeingia eneo hilo hivyo lazima wapige kitu
 
Watu 7 wakazi wa maeneo ya Parki Mugumu wameuwawa kikatili kwa kumiminiwa risasi bila huruma na askari walinzi wa hifadhi ya Serengeti wakiwa kwenye mashimo ya dhahabu ya Kilima Fedha.

Tukio hilo ambalo limetokeea mwezi wa 9 mwishoni na kuja kugundulika mwezi wa 10 baada ya kufichwa lisivuje linaelezwa kuwa limetokea baada ya vijana 10 kwenda kuchimba dhahabu kwenye eneo la hifadhi ya Serengeti katika eneo linalomilikiwa na raia wa Marekani maarufu kama John Walker.

Shuhuda wa habari hizi anasimulia kuwa vijana hao 10 walienda kuokota na kuchimba dhahabu eneo lililo ndani ya hifadhi ya Serengeti huku 7 wakiwa ndani ya shimo na watatu wakiwa juu ndipo walipoona askari "game" wengi wakiwa na bunduki wakiwazingira.

Vijana wale watatu waliwashtua wenzio, na wao kufanikiwa kukimbia na kijificha milimani, lakini wale 7 waliokuwa shimoni walijitahidi kutoka ndani ya shimo bila mafanikio.

Askari wale baada ya kufika eneo la shimo waliwamiminia risasi bila huruma watu wale 7 waliokuwa ndani ya shimo na wote kupoteza maisha hapo hapo.

Miili ya marehemu iliachwa mule mule shimoni ikiwa na majeraha ya risasi mpaka ndugu wa marehemu walipofuatilia na kuikuta ikiwa imerundikwa kwa pamoja ndani ya shimo.

Kutokana na unyeti wa taarifa hizo , mamlaka husika zimejitahidi kuficha zisivuje na wahusika wa mauaji wakiwa hawajakamatwa wala kuchukuliwa hatua yoyote, huku mamlaka zikitumia nguvu kutaka ndugu wa marehemu kuzika ndugu zao ili kuficha ushahidi na kuzima habari hii.

Hii si mara ya kwanza kwa askari "game" kujichukulia sheria mkononi kwa kuwamiminia risasi watu wanaoingia hifadhi ya Serengeti, tofauti kabisa na sheria zinavyoagiza, ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwapeleka mahakamani.

Tunaomba kamanda wa polisi mkoa wa Mara, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Serengeti na mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika wote na kuacha kulifunika funika jambo hili maana tayari liko wazi na linafahamika mpaka kwa raia wa kawaida.

Source: Hidden(kwa sababu za Kiusalama)
Kipindi hayo yakitokea wanaCCM wanachekelea kwa hizo billion
 
Yaani wabongo wanawaua wenzao katika ardhi yao kisa tu kutetea mali za mtu mweusi,

Huu ni utumwa yes tena mbaya sana,

Hapo hao makamanda wa polisi walitajwa huenda wakawa wanajua tukio zima lilivyotokea na wamekaa kimya tu
Mkuu hao sio askari polisi. Ni askari wa maliasili.
 
Askari wa wanyamapori akiwekwa binadamu na swala mbele yake halafu aambiwe shuti kimoja atamshuti binadamu bila kujiuliza.

Sijui wanapewa mafunzo ya aina gani huko vyuoni kwao.
Kwao haki ya maisha ya mnyama iko mbele kuliko haki ya maisha ya binadamu!
 
Hivi MTU avamie pori na silaha, utamwacha? Ukimwacha anakuwahi wewe. Ni kweli tunapenda habari. ila pia tuna tatizo LA kupenda habari zinazoegemea upande mmoja.
Hivi mnakumbuka kuwa kuna rubani wa "hedikofta" aliuwawa akiwa humo porini wakifuatilia hao wavamizi.? Wavamizi hawaingii mikono mitupu. Ni suala LA kuwindana. Akikuwahi anakumaliza huku yeye ndiye mhalifu.

Tujijengee tabia ya kutafuta ukweli kwanza ili tuwe na mijadala huru badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa 100%
 
Hivi MTU avamie pori na silaha, utamwacha? Ukimwacha anakuwahi wewe. Ni kweli tunapenda habari. ila pia tuna tatizo LA kupenda habari zinazoegemea upande mmoja.
Hivi mnakumbuka kuwa kuna rubani wa "hedikofta" aliuwawa akiwa humo porini wakifuatilia hao wavamizi.? Wavamizi hawaingii mikono mitupu. Ni suala LA kuwindana. Akikuwahi anakumaliza huku yeye ndiye mhalifu.

Tujijengee tabia ya kutafuta ukweli kwanza ili tuwe na mijadala huru badala ya kumeza kila kinacholetwa kwa 100%
Bora umenena ukweli, kumbukumbu za wavamizi kuua walinzi zipo
 
Watanzania kweli mapopoma wote, halafu tunapayuka eti tuko huru na kutamba tulipata uhuru 1961 ili tujitawale STUPID IDIOTS! UHURU GANI? MAN INA SWINE!!!
 
give them (niggers) guns and they will kill each other - Botha the racist
 
Nilichogundua waanzisha threads hasa kuhusu habari za kitaifa/kijamii hupotosha eidha kwa makusudi kwasababu zao binafsi au hukurupuka kutoa habari pasipo kujua ukweli wake.

Wachangiaji nao wengi ni wafuata mkumbo tu, unakuta hawajui lolote kuhusu habari iliyoletwa wao wamejaa lawama zaidi pasipo kujua ukweli.
 
Kama kuna waandishi wa habari humu embu limulikeni hili kwa kasi kubwa watanzania na dunia nzima ijue
 
sasa hapa tumlaumu mzungu au serikali yetu? kwa maelezo ya mleta mada askari waliohusika ni wa hifadhi ya serengeti na hifadhi iko chini ya serikali. Kwa upande wangu serikali yetu haiwajali watu wake..

Ingekuwaje kama mgodi wa Nyamongo ungekuwa chini ya serikali na wale akina mura wakavamia kwa umoja wao? serikali hii isingepeleka vifaru kweli kwa ajili tu ya watu wake wenyewe kuvamia mali zao?

Hebu tubadilike, tunapowanyooshea wageni kwa ajili ya usalama wa watu wetu na sisi tuwe wa kwanza kuishi utaratibu huo

Sheria zipo kwa wahalifu kama hao na risasi si mmoja wa sheria hizo
 
Dah! This is too much now! Hawa watu weupe wanatumaliza mpaka ndani kwetu?
Mungu awalaze pema Marehemu wote...Pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.
Tunachukiana weusi Kwa weusi!hata kama amri walinzi hao walipewa toka juu lkn Siyo kufika hatua ya kuwaua bora wangewakamata.
Unajua nini mkuu biashara ya utumwa ilituathiri sana na Mpaka leo hii
Kikubwa hapo sheria ifate mkondo wake

Ova
 
Kwa hili mtetea wanyonge mheshimi raisi hawezi kuliacha hivi hivi raia saba kuuwawa kinyama.
 
Viongozi wa ulinzi na usalama wa raia Serengeti inabidi wawajibishwe kwa kukaa kimya
 
Back
Top Bottom