mugabe na historia!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mugabe na historia!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Iteitei Lya Kitee, Jun 25, 2008.

 1. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2008
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Gdmorning members,leo nina mkanganyiko ambao nauweka hapa ili tuendelee kushare ideas.
  Ni kuhusu viongozi wetu hawa wanaochukulia historia kama kivuli cha kuendelea kubaki madarakani,mfano ni Mugabe,Musevenianaesema
  (I went to the bush to fight for this country!!).Juzi nlikua nikitizama kipindi cha Jenerali On Monday na walikuepo wasomi wenzetu wawili waliokua wakichambua historia inayo mlinda Mugabe awepo madarakani.
  Je ni sawa kwa Mugabe kung'ang'ania kuendelea kuiongoza Zim hata kama wananchi wamesema hapana?Je hii sababu inayotolewa kuwa Tsvangirai ni kibaraka wa UK,Australia,US etc ni ya msingi?
  Wanazuoni naomba mitizamo yenu!!
  Natoa hoja!!
   
 2. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ukiacha historia nzuri ya ukombozi aliyonayo.Si sahihi yeye Mugabe kuamini nchi ni mali yake na kama si yeye uhuru usingepatikana.
  Hizo ni tabia za wale wote WABINAFSI.
  Hili lipo hata hapa kwetu TZ bara na visiwani.
  LAKINI VISIWANI NI ZAIDI.
  NAFIKIRI IFIKE MAHALA WATAWALA WAELEWE KUWA NCHI HII NI YETU SOTE.
  ALIYEONGOZA MAPINDUZI NA YULE ALIYEKUWA NYUMBANI NA FAMILIA YAKE MWAKA 1980 KWA KESI YA ZIMBAMBWE NA 1964 KWA KESI YA ZANZIBAR WOTE NI WADAU WA MUSTAKABALI WA MATAIFA YAO.
   
 3. bintimacho

  bintimacho Member

  #3
  Jun 25, 2008
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata kama ameisaidia zim ikapata uhuru, anatakiwa aachie wengine waongoze..ukiangalia na umri wake,hapo anaonekana kama ana ubinafsi tu.its been more than 30 years yeye yuko in power..jamani waafrika Mungu atusaidie.
   
 4. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Ni sawia kuiacha nchi kwa watu wenye nchi yao mioyoni na sio usoni kumbe rohoni ni vibaraka.
   
 5. M

  Materanus Member

  #5
  Jun 25, 2008
  Joined: Jan 18, 2008
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sikufanikiwa kuona upuuzi wa hao wasomi wenzio ambao walichangia mjadala kwenye kipindi cha jenerali on monday. Lakini akina mugabe na mwenzie Museveni nina wafuatilia vizuri. Wanacho kifanya ni upuuzi mtupu.
  Kimsingi nchi ni ya watu, siyo ya mtu, ukisaidia kuleta uhuru haimaanishi kuwa nchi ni yako. Especially ubongo wako ukianza kuchoka kwa uzee na umaarufu ukianza kupotea. Tatizo nilionalo mimi ni kwamba viongozi wa kiafrika tena hasa nchi jirani zinambeba sana huyo babu yao. Akina Kikwete, Mbeki na Gaddafi, nk. Mi nafikiri nchi zitoazo misaada hazina makosa kushinikiza kuondoka kwa babu, kwani misaada yao inako enda haieleweki. sidhani kama kuna agenda ya siri, na hata kama ipo poa, lakini wao wana raise tatizo linalo onekana na ulimwengu unaona. Its time for african leaders to let democracy take charge.
   
Loading...