Mugabe atangaza njaa kuwa janga Zimbabwe

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ametangaza baa la njaa linalokabili taifa hilo la kusini mwa Afrika kuwa janga la kitaifa.

Taifa hilo halijapokea mvua ya kutosha tangu mwaka jana na watu 1.5 milioni wanahitaji msaada wa chakula, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Maelfu ya mifugo wamefariki kutokana na ukame.

Tangazo hilo la Rais Mugabe limejiri siku chache tu baada ya Muungano wa Ulaya (EU) kumhimiza atangaze baa hilo kuwa janga la kitaifa ili mashirika ya kimataifa ya misaada yaweze kuchangisha pesa haraka za kusaidia raia wa Zimbabwe.

Serikali imewataka raia kutoingiwa na wasiwasi ikisema kuna mkataba wa kununua tani nyingi za mahindi kutoka Zambia.

Sekta ya kilimo ndiyo iliyoathirika sana huku wakulima wa tumbaku na pamba wakikosa mavuno.

Oktoba mwaka jana, Umoja wa Mataifa ulitoa ombi la dharura la $86 milioni la kutoa chakula cha msaada kwa Zimbabwe.

Taifa hilo limekuwa likipokea misaada ya chakula tangu sekta yake ya kilimo iliposambaratika mwaka 2001.

Hii ni baada ya Rais Mugabe kuagiza mashamba makubwa yaliyomilikiwa na Wazungu yatwaliwe.

Wakati mmoja, watu 7 milioni walihitaji msaada wa chakula kwa dharura.


Chanzo:
BBC
 
Tuone kama atakataa wazungu wasimpe dona nitajua jamaa kweli ni mbabe.
 
Mugabe anakula matabishi yake.... Kama wazungu walizalisha na kutokomeza njaa kulikuwa na umuhimu gani kuwaondoa???? Huu ndio unaitwa ujuha.
 
Mkuu #Super Handsome..jibu hoja kwa hoja...me namuona mzigo coz anapambana na wazungu kwenye majukwaa ya AU wakati wananchi wake wapo kwenye lindo la umaskini na njaa ya kutupwa! Sasa uniambie kwa nini Mugabe si Mzigo
 
I wonder why they call him a lion of Africa while his country sinking further down in the abyss of poverty.The biggest mistake to ever be committed by Mugabe is confiscating farms from whites and offer them to the black farmers who had neither capital nor knowledge on how to run the modern agriculture. So he destroyed Zimbabwe economy that relied solely on agriculture because of his dysfunctional economic policies.
 
Have ever been to Zimbabwe? I think you should shut yo ass up!
Acha matusi wewe! jibu hoja kwa nini asiwe mzigo limtu lina miaka zaidi ya 80 bado linang'ang'ania madaraka,inamaana Zimbabwe hakuna watu wengine wwnye uwezo wa kuwa Rais!?
Kama wazungu wabaya kama anavyoimba kila siku why leo anawalilia wamsaidie kuwapa wananchi wake chakula!?
 
Katika maeneo mengi ya vijiji vilivyokumbwa na ukame mbaya, ambapo asilimia 26 ya raia wa nchi hiyo wanakabiliwa na uhaba wa chakula. Hali ya ukame iliyoyakumba maeneo kadhaa ya Afrika iliozidishwa makali na mvua za El Nino, imeziathiri Afrika Kusini na Zambia na pia Zimbabwe, hivyo kusababisha vifo vya maelfu ya mifugo, kukauka kwa mabwawa na mimea. Zimbabwe ambayo ilikuwa ikitegemewa sana kwa chakula barani Afrika, imekumbwa na uhaba mkubwa wa chakula katika miaka ya karibuni na kugeukia manunuzi ya nafaka kutoka nchi jirani ili kukidhi mahitaji yake ya chakula.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom