Mugabe Amsimamisha Mwanasheria Mkuu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mugabe Amsimamisha Mwanasheria Mkuu!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Steve Dii, Dec 16, 2007.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Source link: NewZimbabwe.com


  SteveD.
   
 2. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hii mbinu kajifunza kwa mwenzie Gen (rtd) Pervez Musharraf wa Pakistan. Kumbuka wote wana bifu na wazungu na wamesimamishwa uanachama wa Commonwealth, ambao Jongwe anadai si kitu, "..what is it anyway? A club! There are so many other clubs we can join!" Ndivyo alivyotamka siku alipoambiwa Zimbabwe imesimamishwa uanachama wa Commonwealth. Majuzi Musharraf nae katimua majaji wote ambao wanaonekana dhahiri kimsimamo kutounga mkono masuala yake, na kuteua wapya kabla ya uchaguzi, anasubiri watu wapeleke kesi ya kima kwa tumbili waone hukumu itakavokuwa ya "haki"!
   
 3. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2007
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kithuku,
  AG hayupo chini ya mhimili wa mahakama,ni presidential appointee na anawajibika kwa waziri wa sheria. Binafsi sidhani kama kuna siasa iliyofanyika kumsimamisha na kumchunguza kwa mujibu wa nchi yoyote ile inayofuata utawala wa sheria. Inakupasa uelewe kwanza, hakufukuzwa kazi bali amesimamishwa na uchunguzi unafanyika kuchunguza tuhuma. Kwa serikali inayofahamu wajibu wake hivi ndivyo inavyopaswa kuendeshwa...hivi si ulisikia Vithrani, Depark na Chavda wanaingia na kutoka Bongo? nani anawakingia kifua? kwa serikali inayohamu wajibu wake kuanzia AG wa enzi hizo Chenge, Waziri wa sheria na ghasia zote walishapaswa kusimamishwa na kuchunguzwa. Lakini kwa kuwa serikali yetu haijui wajibu wala majukumu yake ndio maana tunawaona mafisadi wanazidi kutanua. Time imefika ya kumuomba mzee Mugabe ushauri badala ya kumfananisha na Musharaf bila ya sababu ya msingi.
   
Loading...