Mugabe alifariki dunia kutokana na kuugua ugonjwa wa saratani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Harare, Zimbabwe.
Wakati mwili wa Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe ukisubiri mwezi mmoja kuzikwa rasmi imfahamika kuwa kiongozi huyo alifariki dunia kutokana na kuugua ugonjwa wa saratani.
Serikali ya nchi hiyo imefichua siri hiyo leo Septemba 23 mjini Harare na kusema kuwa kiongozi huyo alikuwa akipatiwa matibabu ya mionzi nchini Singapore.
Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa alisema kwamba matibabu ya chemotherapy (tiba kwa njia ya mionzi) anayokuwa akipatiwa ili kupunguza sumu mwilini yalisitishwa wakati ilipodhihirika kwamba hayamsaidii tena.
Mugabe alifariki dunia nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95 alipokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake kurejeshwa nchi kwa ajili ya mazishi ambayo yamepangwa kufanyika baada ya mwezi mmoja.
Kiongozi huyo anatarajiwa kuzikwa katika eneo la kitaifa linalotumika kuzika mashujaa wan chi hiyo ambalo linajengwa mjini Harare sehemu ambayo wapiganiaji uhuru wengi nchini humo na watu maarufu wamezikwa.

Kwa sasa mwili wa Mugabe umerejeshwa nyumbani kwake mjini Harare siku moja baada ya kufanyiwa sherehe za kimila.
Mwili wa Mugabe uliwasili nyumbani kwake mwishoni mwa wiki ukitokea Kutama umbali wa kilometa 90 kuelekea Magharibi wa nchi hiyo ambako ndipo alipozaliwa. Jumatatu iliyopita wanakijiji walitoa heshima za mwisho na kufuatiwa na shughuli ya kimila iliyoendeshwa na viongozi wa ukoo na kimila wakiwamo machifu.
Mwili wa Mugabe ulilala kijijini hapo Jumanne iliyopita kisha kurejeshwa nyumbani kwake siku inayofuata mjini Harare kwa ajili ya kihifadhiwa.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya mazishi ya kitaifa yaliyofanyika Jumamosi na kuhudhuriwa na maelfu ya watu wakiwamo viongozi kadhaa wa Afrika.
Awali akizunguza na Shirika la habari la AFP, mjukuu wa kiongozi huyo, Leo Mugabe alisema ingawa tarehe rasmi ya mazishi haijapangwa lakini familia imekubaliana kumzika baada ya mwezi mmoja.
Mjukuu huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha mwezi mmoja mwili wa kiongozi huyo utahifadhiwa nyumbani mjini Harare.
Mjukuu huyo alisema mwili huo utazikwa mwezi ujao katika makaburi ya kitaifa ya mashujaa, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kaburi lake.

Credit : Mwananchi
 
only in Africa
Kuna yule wa Congo alikaa mochari za Belgium kwa miaka 2 akisubiri mwanaye awe prezida ndo azikwe. Kaburi tu na sanamu lake vikala zaidi ya 6b za madafu. Vipaumbele vyetu vinachekesha sana aisee


wanawake wanafia leba
under 5 mortality iko juu
ebola inawakula
usalama ni tete
maji safi na salama ni msamiati
hospitali hazina dawa
barabara hazipitiki
 
tapatalk_1564209595386.jpeg
 
Back
Top Bottom