#COVID19 Mufti Zuberi: Ibada ya Hijja imefutwa kwa sababu ya Virusi vya Corona

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali ya Saudi Arabia imefuta ibada ya hija kwa mwaka 2021 kutokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Hii ni mara ya pili kwa waumini wa dini ya Kiislamu kutotekeleza ibada hiyo kutokana na gonjwa huo ulioanza kutikisa mwishoni mwa mwaka 2019.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatano Juni 16, 2021, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi amesema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kaimu Balozi wa Saudi Arabia, Abdul Aziz Hamad, hija itatekelezwa kwa raia wa Saudi Arabia pekee na si wananchi kutoka mataifa mengine duniani.

"Kutokana na taarifa niliyopata hakutakuwa na hija mwaka huu, isipokuwa itatekelezwa na wenyeji Saudi Arabia ambao ni wakazi wa palepale kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.”

"Serikali ya Saudi Arabia wameona waifute kwa maana ya raia kutoka nchi nyingine kutoingia Saudi Arabia na watakaoshiriki ni wenyeji peke yao kwa idadi ndogo isiyozidi mahujaji 60,000," amesema.

Huku akiwataka Watanzania kujiandaa kwa hija mwaka 2022 amesema, “mwenyezi Mungu atupe subira juu ya jambo hili, huu ni mwaka wa pili kutokwenda hija, hii inatokana na ucha Mungu katika ibada.”

Chanzo: Mwananchi
 
Shetwani kashinda.?
Kwani Yale maombi ya upako ambayo waislamu walifanya hpa Tz na kuimaliza Corona hayakuweza kufika Saudia? Au kwa nini Mh. Mufti Mkuu hakuwapa upako waislamu wenzake Wa Saudia ili nao wafanye maombi kama Yale na kuitokomeza ili Mahujaji wasizuiwe kwenda kufanya ibada? Au waislamu Wa Saudia imani yao ni haba kuliko waislamu Wa kwetu?
 
Waende tena wakaanze mahubiri yao uchwara ya kuwafanya watanzania wote wawe waislamu hadi kupelekea mapdri kuanza kuchinjwa na magaidi ya kibiti
 
Kwani Yale maombi ya upako ambayo waislamu walifanya hpa Tz na kuimaliza Corona hayakuweza kufika Saudia? Au kwa nini Mh. Mufti Mkuu hakuwapa upako waislamu wenzake Wa Saudia ili nao wafanye maombi kama Yale na kuitokomeza ili Mahujaji wasizuiwe kwenda kufanya ibada? Au waislamu Wa Saudia imani yao ni haba kuliko waislamu Wa kwetu?
Huyu mzee ni tapeli sn
 
Saudia pamoja na hijja walikuwa wanatengeneza hela ndefu sana ila uchumi ni mgumu duniani kwa sasa

Hata wao hawana la kufanya zaidi ya kusubiri haya yapite
 
Mufti arejee vyema kauli yake”Ibada ya hijja haijafutwa isipokuwa wataKaO idiriki ibada hii tukufu ya Hijjah ni wale waliopo nchin saudi arabia pekee sio kusema ibada ya hijja imefutwa hapa amefanya makosa angewafafanulia watu ili waelewe vyema
 
Back
Top Bottom