GAS STATE
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 1,770
- 952
uko sahihi sheikh BAKWATA ni dumavu tangu ilipoasisiwa miaka ya uhuru, ila unapoilaumu na kuishangaa inabidi ujuwe yafuatayo:Bakwata ni taasisi iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchini tanzania inakatiba yake na miongozo yake juu ya uendeshaji dini ya uislam.nchi yetu inaruhusu uhuru wa kuabudu kwa kila raia wake ilimladi hauvunji sheria za nchi.
BAKWATA siyo UISLAM bakwata ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine za ALHIKMA,ANSARI SUNNA.SALAFY.ISLAMIC F.hizi taasisi zote zina waislam wanaowaongoza kwa taratibu wanazozifaham wao kwa elimu waliyokuwa nayo.Bakwata wanapoendesha shughur zao waendeshe wanavyotaka wao tumewaacha na misikiti yao na madrasa zao
inaumiza sana kuona chombo kilichokuwa cha mwanzo hapa tanzania kusajiliwa leo hakina maendeleo yoyote zaidi ya kutumika kuudumaza uislam kilal kukicha.hatufurahi kuona waislam tumeshindwa kuwa na hospitar zetu zinazoendeshwa kwa taratibu za dini.tumeshindwa kuwalipa mishahara walimu wa madrasa zetu.tumekalia kuangalia suruali fupi na ndefu,mfuga ndevu na asiyefuga ndevu,kaswali leo iddi ataswali kesho idi.Bakwata fanyeni yenu nasisi tunafanya yetu hatupaswi kukaa majukwaani na kulishiana vitisho
i)ndio msimamizi mkuu wa masuala ya Uislam nchini haijalishi dhehebu gani
ii)kusema ni sawa na taasisi zingine itakuwa umekosea na kuidhalilisha kwa kiwango hali ya juu, kumbuka serikali haisajili taasisi yoyote ya Kiislam bila katiba yake kupitiwa na BAKWATA.
III)iltaka kujenga taasisi za elimu na afya lakini ilizuiwa na serikali ya rais yule ambaye alitaka kila kitu cha umma na sio binafsi
iv)kuilaumu leo kwa makosa ya nyuma itakuwa huisaidii bali ni kuikandamiza tu kama una ushauri peleka.