Ingekuwa dua inafanya kazi hivyo, mbona uarabuni kusingekuwa na jangwa

Tumechoka na vimbwanga saizi tunataka wakiomba hiyo dua watutajie na tarehe na mwezi kabisa ambao Mungu wao kawaahidi mvua ataishusha ili ikitokea haijanyesha tujue ni uwongo

Hizi habari za kusema tunafanya dua mvua inyeshe na unaelewa kabisa kua tuko ukingoni mwa kiangazi tumekikaribia kifuku na ni wazi kabisa kua kifuku ni season ya mvua, kutuambia mvua imenyesha kwasababu ya dua yako huko ni kututapeli kizungu
 
Inaonekana mufti alipitia hapa kwanza, akacheki huu utabiri wa siku kumi mbele afu akaitisha maombi

1637174378814.png
 
Kiongozi mkuu wa waislamu Mufti Sheikh Zuberi aitisha maombi ya siku tatu kwa waislamu wote kuombea mvua yenye heri kuanzia kesho Alhamisi

Maaskofu wakristo naona wanashindana tu kuvaa barakoa hawaitishi maombi kulikoni?
Hahahaha yule mshamba aliidharau barakoa ikamla kichwa angekua anatufokea tu saa hii.
 
Samia mwenyewe hataki hayo maombi,tangia apate madaraka sijawai kusikia anatamka neno Mungu au mtume mwamadi, Yeye anaamini mzungu kutatua matatizo yetu,na kupata msaada,hata salamu anasema kazi iendelee,tutapigwa sana ukame maana hata Rais wetu aamini uwepo wa Mungu
Wewe ukiamini nadhani inatosha.
 
Zaburi :14:1
Wapumbavu hujisemea moyoni: “Hakuna Mungu.” Wote wamepotoka kabisa, wametenda mambo ya kuchukiza; hakuna hata mmoja atendaye jema!
Ni kweli hata mimi nakubaliana na wewe huyo mtu lazima awe mpumbavu kwasababu katumia organ (moyo) isiyo sahihi

Kwasababu kwenye swala la Miungu/Mungu, moyo sio kiungo sahihi kukitumia katika kufanya maamuzi, moyo mara nyingi huambatana na viashiria vya mihemko (emotions)

Mpumbavu ataamua kupitia moyoni na kusema hakuna Mungu, ila mtu mwenye akili timamu ataamua kusema Mungu hayupo kupitia ubongo wake
 

Hili nililisema ktk uzi fulan, kuwa haya mambo ya mabadiriko ya hali ya hewa inabidi lifanyike jambo la utatuzi ambalo litahusisha solutions za kiroho na kisayansi il tujiepushe na madhara ya ukame, cha ajabu kuna wapuuzi walinipinga sana kwa kusema maombi ama dua hazina nafasi ktk masuala ya kijiografia

Kama mashehe wenye akil timamu wameweza kuthubutu kufanya maombi ujuwe kuwa wanajua kuna effects za kuleta matokeo chanya, elimu za kigeni & utandawazi usitusahaulishe kuwa sisi ni watu wa kiroho, changamoto kama hizi tulikuwa na uwezo wakuzitatuwa kiimani zaidi

Screenshot_20211117-215104.jpg
 
Samia mwenyewe hataki hayo maombi,tangia apate madaraka sijawai kusikia anatamka neno Mungu au mtume mwamadi, Yeye anaamini mzungu kutatua matatizo yetu,na kupata msaada,hata salamu anasema kazi iendelee,tutapigwa sana ukame maana hata Rais wetu aamini uwepo wa Mungu
Kwani siku anakula kiapo alikuwa kashika kitabu gani?Kuamini kuwa Mungu yupo inahitaji awe kila siku anasema tumtangulize Mungu mbele ndio utafaurahi sio?

Kuna siku umekutana na Samia akakusamilia hivyo?Kazi iendelee ni salamu ya watu wapi hapa Tanzania?Lakini nyie alipokutaka uchangie kidogo kwenye muamala nyie si ndio mlikuwa mstari wa mbele kusema mnaumizwa? sasa kama ndivyo kwanini asiende kupata usaidizi kwenye mataifa ya watu
 
Kiongozi mkuu wa waislamu Mufti Sheikh Zuberi aitisha maombi ya siku tatu kwa waislamu wote kuombea mvua yenye heri kuanzia kesho Alhamisi

Maaskofu wakristo naona wanashindana tu kuvaa barakoa hawaitishi maombi kulikoni?
Waache unafiki tawi la CCM kama wana nguvu waombe mvua dodoma kipindi cha kiangazi. Kama kwao mtume jangwani aliishi watashindwa vipi kuishi bila mvua wafuasi.

Wametegeshea tarehe za mwishoni za mvua kuanza ndio wanajifanya maombi ya mvua ili zikianza kunyesha waseme maombi yamefanya kazi..hizi janja janja tu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom