Mufti Mkuu, umenena tumlipe Rais basi tukishindwa tumuombee heri

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,441
Nafuatilia kauli ya Mufti Mkuu wa BAKWATA Tamzania Sheikh Abubakari Zuberi akimshukuru Rais kwenye ufunguzi wa Msikiti Dodoma kuwa Rais amejenga Msikiti katika maeneo mbalimbali Chato, Kinondoni, Chamwino, Sumbawanga nk na kurejesha mali za Waislamu zilizopotea.

Mimi niseme wazi Rais Magufuli amejitahidi sana kugusa kila nyanja bila ubaguzi wewe kidini, kikanda na kikabila

Shukrani zetu ni kumpa kura na kisha tuendelee kumuombea.
 
Muft wetu pamoja na Rais wetu Mungu awabariki na awape maisha marefu.
"Aaaamin"
 
Back
Top Bottom