Mufti mfikishie salamu zetu Mh rais atapofika kama mgeni rasmi katika hilo baraza la Eid...!

Status
Not open for further replies.

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,376
12,822
Nianze kwa Salaam na kuwatakia heri ya Eid kwa ndug zangu waislam na wale wasio waislam tunashukuru kwa upendo mliotuonesha kipind chote hiki cha mfungo wa ramadhan ikiwemo na kujali kwenu na kutokutujengea mazingira magumu ya ugumu katika kutekeleza ibada hii...sisi sote ni viumbe wa mungu na ipo siku sote kwake tutarejea...na sisi sote pia ni watanzania wazaliwa wa ardhi hii iliyo tulivu kabisa...

Lengo langu ni kuwafikia ndug zangu kupitia hapa JF na kutumia kama forum ya kupenyeza ujumbe wangu ukufikie Mufti ya kwamba kwa kuwa Mh Rais Magufuli atakuwa ni mgeni rasmi katika baraza hilo basi tafadhali mfikishie ujumbe huuu...

Mufti...Tafadhali mwambie Mh Rais kuwa kipindi anasimama kuomba kura alisimama kuomba kura kwa umma wa watanzania wote pasi na kuangalia iman zao...kanda wanazotokea...makabila yao...rangi zao...jinsia zao na kadhalika...kwa ufupi hakuomba kura kwa kubagua kitu cha aina yoyote ile...

Tanzania kama nchi ni nchi yenye mchanganyiko wa makabila mbali mbali...na tunashukuru mungu suala la ukabila au kubaguana kwa ukabila ndan ya nchi hii mungu ametulinda na hata waasisi wa taifa hili walifanikiwa kulidhibiti suala hili...tunashukuru kwa kias kikubwa suala la kubaguana au kutazamana kwa ukabila ndan ya nchi hii kwa kias kikubwa halipo..

Vivo hivyo hata suala la udini ndan ya nchi hii kuna dini mbali mbali ingawa dini kuu mbili ndan ya nchi hii na zenye wafuas wengi ni ukristo na uislam...mungu mkubwa pamoja na changamoto nyingi zinazookumba dini ya kiislam dunian lakin atleast Tanzania nchi yetu kuna maingiliano na kuishi kwa kuvumiliana baina ya watu wa iman hizi zilizopo ndan ya nchi hii...na pale zinapotokea changamoto haraka sana busara hutumika na kutufanya kukosoana kwa wema na utu na kurudi katika hali yetu ya kuish kwa kuvumiliana...

Pamoja na yote hayo bado hapakosekani nyufa na manung'uniko kutoka pande mbali mbali...

Mufti naomba umueleze kinagaubaga tena pasi na kumficha kwamba katika kuongoza serikali hii ambayo ni ukweli ulio waz kwamba amechaguliwa na watu wa iman mbali mbali wakiwemo wakristo,waislam na hata wasio na dini aache ubaguz na upendeleo...

Ajitahid atleast kubalance na kutengeneza serikali iliyo na taswira ya kitaifa kwan nchi hii ni mchanganyiko wa watu wa sampuli mbali mbali kama nilivyoeleza hapo juu...

Sisi waislam tumekwazika na tunazid kukwazika sana na upendeleo wa waz waz kabisa ambao Mh Rais ameuonesha katika teuzi zake kuanzia kwa baraza la mawaziri...makatibu na manaibu katibu wakuuu...wakuu wa mikoa...wakuu wa wilaya na hata kwa makatibu tawala...

Tumeona upendeleo waz waz kabisa katika teuzi za Mh Rais huku idad ya waislam ikiwa si zaid ya 20% ya wawakilishi wote ambao hawa wanaenda kufanya decisions zinazohusu taifa hili...

Jambo hili either linafanyika kwa makusudi kabisa au kwa kutojua basi ifahamike kuwa ni jambo linalopandikiza hisia hasi kabisa na linaloweka doa kubwa katika uongozi wake na mustakabali wa baadae wa taifa letu...

Hakuna justification ya aina yoyote inayoweza kuhalalisha upendeleo huo na ubaguz huo wa waz waz unaofanywa na mh rais...

Umueleze kwamba sisi hatutak kupendelewa wala hatutak wengine wapendelewe..tunachomsihi ni kwamba akumbuke ahad zake wakati wa kampeni na akumbuke pia waislam walimpigia kura yeye pasi na kuangalia iman yake...iweje yeye leo awabague kwa kigezo cha iman yao?..

Umueleze kwamba waislam wanakiona kinachofanyika na kukaa kimya si kwamba wameridhika na utaratibu huo unaondelea...

Umueleze kuwa kwa kuwa kuna namna nyingi ya kumfikishia ujumbe basi atambue kuwa nchi hii kwa sasa haina tena siri wala kificho katika uendeshaji wake..na si kwa yeye tuh hata kwa Rais yeyote atakaekuja hawez kuliweka kando suala la balance of power baina ya watu wa aina mbali mbali ndan ya taifa hili...

Mfano katika makatibu tawala 130 walioteuliwa hizi punde waislam hawazid 18..!je hiyo ni haki?siend huko kwa mawaziri...makatibu na manaibu katibu wakuu...wakuu wa mikoa na wilaya huko ndiko hakufai kabisa...

Kipi ambacho waislam wamemkosea Mh Rais had afikie hatua ya kuwakandamiza na kutowashirikisha kwenye serikali hii?...

Yapo mengi ya kuongea ila kikubwa ni kumfikishia ujumbe huu ya kwamba kinachofanyika kinaonekana na hakivumiliki...

Eid Mubarak..!
 
Assalaam alaykum ustadhi. Pole sana Mkuu. Endelea kufanya ibada kwani ndio amali pekee utaingia nayo kaburini na kesho akhera. Haya ya duniani yakija uyapokee ila ukiyakosa usihuzunike sana
Du maneno mazito sana Ila tambua madhambi duniani adhabu mbinguni pia wema duniani thawabu mbinguni Nakutakia id njema pia nakukaribisha kesho nitakuwa nyumbani Lindi
 
Du maneno mazito sana Ila tambua madhambi duniani adhabu mbinguni pia wema duniani thawabu mbinguni Nakutakia id njema pia nakukaribisha kesho nitakuwa nyumbani Lindi
Ahsante sana ndugu. Tupo pamoja sana. Msalimie sana Ukana Shilungo
 
Nchi hii kuna vingi vya kubalance hadi mwisho wa siku unawezakujikuta viongozi wanakuwa kama kamati ya harusi.
1: Balance Uislam vs Ukristo
2: Huko kwa waislam wengine wataleta usunni na Ushia. Inabidi ubalance pia, usiahau ubakwata etc
3:Huko kwa wakristo ubalance RC, walokole, wasabato,waanglikana,
3:Balance mikoa.
4:balance kanda
5:balance rangi
6:balance makabila
7: balance jinsia "wanawake 50%"
8:Hapo hujabalance makada na washkaji wa karibu unaowakubali
9:Balance wasomi, napo ukiweka wengi wa udsm.udom,mzumbe,SUA watalia
10:Balance na Mashabiki wa Simba na Yanga. Unaweza kusikia serikali yote ni Simba.
11:hUJABALANCE UZANZIBARI NA UZANZIBARA PIA UNATAKA EQUAL SHARE KATI YA SISIMIZI NA TEMBO. HAPA TU HATA AKIPeWA NCHI OBAMA LAZIMA AKIMBIE

Katika yote hayo hpo tumesahau kubalance na wapagani, walemavu wa aina zote, walitokea jamii za wakulima vs wafugaji, etc kuna sababu nyingi sana kwa nini sisi ni masikini.
Hapa ukiendekeza saana bila umakini hii tabia utaishia kufurahisha watu nchi inadumaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom