Mufti Issa Shaaban Bin Simba Kuzikwa Leo.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
WAKATI mwili wa Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba (78) aliyefariki dunia jana asubuhi ukitarajiwa kuzikwa leo jioni mkoani Shinyanga, Rais Jakaya Kikwete ameungana na Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kuomboleza kifo cha kiongozi huyo wa juu wa kiroho nchini.



Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya familia, Mufti aliyefikwa na mauti akiwa katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu, atazikwa leo kutokana na wosia aliokuwa ameuacha kuwa, akiaga dunia mwili wake usiachwe muda mrefu bila kuzikwa.



Hata hivyo, taarifa kutoka Bakwata zinasema kwa upande wao wanatarajiwa kuuhifadhi mwili wa Mufti kesho au keshokutwa, kwani alikuwa mtu wa watu hivyo kuna umuhimu wa kutoa fursa kwa wengi kutoa salamu zao za mwisho kwa mpendwa wao.


Mmoja wa watoto wa marehemu, Selemani Simba alisema mwili utasafirishwa kwa ndege leo saa 3:00asubuhi kuelekea mkoani Shinyanga,ambako atazikwa katika eneo la Majengo.¡°Hali yake ilibadilika siku ya Ijumaa ambapo tulimkimbiza Hospitali ya TMJ ambako baada ya kufanyiwa vipimo ikabainika mapafu yalikuwa yamejaa maji hivyo ilitakiwa afanyiwe upasuaji,¡± alisema.



Alisema baada ya kufanyiwa upasuaji huo juzi, madaktari waliagiza mgonjwa apewe muda wa kupumzika na asisumbuliwe, hivyo hakuweza kuzungumza na mtu yeyote hadi umauti ulipomfika jana saa 3:45 asubuhi.





Rais Kikwete Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete alisema; ¡°Kifo kinaleta huzuni, hata hivyo kifo hakizuiliki, hatuna budi kukikubali nani wajibu wetu kumuombea Shehe Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele¡±.





Rais Kikwete ametuma salamu hizo za rambirambi kupitia kwa Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum.¡°Nawaombea subra wana familia, ndugu, jamaa, Waislamu wote na wana jamii kwani Mufti alikuwa kiongozi katika jamii yetu,¡± Rais alisema na kueleza kuwa, ¡°Kamwe mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa ujumla na hakika sote tutamkumbuka.¡±Mufti Simba alijiunga na BAKWATA mwaka 1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na mwaka 1970 alikuwa Shehe wa Mkoa wa Shinyanga.





Rais alimwelezea Mufti kama mwalimu katika jamii ambaye alikuwa na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda dini yake na kuitumia kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka.¡°Amekuwa mwalimu imara na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika Uislamu na jamii kwa ujumla, hakika tutamkumbuka siku zote.¡±Shehe Issa Bin Shaaban Simba alikuwa na uzoefu mkubwa ndani ya Bakwata na aliwahi kukaimu nafasi ya Mufti kwa siku 90, baada ya kifo cha Mufti Hemed mwaka 2002.



Baada ya hapo akasimamia mchakato wa uchaguzi wa Mufti Mkuu na baadaye 2003 akachaguliwakuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.



Dk Mukangara aomboleza Kama ilivyokuwa kwa Rais Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara nayeametuma salamu za rambirambi Bakwata na kwa Waislamu wote nchini kutokana na kifo hicho.Kwa mujibu wa taarifa yake jana, ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado taifa lilikuwa likimhitaji, hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.Alisema Mufti atakumbukwa kwa upole, unyenyekevu na kutopenda makuu wakati wa uhai wake ambapoalikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.


Chanzo : Habari Leo
 
Back
Top Bottom