Mufti ataka Mwaka Mpya wa Kiislamu iwe siku ya mapumziko


kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
22
Points
135
Age
42

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 22 135
Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba, amesema wameiandikia serikali barua kuomba siku ya Mwaka Mpya wa Kiislamu kuwamo katika orodha ya sikukuu zinazotambuliwa kuwa ni siku rasmi za mapumziko ya kitaifa nchini.
Alisema hayo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa wanahabari aliouitisha makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) jana kwa lengo la kutoa salaamu za mwaka mpya wa Kiislamu wa 1432, maarufu kama Alhjriyyah (A.H.).
Mufti Simba alisema wamefikia hatua hiyo ili kurekebisha makosa yaliyofanywa na viongozi wa Kiislamu waliopita kuhusu Sikukuu za Kiislamu, ambazo zinapaswa kuwa siku rasmi za mapumziko kitaifa.
Alisema viongozi hao walipotakiwa na serikali kuorodhesha sikukuu hizo, walitaja kuwa ni tatu; ambazo ni Iddi-El-Fitr, Idd-El-Hajj na Maulid na kuacha kuorodhesha Mwaka Mpya wa Kiislamu.
“Hivyo, kwa kuliona hilo, tumeiandikia barua serikali kuomba Mwaka Mpya wa Kiislamu uwe pia siku ya mapumziko. Tunasubiri majibu kutoka serikalini,” alisema.
Mufti Simba mbali ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwafikisha katika mwaka huo aliwataka Waislamu kuelekeza fikra zao katika mwaka uliopita kwa kutaza waliyofanya katika kujenga maendeleo yao, kiimani katika familia na jamii yao kama Waislamu.
Alisema wanaposherehekea kumalizika kwa mwaka 1431 na kuingia mwaka 1432, wanapaswa kuzingatia maana ya neno “Hijria”, ambayo alisema inamaanisha ‘kuhama’ Mtume Muhammad (S.A.W.) kutoka Makka kwenda Madina kama alivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuinusuru dini.
Aliwataka Waislamu kutoipoteza maana hiyo katika fikra na nyoyo zao, badala yake wawajibike kufanya ‘Hijra’ kwa maana kuyahama maovu na kuelekea kwenye mema.
Alisema katika kujenga ufanisi katika maisha ya Waislamu, Mwenyezi Mungu amewaamrisha kujenga umoja na mshikamano, kujitolea mali zao na nafsi zao katika njia ya Mungu, pia kujielimisha na kuukimbia ujinga, kuamrisha mema na kukataza mabaya.
Alimuomba Mwenyezi Mungu awape mafanikio Waislamu na wananchi wa Tanzania kwa jumla na kumbariki Rais Jakaya Kikwete pamoja na Baraza lake la Mawaziri walifanyie Hijra taifa lihame kutoka Watanzania walipo na kuelekea kwenye mafanikio zaidi.
 

Nzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
13,643
Likes
5,607
Points
280

Nzi

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2010
13,643 5,607 280
This thread has the same message as a thread posted earlier today talking on mahakama ya kadhi. Mods what r u doing?
 

Leornado

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
1,534
Likes
20
Points
0

Leornado

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
1,534 20 0
Jamani bado kidogo na mabuddha nao watadai mwaka wao kulingana na kalenda yao. Manake nao ni din kubwa yenye heshima. Tufike mahali tuache kuyumbishwa na dini. Serikali haina dini hata kama the top cream wote waislam.
 

Cynic

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2009
Messages
5,154
Likes
641
Points
280

Cynic

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2009
5,154 641 280
Tatizo kubwa ni kwamba Mamufti wengi hawajaenda shule ya kutosha na hawana exposure. Kwa shule sana sana madrassa + Form V, na kwa exposure sana sana ni safari za Macca na Mombasa
 

Forum statistics

Threads 1,204,496
Members 457,348
Posts 28,160,883