Mufindi: Mmiliki QWIHAYA General Enterprises atakiwa kuhamisha kiwanda ili kupisha gereji na nyama choma

Kabla ya kulaumu madiwani, ni vyema tukajua hiyo kampuni ilipata vipi hiko kiwanja au ilikipata kwa kutumia njia zipi halali. Kuna uwekano kabisa hiko kiwanja kilishakuwa katika ramani ya mpango mji. Na hilo wanalolisimamia ndio utekelezaji wake.

Inawezekana pia hiyo kampuni ilipata au ilivamia hilo eneo kwa kupitia mgongo wa nyuma au kwa kuhonga watu wachache katika Halmashauri iliyopita.
 
Yakipatikana na maelezo ya upande wa pili itakuwa rahisi kutoa hitimisho.

Inaonesha kuna kitu kikubwa tu hapo tena cha muda mrefu na kimepitia hatua kadhaa za usuluhishi bila mafanikio.

Serikali kuwa ya viwanda haimaanishi wenye viwanda ndo wawe miungu watu.

NEMC imefunga viwanda kibao tu kwa kukiuka sheria ya mazingira.

Dangote Cement mwenyewe anapigwa pin anasitisha uzalishaji itakuwa hicho kilichoajiri watu 350?
 
Madiwani ni watu wajinga sana tena ccm.
Nishangaa kuona wamepanga tozo za uchafu ambazo unaweza kucheka sana yani anayezalisha taka nyingi mfano gengeni 3000,hotelini 5000 ila mwenye duka mfano kibanda cha mpesa 10000,maduka ya jumla 10000 ambayo kuzalisha takataka ni ngumu kama depo ya vinywaji vya jumla nao 10000.
Sasa unategemea watu wwnaojua kusoma na kuandika tu Kama kigezo Cha kuchaguliwa watapanga Mambo gani ya maana
 
Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na wewe kwamba kiwanda hicho kunichangia 30% ya mapato ya halmashauri na bado madiwani na viongozi wengine wanataka kukiondoa.
 
30% ya mapato ya mufindi hivi unajua pato la Mafinga kwa mwaka?
Hapo kuna figisu ila sio kwa kusema hicho kiwanda kinatoa 30% ya pato la Mafinga!
Yaani hicho kiwanda ni zaidi ya mashamba ya chai UNILEVER, ni zaidi ya hao vigogo wote wa Sao Hill.

Mleta mada anafikiria watu wote humu ni wa Dar au Kasulu au Nanjilinji 😅

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Mkuu mbona post yote imejieleza Hapo
Wanyalu kama kweli kawakosea kaleta dhuluma watamdindishia kama general Mwandindi na Kleruu..

Mleta mada hajasema huyo jamaa alifikaje hapo na kusimika kiwanda, kuna kitu hakiko sawa.
Kama aliwakodi wenye eneo afanye shughuli miaka mi3 atawarudishia, mkataba umeisha, aondoke laah arudi kwenye meza ya mazungumzo, hata mwenye gereji na nyama choma ana haki.

Kiwanda anaweza kufungua ndani huko hata Iyegeya huko yeye ni Msukuma mwenye hela. 😅

Pamoja na 'makoneksheni' hana uwezo wa kuwafanya chochote madiwani wa hapo uchaguzi ulishaisha!

Wanyalu kamwene!? Mnogageh!? Makasi

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Njaa mbaya Sana,kuna harufu ya Rushwa ndani yake hapo.Unaambiwa kuna mtu analitaka hilo eneo KWA hiyo Wao wanataka kumfanikishia huyo mtu KWA Usiri Mkubwa Ili wapate Chao...Njaa Mbaya Sanaa Aisee.Kwanini Wana CCM Tunafeli hivi
Kamwene Wanyalukolo wote wa Mufindi!! Sisi Wakabila tupo tu pembeni tukiwaangalia. 😇

Wilaya ina utajiri wa maliasili za misitu na chai, lakini barabara zake sasa!!! Mko busy tu kuitukuza CCM! Madiwani wa Mufindi wana njaa sana kiasi cha kupelekeshwa tu kama magari mabovu na wafanyabiashara wenye hela.
 
QWIHAYA -- kampuni hii imekuwepo takriban miaka 3 ikifanya Kazi katika eneo hilo na ikiwa inasambaza nguzo hizo za umeme kwa mikoa yote kwa kipindi chote hicho.

Wakati haya yakifanyika uongozi wa Halmashauri ikiwemo baraza hilo la madiwani la kipindi hicho lilikuwepo na lilikuwa likiona haya.
Mbona una-sound kama ndio ukweli wenyewe na mnaufahamu?! Mbona kama mnataka kuhalalisha kwa hoja "baraza la madiwani lilikuwepo na liliona hayo yakifanyika"?! Mmiliki halali wa kiwanja ni nani?!

Kwamba madiwani, sijui nini na nini, sio hoja kwa sababu sidhani kama viwanja vinatolewa na madiwani. Kama mlipewa hati ya umiliki na mamlaka rasmi basi mnaweza kugoma kuondoka mkianzia kwa kwenda mahakamani.

Na kama mlipewa hati na mamlaka rasmi lakini ikaja kugundulika kiwanja kilikuwa kinamilikiwa na mtu mwingine, basi hapo hamna budi kuondoka. Mnachoweza kufanya ni kuongea biashara na mmiliki halali au kwenda mahakamani kuwafungulia kesi ya madai mamlaka iliyowapa kiwanja wakati wanafahamu hicho kiwanja kinamilikiwa na mtu mwingine.
 
Nitakuwa wa mwisho kukubaliana na wewe kwamba kiwanda hicho kunichangia 30% ya mapato ya halmashauri na bado madiwani na viongozi wengine wanataka kukiondoa.
Kaka Saohill wana ekari zaidi ya 120,000 za miti, kuna makampuni makubwa kama Tanwat na kuna mashamba binafsi ,viwanda vinavyotoa mamilioni ya kodi.
Sasa unakuja kusema kiwanda kinagombana na wauza nyama choma kinatoa 30%ya pato la mji wa Mafinga?
 
Mufindi ni moja kati ya wilaya tajiri zaidi hapa nchini ipo ndani ya top five

Hii inafanya hoja yako ya kutuambia kua hicho kiwanda kilichoanzishwa miaka mitatu iliyopita eti kinachangia 30% ya mapato ya wilaya hiyo kua ni chai kama chai zingine za hapo hapo mufindi.
 
Back
Top Bottom