Mufindi: Mmiliki QWIHAYA General Enterprises atakiwa kuhamisha kiwanda ili kupisha gereji na nyama choma

mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
2,463
3,932
Sakata lake Liko hivi

QWIHAYA ni kiwanda Cha nguzo za Umeme ambacho tangu Rais, John Pombe Magufuli aagize kuanza kutumika kwa nguzo zinazozalishwa ndani ya nchi, kimefanikiwa kuongeza ajira 350 kutoka chini ya 50 kabla ya mwaka 2015, wengi kutoka ndani ya mji wa Mafinga, na Wilaya ya Mufindi kwa ujumla.

QWIHAYA General Enterprise's ni kiwanda kinachochangia asilimia 30 ya mapato katika halmashauri Mji wa Mafinga.

Pia, kiwanda kinachangia kukua kwa uchumi wa wakulima wa mazao ya misitu ambao huuza miti ya nguzo za Umeme.

Mpaka sasa QWIHAYA anamiliki viwanda Njombe, Kigoma na Kibaha ambako muda sio mrefu kitafunguliwa kuunga mkono sera ya TANZANIA YA VIWANDA.

BARAZA LA MADIWANI LA MJI WA MAFINGA LIMEMPA SIKU 14, AONDOKE KUPISHA ENEO LA GARAGE NA NYAMA CHOMA

QWIHAYA -- kampuni hii imekuwepo takriban miaka 3 ikifanya Kazi katika eneo hilo na ikiwa inasambaza nguzo hizo za umeme kwa mikoa yote kwa kipindi chote hicho.

Wakati haya yakifanyika uongozi wa Halmashauri ikiwemo baraza hilo la madiwani la kipindi hicho lilikuwepo na lilikuwa likiona haya.

Kwani baada ya kuwepo kwa baraza JIPYA kumekuwepo na sitofaham ambayo inakuwa kam muwekezaji amevamia eneo, Hana Mamlaka wala hatakiwi zaidi ya kuondoka.


Nyuma ya hii Kuna nini na kwanini imekuwa kauli ya kutoa masaa 24 imekuja ya siku 14 wakati huo wakitaka aondoke lkn Kuna kuwa na kauli ya tukae meza ya mazungumzo

Kwanini mwenyekiti wa Halmashauri alishindwa ama imeshindikana kukaa na wataalamu wake katika Halmashauri na kuyajenga kuliko kutoa matamko na masaa na siku ya kumwondoa muwekezaji?.

Je, tumeshapima athari itakayojitokeza pindi muwekezaji atakapo kuwa anahangaika na shughuli za kuhama kwake

Je, tunatambua pindi atakapo anza Kazi za kuondoka itafanya uzalishaji usimame kwanza

Kwanini isifanyike utaratibu wa kuondoa hao ambao BADO hawajafanya uwekezaji mkubwa na kma Kuna gharama basi muwekezaji akachangia na kumbadilishia matumizi yeye akaendelea na uzalishaji.

Nijambo linafanywa na Halmashauri lkn ni la kitaifa zaidi kutokana na shughuli za kampuni yenyewe.

Wenye Mamlaka wataamua sie watoa maoni na watazamaji lkn ndio walaji wa mwisho tukumbuke na hili.

Kwa Mwendo huu Tanzania ya Wiwanda Tutafanikiwa?

Rais Magufuli anasema Hili, wa chini yake Hili au ndio Tuendelee Kujifukiza!
 
Eneo hilo linaonesha kuna ujenzi ulikuwa ukifanyika ukatelekezwa, pia hicho kinachodaiwa kuwa ni gereji kinachoonekana ni machine chakavu ambazo zilitelekezwa na ambazo ni aghari kuzikarabati.

Hapa inaonekana kunawatu wanataka kuwatumia hao vijana ili walipate eneo hilo kupitia mgongo wa vijana hao.
 
Mmiliki WA kiwanda ni msukuma so nadhani aangalie namna atafanikiwa.
Imeishaaa hiyo! Yeye kuwa msukuma ndiyo imeleta msukumo tokea kwa Wanyalukolo kusema 'swela beeh'!

Mmiliki atakuwa kakaa kimabavu hapo!

Everyday is Saturday............................ :cool:
 
Kamwene Wanyalukolo wote wa Mufindi!! Sisi Wakabila tupo tu pembeni tukiwaangalia. 😇

Wilaya ina utajiri wa maliasili za misitu na chai, lakini barabara zake sasa!!! Mko busy tu kuitukuza CCM! Madiwani wa Mufindi wana njaa sana kiasi cha kupelekeshwa tu kama magari mabovu na wafanyabiashara wenye hela.
 
Imeishaaa hiyo! Yeye kuwa msukuma ndiyo imeleta msukumo tokea kwa Wanyalukolo kusema 'swela beeh'!

Mmiliki atakuwa kakaa kimabavu hapo!

Everyday is Saturday............................ :cool:
Acheni utoto na upuuzi, si kila sehemu wana ukabila kama kwenu

Hujaona sababu zilizotolewa?
 
Madiwani ni watu wajinga sana tena CCM.

Nishangaa kuona wamepanga tozo za uchafu ambazo unaweza kucheka sana yani anayezalisha taka nyingi mfano gengeni 3000,hotelini 5000 ila mwenye duka mfano kibanda cha mpesa 10000,maduka ya jumla 10000 ambayo kuzalisha takataka ni ngumu kama depo ya vinywaji vya jumla nao 10000.
 
akiweza kupush hii news ikamfikia mkulu. kama nawaona madiwani vile watakavyo nywea
Wanyalu kama kweli kawakosea kaleta dhuluma watamdindishia kama general Mwandindi na Kleruu..

Mleta mada hajasema huyo jamaa alifikaje hapo na kusimika kiwanda, kuna kitu hakiko sawa.
Kama aliwakodi wenye eneo afanye shughuli miaka mi3 atawarudishia, mkataba umeisha, aondoke laah arudi kwenye meza ya mazungumzo, hata mwenye gereji na nyama choma ana haki.

Kiwanda anaweza kufungua ndani huko hata Iyegeya huko yeye ni Msukuma mwenye hela. 😅

Pamoja na 'makoneksheni' hana uwezo wa kuwafanya chochote madiwani wa hapo uchaguzi ulishaisha!

Wanyalu kamwene!? Mnogageh!? Makasi

Everyday is Saturday................................:cool:
 
Back
Top Bottom