Mufindi: Mmiliki QWIHAYA General Enterprises atakiwa kuhamisha kiwanda ili kupisha gereji na nyama choma

Ngisibara

JF-Expert Member
Jan 2, 2009
3,091
2,000
Kama ana nyaraka halali za kumiliki eneo hilo akaweke stop order....ili apewe maelezo ya nayoeleweka ya kwa nini apishe gereji na nyamachoma!

Tatizo la wanyalu wa Mafinga ni siasa na hasa CCM, ili uweze kufanya biashara Mafinga ni lazima ujifanye wewe ni mccm kindakindaki vinginevyo utapigwa vita mpaka kwa mkeo
 

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,438
2,000
Sakata lake Liko hivi

QWIHAYA ni kiwanda Cha nguzo za Umeme ambacho tangu Rais, John Pombe Magufuli aagize kuanza kutumika kwa nguzo zinazozalishwa ndani ya nchi, kimefanikiwa kuongeza ajira 350 kutoka chini ya 50 kabla ya mwaka 2015, wengi kutoka ndani ya mji wa Mafinga, na Wilaya ya Mufindi kwa ujumla.

QWIHAYA General Enterprise's ni kiwanda kinachochangia asilimia 30 ya mapato katika halmashauri Mji wa Mafinga.

Pia, kiwanda kinachangia kukua kwa uchumi wa wakulima wa mazao ya misitu ambao huuza miti ya nguzo za Umeme.

Mpaka sasa QWIHAYA anamiliki viwanda Njombe, Kigoma na Kibaha ambako muda sio mrefu kitafunguliwa kuunga mkono sera ya TANZANIA YA VIWANDA.

BARAZA LA MADIWANI LA MJI WA MAFINGA LIMEMPA SIKU 14, AONDOKE KUPISHA ENEO LA GARAGE NA NYAMA CHOMA

QWIHAYA -- kampuni hii imekuwepo takriban miaka 3 ikifanya Kazi katika eneo hilo na ikiwa inasambaza nguzo hizo za umeme kwa mikoa yote kwa kipindi chote hicho.

Wakati haya yakifanyika uongozi wa Halmashauri ikiwemo baraza hilo la madiwani la kipindi hicho lilikuwepo na lilikuwa likiona haya.

Kwani baada ya kuwepo kwa baraza JIPYA kumekuwepo na sitofaham ambayo inakuwa kam muwekezaji amevamia eneo, Hana Mamlaka wala hatakiwi zaidi ya kuondoka.


Nyuma ya hii Kuna nini na kwanini imekuwa kauli ya kutoa masaa 24 imekuja ya siku 14 wakati huo wakitaka aondoke lkn Kuna kuwa na kauli ya tukae meza ya mazungumzo

Kwanini mwenyekiti wa Halmashauri alishindwa ama imeshindikana kukaa na wataalamu wake katika Halmashauri na kuyajenga kuliko kutoa matamko na masaa na siku ya kumwondoa muwekezaji?.

Je, tumeshapima athari itakayojitokeza pindi muwekezaji atakapo kuwa anahangaika na shughuli za kuhama kwake

Je, tunatambua pindi atakapo anza Kazi za kuondoka itafanya uzalishaji usimame kwanza

Kwanini isifanyike utaratibu wa kuondoa hao ambao BADO hawajafanya uwekezaji mkubwa na kma Kuna gharama basi muwekezaji akachangia na kumbadilishia matumizi yeye akaendelea na uzalishaji.

Nijambo linafanywa na Halmashauri lkn ni la kitaifa zaidi kutokana na shughuli za kampuni yenyewe.

Wenye Mamlaka wataamua sie watoa maoni na watazamaji lkn ndio walaji wa mwisho tukumbuke na hili.

Kwa Mwendo huu Tanzania ya Wiwanda Tutafanikiwa?

Rais Magufuli anasema Hili, wa chini yake Hili au ndio Tuendelee Kujifukiza!
Huyu ni mwajili wako? Yeye mwenyewe hiyo ardhi aliipataje?
Ajira siyo sababu ya kukiuka sheria. Afuate sheria, FINITO! KIwanda gani hicho? Kwani lazima kiwe kati ya shughuli za binadamu? Kama alikipata kwa njia za panya hiyo ndo gharama yake na kama ni sehemu iliyopangwa kwa malengo mengine tangu zamani, mwambie aondoe. Usiweke mambo ya kuunda.
 

Dadyaga

Member
Sep 16, 2020
39
125
Kamwene Wanyalukolo wote wa Mufindi!! Sisi Wakabila tupo tu pembeni tukiwaangalia. 😇

Wilaya ina utajiri wa maliasili za misitu na chai, lakini barabara zake sasa!!! Mko busy tu kuitukuza CCM! Madiwani wa Mufindi wana njaa sana kiasi cha kupelekeshwa tu kama magari mabovu na wafanyabiashara wenye hela.
mufundi yetu kila kchwa knaitukza ccm ndo maan hat maebdeleo hakun washajua wanapendwa
 

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,438
2,000
Yaani kiwanda kinachangia 30% ya mapato ya H/W halafu kinaambiwa kipishe garage?? na nyamachoma??

Tanzania ya viwanda
Muleta mada ni bwege tu! Kiwanda cha kuchemsha nguzo hakiwezi kufikia 30% ya mapato ya halmashauri. Hayo matanuru yapo kibao maeneo ya Mufindi, hilo moja ndo liingize 30%! NO! Ni muongo tu anatafuta kuungwa mkono na bhlabla za ajira.
 

libeva

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
3,406
2,000
Yawezekana mmiliki kafuatwa na madiwani awakatie hela ya posho kawakatalia
 

libeva

JF-Expert Member
Mar 25, 2015
3,406
2,000
Muleta mada ni bwege tu! Kiwanda cha kuchemsha nguzo hakiwezi kufikia 30% ya mapato ya halmashauri. Hayo matanuru yapo kibao maeneo ya Mfindi, hilo moja ndo liingize 30%! NO! Ni muongo tu anatafuta kuungwa mkono na bhlabla za ajira.
Msome tena utaelewa, usimbeze ana hoja za msingi, leta ushahidi wako kama hachangii mapato ya halmashauri ya Mufindi
 

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,438
2,000
Msome tena utaelewa, usimbeze ana hoja za msingi, leta ushahidi wako kama hachangii mapato ya halmashauri ya Mufindi
Kuchangia mapato ni sahihi lakini hakuwa na sababu ya kusema ni 30% ya mapato ya halmashauri. Muulize kama mapato ya Mufindi anayajua.
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,155
2,000
Iko haja suala hili lisiende kwa mihemko ya kisiasa kwa kuwa baraza lina mamlaka ya kusema huyu aondoke na huyu aje.

Tuanze na drawing board, ili kiwanda kijengwe na kiweze kufanya shughuli zake za uzalishaji lazima kuna mamlaka za kiserikali zimetoa vibali/leseni;
Mathalani BRELA kama ni kampuni au jina la Biashara.
TIN toka TRA kwa kuwa chanzo cha kodi kutokana na mapato kinayotengeneza.

Leseni toka Halmshauri ambapo madiwani wamekasimisha shughuli za kutaalam kwa ofisi ya biashara kutoa leseni.
Kuna kodi ya ardhi na kodi ya majengo pia.

Suala la msingi, kuna sheria/kanuni gani ambayo kiwanda kimekiuka mpaka kitakiwe kuondoka?

Ujio wa nyama choma utaingiza kiasi gani kwenye mzunguko ukilinganisha na uwepo wa kiwanda cha nguzo.

RC, DC, DED wao kama viongozi wanasimama wapi kwa kuonesha uongozi kwenye kutatua mizozo. Kama tuna nia ya kujenga uchumi wa kati kwa kutumia viwanda, nyama choma ukilinganisha na mzalishaji wa nguzo, nani anajenga uchumi endelevu na jumuishi kwenye kusisimua kukua kwa uchumi.

Tukiweza kujibu haya, tutawatia moyo watu wote wenye nia njema ya kuwa sehemu ya kujenga uchumi Tanzania.

Wasalaam.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom