Winner Magele
Member
- Jan 9, 2013
- 86
- 49
Kumekuwa na kawaida kwa watu wa music wa dansi,ambao shughuri yao huifanya katika bar na kumbi za starehe zilizopo kwenye makazi ya watu,hawa jamaa kazi yao huwa wanafanya usiku kuanzia saa tatu,mpaka saa kumi alfajiri,muda ambao wengi huwa tumerudi majumbani kwetu,na tungehitaji kupumzika na familia zetu kwa ajiri ya kujiandaa na siku nyingine,lakini imekuwa shida tunakosa muda huo kutokana na kelele za music wa hawa jamaa,kibaya zaidi hata zile siku za mapumziko,mf;juma mosi na juma pili kwao mchana ndio muda wa kujaribu vyombo kwa ajiri ya kujiandaa na show,hivyo kutunyima hata ile fulsa ya kuzungumza na wageni wetu na familia zetu,na hii imekuwa kero hata kuwafanya watoto washindwe kujisomea,cha kushangaza hawa jamaa kwao mchana ndio muda mzuri wa kulala na kupumzika,wakati sisi tukiwa makazini lakini usiku ndio muda wa "dose dose" tena kwa Fuji zote hivyo mueshimiwa Waziri nakuomba unapo shughulika na kero mbali mbali,shughulika na hili pia asante.
Last edited by a moderator: