Muendelezo wa yaliyojiri kwenye kesi ya mwanangu, wazazi msiwabane sana watoto!

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,174
2,000
Niliwahi kuleta hapa hii maada takribani miezi miwili iliyopita ila mnisamehe bure nilisahahu kuleta mrejesho

kiufupi niliitwa shuleni kama mzazi mimi pamoja na wazazi wengine, mwanangu wakimsingizia kushawishi watoto zao waache kupanda schoolbus wawe wanatembea kama mwanangu na wenzake wachache wasiopanda school bus.

Naweza kusema kesi niliishinda kirahisi mno, maana hata watoto hao wanaodhaniwa wanashawishiwa kutopanda school bus, walikiri hawajashawishiwa ila ni wao tu hawataki kupanda school bus, wao wanataka wawe wanatembea.

Licha ya hivyo wazazi walifuka na kukandia hasara za kutopanda schoolbus, point zao zilikuwa ni usalama wa watoto, watoto kuwahi kufika shule, watoto kufika shuleni wakiwa hawajachoka, nk.

Mimi point yangu ya kwanza ilikuwa kama mwanangu hajawashawishi watoto wao wasipande school bus ila ni wenyewe tu wanataka kumwiga mwanangu je mwanangu anahusikaje 😂 😂

Kiufupi nilianza kutiririka sababu za mimi kuamua mtoto wangu kutopanda school bus ( ghaama ya school bus kwangu sio tatizo kabisa)

1. Afya ya mtoto huimarika kwa kufanya zoezi la kutembea, umbali wa nyumbani hadi shuleni ni dakika kama 20 tu kwa mwendo wa kawaida kabisa, mara chache chache mimi au mke wangu tunampa lifti ya gari tunapoenda kwenye shughuli zetu

2. Kuna mamilioni ya watoto wa shule za msingi hasa za serikali huwa wanatembea kwenda shuleni, shida iko wapi mwanangu kambatana na wenzake kwenye kutembea, kuna shule ipo karibu yao ni ya serikali, wenzake wengi tu huwa wanakutana njiani na hakuna tatizo.

3. Kwa sasa naweza nikawa na uwezo wa kulipia hiyo school bus, ila hali yangu ya kiuchumi ikibadilika mtoto wangu atapata shida.

hizo ndizo zilikuwa sababu zangu, ila zaidi ya hapo, kuna mtoto flani anajiamini sana hana uwoga akaelezea sababu zake

Yeye kwa niaba ya wenzake alisema walikuwa wanapenda wanavyoona mtoto wangu pamoja na wenzake wachache wasiopanda school bus pale wakitoka shuleni, kuna shule karibu sana ya serikali kuna uwanja wa mpira, hapo huwa wakitoka shuleni wanapata nafasi ya kujumuika na wenzao wa hio shule wanacheza na kujumuika na watoto wa shule hio ya kata, si mnajua tena watoto wanavyopenda kucheza.

Lakini pia hapo uwanjani wanapokutana na watoto wengine, mwanangu na rafiki yake aliemzidi darasa moja ambae nae hapandi school bus, walijifunza sarakasi kadhaa na hata mimi nikiri tu kwamba kipaji cha sarakasi cha mwanangu si haba, sasa wakirudi hio shule yao wakianza kuruka ruka hizo sarakasi wenzao wanakusanyika kushangaa, hii nayo ndio ikawa inapelekea nao wengine kugoma

Kiufupi sababu ndizo zilikuwa hizo, lakini licha ya hivyo wazazi waliona watoto wao bado ni wadogo sana waliokuwa wakiongea utoto mwingi n.k kwa hio waliwakataza kabisa watoto zao kurudia tena kuibua upya haya mambo.

Leo nimeandika hii maada baada ya mtoto flani kuwa kiburi na kutaka kufosi nae asiwe anapanda school bus, wazazi wake wanamtandika sana lakini ikifika mida ya kutoka anakwepa school bus 😂😂 ila watoto bwana.

ni hayo tu ndugu zangu
 
Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
17,427
2,000
Niliwahi kuleta hapa hii maada takribani miezi miwili iliyopita ila mnisamehe bure nilisahahu kuleta mrejesho

kiufupi niliitwa shuleni kama mzazi mimi pamoja na wazazi wengine, mwanangu wakimsingizia kushawishi watoto zao waache kupanda schoolbus wawe wanatembea kama mwanangu na wenzake wachache wasiopanda school bus.

Naweza kusema kesi niliishinda kirahisi mno, maana hata watoto hao wanaodhaniwa wanashawishiwa kutopanda school bus, walikiri hawajashawishiwa ila ni wao tu hawataki kupanda school bus, wao wanataka wawe wanatembea.

Licha ya hivyo wazazi walifuka na kukandia hasara za kutopanda schoolbus, point zao zilikuwa ni usalama wa watoto, watoto kuwahi kufika shule, watoto kufika shuleni wakiwa hawajachoka, nk.

Mimi point yangu ya kwanza ilikuwa kama mwanangu hajawashawishi watoto wao wasipande school bus ila ni wenyewe tu wanataka kumwiga mwanangu je mwanangu anahusikaje

Kiufupi nilianza kutiririka sababu za mimi kuamua mtoto wangu kutopanda school bus ( ghaama ya school bus kwangu sio tatizo kabisa)

1. Afya ya mtoto huimarika kwa kufanya zoezi la kutembea, umbali wa nyumbani hadi shuleni ni dakika kama 20 tu kwa mwendo wa kawaida kabisa, mara chache chache mimi au mke wangu tunampa lifti ya gari tunapoenda kwenye shughuli zetu

2. Kuna mamilioni ya watoto wa shule za msingi hasa za serikali huwa wanatembea kwenda shuleni, shida iko wapi mwanangu kambatana na wenzake kwenye kutembea, kuna shule ipo karibu yao ni ya serikali, wenzake wengi tu huwa wanakutana njiani na hakuna tatizo.

3. Kwa sasa naweza nikawa na uwezo wa kulipia hiyo school bus, ila hali yangu ya kiuchumi ikibadilika mtoto wangu atapata shida.

hizo ndizo zilikuwa sababu zangu, ila zaidi ya hapo, kuna mtoto flani anajiamini sana hana uwoga akaelezea sababu zake

Yeye kwa niaba ya wenzake alisema walikuwa wanapenda wanavyoona mtoto wangu pamoja na wenzake wachache wasiopanda school bus pale wakitoka shuleni, kuna shule karibu sana ya serikali kuna uwanja wa mpira, hapo huwa wakitoka shuleni wanapata nafasi ya kujumuika na wenzao wa hio shule wanacheza na kujumuika na watoto wa shule hio ya kata, si mnajua tena watoto wanavyopenda kucheza.

Lakini pia hapo uwanjani wanapokutana na watoto wengine, mwanangu na rafiki yake aliemzidi darasa moja ambae nae hapandi school bus, walijifunza sarakasi kadhaa na hata mimi nikiri tu kwamba kipaji cha sarakasi cha mwanangu si haba, sasa wakirudi hio shule yao wakianza kuruka ruka hizo sarakasi wenzao wanakusanyika kushangaa, hii nayo ndio ikawa inapelekea nao wengine kugoma

Kiufupi sababu ndizo zilikuwa hizo, lakini licha ya hivyo wazazi waliona watoto wao bado ni wadogo sana waliokuwa wakiongea utoto mwingi n.k kwa hio waliwakataza kabisa watoto zao kurudia tena kuibua upya haya mambo.

Leo nimeandika hii maada baada ya mtoto flani kuwa kiburi na kutaka kufosi nae asiwe anapanda school bus, wazazi wake wanamtandika sana lakini ikifika mida ya kutoka anakwepa school bus ila watoto bwana.

ni hayo tu ndugu zangu
Umenikumbusha mbali sana.

Tulikua tunatembea almost 10km per day
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,440
2,000
Vitu vingine kweli ni kujiendekeza,mi pia mtoto wangu anatembea tu baada ya kubadilishiwa ratiba ya school bus kuwekewa sa 12 kasoro. Saizi anaamka saa 12 na nusu kwa raha zake. Mwanzoni alikua anaona kama hatumpendi ila saizi humwambii kitu anaona school bus miyeyusho maana yeye anafika home nusu saa au lisaa ndio school bus inapita kushusha. Siku mojamoja namsindikiza nikijiskia kumpa kampani tunapiga mastory njia nzima maana kurudi kwangu night kali washalala. Na actually ni kama mwendo wa dakika 15 hadi 20. Vitu vingine tunajiendekeza.
 
mtoto usimpe kila kitu na wala usimnyime kila kitu, hio ndio kauli yangu :)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom