Kipangaspecial
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 19,408
- 25,926
Ndugu wananchi wenzangu wa Jamhuri ya muungano wa nchi mbili, natumaini wote ni wazima wa afya na mnaendelea vizuri na majukumu yenu ya kila siku.
Siku ya leo tujadiliane kuhusu kutotolewa kwa ripoti kamili kuhusu shambulio la Mh Mbowe.
Kama tunakumbuka wiki mbili kama sio moja , mwenyekiti wa Chama cha Upinzani Mh Freeman Mbowe, inadaiwa na chama chake kuwa alishambuliwa na watu wasiojulikana.
Wakati sakata hilo likiendelea upande wa pili yaani wa CCM ukiongozwa na Job Ndugai aliyekuwa spika wa bunge la 11 waliuambia umma wa Tanganyika kwamba mh Mbowe ni mlevi na tukio lililompata ni matokeo ya mlevi.
Chadema kupitia Katibu mkuu wa chama walioita press na kuelezea kwamba ni kweli Mh Mbowe alivamiwa na alikuwa na watu kadhaa eneo la tukio.
Sasa ni muda kidogo umepita ambapo mh Mbowe ametolewa hospitali, na tunasikia akiendelea na shughuli za chama. Lakini kinachoshangaza ni CHADEMA kukaa kimya baada ya kuelezea nini hasa kilitokea siku hiyo.
Tukichukua ile taarifa ya jeshi la polisi inayosema kuwa mhe alilewa na kuwafanya wananchi wengi waamini Mbowe alilelewa hadi kufikia hatua ya kudondoka.
Je, CHADEMA hawaoni umuhimu wa kuondoa sintofahamu iliyopo miongoni mwa jamii kuhusu tukio hili?