Muendelezo wa kuwafanya watanzania wawe masikini

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,527
Kuna mpango unaratibiwa kwa ustadi mkubwa sana wa kuwa fanya wananchi masikini, lengo la mpango huu ni kuwafanya wananchi hao wawe masikini ili watawalike vizuri, sehemu zote nyeti za kiuchumi zinaguswa na kuharibiwa kwa maksudi makubwa sana, wanaofanya haya wana ajenda yao nzito, wanajua ni vigumu kumtawala mtu ambae yupo vizuri kiuchumi lakini masikini unampeleka unavyotaka.

Sehemu nyingi nyeti za kiuchumi zimeguswa sana ikiwemo madini, kilimo, mishahara, biashara kwa ujumla wake, mfano katika madini wawekezaji ambao walikuwa wanakuza uchumi wa nchi na uchumi wa eneo husika wamesumbuliwa sana hata wengine kufungasha, wananchi wamekosa ajira na maafao yao wameambiwa mpaka miaka 55 hii ni kuongeza Umasikini.

Biashara imekuwa ngumu, kodi zimezidi na kuna ubambikizaji wa kodi na makadirio yasiyoendana na hali halisi huku uwezo wa kununua toka kwa wananchi umepungua, ukiongea wafanyabiashara wengi wanasema kiwango cha mauzo katika kipindi hiki kimepungua kwa asilimia 70 mfano kama zamani ulikuwa unauza laki kwa siku sasa hivi unaweza uza 30000/= hali hii imewalazimu wengi kufunga biashara zao.

Kwenye kilimo napo wametia mguu tukianzia kwenye zuio la kuuza mazao nje, ukweli ni kwamba lengo la zuio lile lilikuwa ni kuwanyongonyesha wakulima na sio kuwasaidia watanzania, wakati wa zuio gunia moja la mahindi Kenya lilikuwa linauzwa zaidi ya laki moja, endapo mahindi yale yangeruhusiwa kuuzwa Kenya hakika mkulima wa nchi hii angeneemeka sana, matokeo ya zuio lile Kenya wakaagiza mahindi toka Mexico na Zambia matokeo yake bei ya mahindi ikaporomoka zaidi na wakulima wengi kupata hasara.

Tukibaki kwenye kilimo hapo, mazao yote muhimu yaliyokuwa yanauzwa vizuri yameharibiwa bei na watawala mfano mbaazi, na sasa ni zamu ya korosho, sio kweli kwamba wanampenda mkulima wa korosho wanataka kuharibu soko na bei nzuri ya korosho, hili ndio zao pekee ambalo lilikuwa lina fanya vizuri na kumuinua mkulima, wametia mguu na kuliharibu kwa maksudi, hakuna mfanyabiashara ambae atataka kununua korosho mwakani na wafanyabiashara hawa watafanya figisu korosho isinunuliwe nje, matokeo yake zao hili muhimu lililokuwa linawakomboa wananchi wa kusini litakufa, Umasikini.

Tugutuke sio 2020 wala 2025 maandalizi yameanza.
 
huyuu mwisho wake 2020 arudi chato kulima bustani ya urithi.
Mwisho wake hauwezi kuwa 2020, kwa tume ipi hii hii ambayo mwenyekiti ni mteule wake au? Tunae 2025 na kuendelea maandalizi yameanza, ikiwemo tia Umasikini utawale vizuri.
 
Back
Top Bottom