Muendelezo Vita Dawa ya Kulevya: Masogange apelekwa kwa Mkemia Mkuu

James7

Senior Member
Nov 2, 2010
120
80
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa Agness Gerald, maarufu Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange ambaye ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi.

Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani

"Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, " amesema Kamishna Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 349 wamekamatwa kwenye operesheni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza Februari Mosi mwaka huu.

Chanzo: Muungwana
 
Kweli awamu hii hakuna utani!!
Huu nii utani my dear!

Sisi hatuhitaji kuwajua watumiaji mbona ukipita vituo vya daladala wamejaa wengi tu tena wanabembea bila shida. Ila tunahitaji wakamatwe wauzaji na wasambazaji ili hii biashara ikome kabisa au ipungue maana wanaoumia ni vijana wenzetu na watoto wetu. So wakishampima Masogange akikutwa anatumia watakuwa wamezuia kiasi kuingia kwa madawa hapa nchini?

Huu ni utani uliotukuka!!!
 
Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa Agness Gerald, maarufu Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange ambaye ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi.

Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani

"Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, " amesema Kamishna Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 349 wamekamatwa kwenye operesheni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza Februari Mosi mwaka huu.
 
Mnhh..huyo mkemia kama wa kiume anaenda ingia majaribuni jamani.... Lile tako ....

nh.jpg
 
Kigezo gani kinatumika kuamua nani akapimwe na nani asiende kupimwa?
Samaritan hiyo inaitwa Random sampling.Ni kitu cha kawaida ukienda viwandani,migodini asubuhi huwa wanapima kilevi wakati wafanyakazi wanaingia kazini.Wanachagua holela holela wanapima kiwango cha pombe ambapo kiwango kinachokubalika ni 0% alcohol tu.
 
Kweli teknologia imekuwa sana siku hizi. Naomba ni juzwe jinsi mkemia mkuu anavyopima na kumgundua muuzaji na msafirishaji wa madawa ya kulevya.

Hili la kutumia sio tatizo kwani tunajua mtumiaji akikosa unga anakuwa amekata seal.

Na washawasha!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom