Muendelezo Vita Dawa ya Kulevya: Masogange apelekwa kwa Mkemia Mkuu

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa Agness Gerald, maarufu Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange ambaye ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi.

Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani

"Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, " amesema Kamishna Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 349 wamekamatwa kwenye operesheni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza Februari Mosi mwaka huu.

Chanzo: Muungwana
Mengine sawa ila kwenye kusafirisha hakuna uchunguzi zaidi ya ile issue ya kudakwa pale Oliver Tambo Airport akiwa misanduku ya dawa hizo akitokea JKIA hapa Dar na kufunguliwa mashtaka.
 
nh.jpg
Jf Bwana ina raha zake aiseeh
 
Kwa mkemia mkuu kufanya nini sasa? Yaani sasa tunaishia kutafuta "watumiaji". Kumbe mbwembwe na mikogo yooote bado hatuwajui wauzaji na wasambazi wakuu mpaka leo.

Usikurupuke, ACP Siro amesema anachunguzwa kwa mambo matatu, kama anauza, safirisha na ama kutumia! Wasambazaji wakuu wa nn mlipiga kelele wasitangazwe!!!
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa Agness Gerald, maarufu Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange ambaye ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi.

Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani

"Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, " amesema Kamishna Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 349 wamekamatwa kwenye operesheni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza Februari Mosi mwaka huu.

Chanzo: Muungwana

Naona kama namna ya kusafisha chombo ya mfalme wa dar, ili muache kuchonga kuwa ana upendeleo; taarifa zitarudi queen of dar yuko safi kama gwajima
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa Agness Gerald, maarufu Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukua vipimo vya damu ili kubaini kama anatumia dawa za kulevya.

Masogange ambaye ni mrembo maarufu anayetamba katika video za wasanii mbalimbali wa bongo fleva alikamatwa na polisi juzi.

Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kwamba majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani

"Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, " amesema Kamishna Sirro.

Katika hatua nyingine, Kamishna Sirro amesema watuhumiwa 349 wamekamatwa kwenye operesheni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanza Februari Mosi mwaka huu.

Chanzo: Muungwana

Wamekamatwa lakini hakuna kilichokamatwa ila utasikia kete 18. Tunataka tusikie tumekata "mzigo" kilo 10 au 30 na waliokamatwa nao ni hawa. Hii movie ni fake tupu
 
Masogange hatumii madawa masogange anauza madawa ya kulevya..hili mbn lipo wazi..kamata funga jela miaka ya kutosha tu..i wish ningekuwa IGP( in dingi voice)
 
Hivi Chidi Passo bado hajapata nauli ya kwenda kuitikia wito,aache zengwe ilala mpaka central si anatembea tu na kijua cha asubuhi
 
Sasa wanamchunguza Masogange kama anasafirisha dawa za kulevya wakati alishakamatwa akisafirisha????? Halafu miaka yote walikua wapi wakati agnes anakamtwa south Africa???

Kweli hii ndio nchi ya "UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA"..
Hayo mambo ya uchunguzi bado unaendelea itafika wakati mtu kauwawa kwa radi kisha tutaambiwa uchunguzi unaendelea kubaini kama ni radi ya mungu au ya kutengenezwa kichawi.
 
Mtumishi wa bwana huwa havunji hekaru bali hutii amri ujinga mzingo ni bora njaaa ya tumbo kuliko njaa ya akiri picha imekwisha
 
Kweli teknologia imekuwa sana siku hizi. Naomba ni juzwe jinsi mkemia mkuu anavyopima na kumgundua muuzaji na msafirishaji wa madawa ya kulevya.

Hili la kutumia sio tatizo kwani tunajua mtumiaji akikosa unga anakuwa amekata seal.

Na washawasha!
Kuna mahali tunakaribia kupoteana. Tunataka wasambazaji na wauzaji, mbona watumiaji tunao kila kona na wanajulikana waziwazi?
 
Samaritan hiyo inaitwa Random sampling.Ni kitu cha kawaida ukienda viwandani,migodini asubuhi huwa wanapima kilevi wakati wafanyakazi wanaingia kazini.Wanachagua holela holela wanapima kiwango cha pombe ambapo kiwango kinachokubalika ni 0% alcohol tu.

Unavyoelezea 'random sampling' na maana ya ''random sampling' haviendani mkuu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom